Afrika kupigana na ufisadi ni kazi ngumu sana, hata kama una uzalendo na utashi wa hali ya juu. Marais wote kabla hawajaingia kwenye uongozi wa nchi huwa kuna makada fulani ambao huwa wamegharamia shughuli yote. Chukulia Bongo kwa mfano, rais wao Magu huwa anaongea kwa ukali sana dhidi ya ufisadi, lakini mwenyewe alishasema hawezi kufukua makaburi (yaani ufisadi uliotendeka kabla yake), juzi gazeti fulani lilijaribu kutaja viongozi wa hapo awali likapigwa ban ya miaka miwili.
Ukimskliza Tundu Lissu anavyotaja ufisadi ulivyokithiri hadi leo pamoja na mikwara ya Magu hadi inakatisha tamaa.