Manifesto ya NASA na Jubilee

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,884
49,035
Kama kawaida, wanasiasa wametupea manifesto zao na uhakika ni kwamba raia wengi huwa hawazisomi. Na pia hapo tulipo sasa ni wachache watabadilisha maamuzi yao kwa kusoma manifesto. Lakini pamoja na yote, kuna wale tunazisoma na kuzidadavua.

Binafsi nimesoma zote mbili na haya hapa ndio mambo niliyoyaona humo, kuna mengine ya kawaida kama miundo mbinu sijayataja.
Wadau tunaweza tukazijadili bila mihemko ya uchama, una uhuru wa kuongeza au kunikosoa.
Nitaendelea kuongeza kadiri ninavyochambua ilani zote mbili

Raila
- Ataboresha ukulima wenye kuzingatia mifumo ya kisasa ili kuhakikisha chakula kwa wingi
- Atapigana na ufisadi na kuhakikisha maadili kwa jamii
- Atapambana na wapiga dili wale wa 10%
- Atajizuia na ukopaji wa madeni
- Ataboresha soko la ajira
- Elimu ya bure hadi kuanzia chekechea hadi sekondari
- Ataondoa jeshi la KDF Somalia
- Ataongeza idadi ya polisi

Uhuru
- Ataboresha soko la ajira
- Vijana wote baada ya chuo watapata mishahara kwa mwaka mmoja hadi pale watapata ajira, na watakua wakipitia mafunzo fulani
- Malipo ya 'Inua Jamii' yatawafikia wazee wote waliozidi miaka 70 na hawana namna kimaisha
- Elimu ya bure hadi sekondari
- Umeme kwa kila nyumba
- Boresha miradi ya unyweshaji alioanzisha ili kuhakikisha chakula
- Ataendelea kuboresha ulinzi kwa kuongeza vitendea kazi
 
Raila
- Ataboresha ukulima wenye kuzingatia mifumo ya kisasa ili kuhakikisha chakula kwa wingi
- Atapigana na ufisadi na kuhakikisha maadili kwa jamii
- Atapambana na wapiga dili wale wa 10%
- Atajizuia na ukopaji wa madeni
- Ataboresha soko la ajira
- Elimu ya bure hadi sekondari
Napata shida kidogo kujadili, ila nina maswali ambayo kama nitapata majibu naweza kuchangia vizuri.
Hebu tuanze na Raila kwanza...

-Ameeleza ataboreshaje ukulima?
-Kwa mtazamo wako, ataweza kweli kuupiga vita ufisadi?: Nauliza hivi nikijaribu kuangalia timu yake na watu wanaomzunguka (bahati mbaya siwafahamu vizuri), je, wana historia nzuri ya uadilifu?
-Atawezaje kuendesha nchi pasipo kukopa? Ameainisha vyanzo vyake vya mapato yatakayoendesha nchi bila kukopa?
-Kuhusu soko la ajira?
-Elimu bure sina comments (ingawa kiuhalisia huwa sio bure, kwa kuwa watoto wetu wanasoma kwa kodi zetu, ni namna nzuri tu ya kuzitumia kodi katika elimu)...
 
#Team_Nasa
Ha ha,nawe utapiga kura?
Raila king'ang'anizi sana,hafai.
Ameainisha njia za kuongeza mapato ili asikope?atajizuiaje kukopa?
Afahali ya Uhuru kuliko huyo jamaa ambaye anajina bora kuliko yoyote yule Kenya yote.
 
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Nampenda sana Raila na nilitamani sana awe Rais, ila kwa sasa wamwache Uhuru amalize muda wake...
 
Napata shida kidogo kujadili, ila nina maswali ambayo kama nitapata majibu naweza kuchangia vizuri.
Hebu tuanze na Raila kwanza...

-Ameeleza ataboreshaje ukulima?
-Kwa mtazamo wako, ataweza kweli kuupiga vita ufisadi?: Nauliza hivi nikijaribu kuangalia timu yake na watu wanaomzunguka (bahati mbaya siwafahamu vizuri), je, wana historia nzuri ya uadilifu?
-Atawezaje kuendesha nchi pasipo kukopa? Ameainisha vyanzo vyake vya mapato yatakayoendesha nchi bila kukopa?
-Kuhusu soko la ajira?
-Elimu bure sina comments (ingawa kiuhalisia huwa sio bure, kwa kuwa watoto wetu wanasoma kwa kodi zetu, ni namna nzuri tu ya kuzitumia kodi katika elimu)...

Hii hapa chini video yake imeelezwa kwa kina, ila hilo la vita dhidi ya ufisadi ni uwongo kwa pande zote mbili maana ukiangalia kwa mfano kuna waziri anaitwa Ngilu alitupwa nje kwa ajili ya ufisadi, halafu Raila akampokea na sasa wanatembea naye wakiisema serikali. Pia hao waliomzunguka kila mmoja wao ana daftari iliyojaa tuhuma za kila aina.

Upande wa Jubilee pia hili la ufisadi limewashinda.

Hilo la kuendesha nchi bila kukopa halikwepeki, ndio maana manifesto huwa ni sound tu za kuongea ongea. Mengine naweza kubaliana nao, yanawezekana.

Halafu pande zote mbili hawana uwezo wa kupigana na ukabila, ukiangalia NASA, viongozi hao wote kila mmoja ni kiongozi wa kabila analotoka na ndio bargaining power yake, kwamba mimi nakuja na kura milioni moja za kabila langu, hivyo mamlaka lazima nipewe zaidi.
Ndio mchezo wa Jubilee pia, leo hii rais Uhuru athubutu kumtema Ruto ndio patachimbika, maana ataagwa na bonde la ufa lote.

Hmm!... I quite agree with you... ila mnatakiwa kuchagua upande wenye afadhali...
 
Mengine naweza kubaliana nao, yanawezekana.
Nimesoma sehemu kuwa walimu wa Kenya wametilia shaka ahadi za wagombea urais wa Nasa na Jubilee kuhusu kutoa elimu bure kwa ngazi ya sekondari kama vitachanguliwa katika uchaguzi mkuu huo na kuingia madarakani. Imesemwa Umoja wa Walimu wasio wa shule za msingi nchini Kenya (Kuppet) umesema umebaki katika mashaka mazito kuhusu ahadi hiyo ukisema haitekelezeki.

Katibu Mkuu wa Kuppet, Akelo Misori alihoji inawezekanaje Serikali ikawahakikishia Wakenya elimu bure kwa ngazi ya sekondari, wakati imeshindwa kutoa elimu kwa gharama nafuu kwa ngazi ya sekondari wala elimu bure kwa shule za msingi.

Misori alisema kuwa hakubaliani nao wote; wa Nasa wala wa Jubilee wanapozungumzia elimu bure kwa ngazi ya sekondari katika ilani zao. Kutenga Sh 1,300 kwa watoto wa shule za msingi kwa mwaka mzima, limekuwa jinamizi na na hivyo ameshindwa kujua ni vipi elimu bure ya sekondari itakavyotolewa.

Akaendelea kusema hawezi kuelewa ni namna gani serikali ijayo itatoa Sh 89,000 kwa kila mtoto kwa shule za sekondari za umma na kuwa ahadi hiyo inayotolewa na wagombea wa vyama hivyo vikuu imelenga kuwavuta wananchi kuwapigia kura, lakini haina uhalisia, kwamba wanasema tu kwa sababu wanajua Wakenya wamekata tamaa na wangependa vitu vya bure. Katika hali hii elimu haiwezi kuwa bure.

Je, madai haya ya walimu yana ukweli wowote?...
 
Manifesto za pande zote mbili zin fanana more or less...sijui kwa miundo msingi zinatofautiana kivipi? kwasababu kama ni elimu ya bure hadi sekondari naona wote wanafatilia mkondo huo huo...sielewi hili swala la kukosa kukopa...
Kenyatta aliahidi Lamu port itamalizwa miaka mitano inayofuata pamja na SGR..
aliahidi pia reli mpya toka Miritini Mombasa hadi Lamu..
akaahidi pia barabara ya leni sita kwenda Mombasa
akaahidi pia barabara toka Lamu hadi Isiolo

Odinga naye akaahidi commuter rail Mombasa na Nairobi
 
Nimesoma sehemu kuwa walimu wa Kenya wametilia shaka ahadi za wagombea urais wa Nasa na Jubilee kuhusu kutoa elimu bure kwa ngazi ya sekondari kama vitachanguliwa katika uchaguzi mkuu huo na kuingia madarakani. Imesemwa Umoja wa Walimu wasio wa shule za msingi nchini Kenya (Kuppet) umesema umebaki katika mashaka mazito kuhusu ahadi hiyo ukisema haitekelezeki.

Katibu Mkuu wa Kuppet, Akelo Misori alihoji inawezekanaje Serikali ikawahakikishia Wakenya elimu bure kwa ngazi ya sekondari, wakati imeshindwa kutoa elimu kwa gharama nafuu kwa ngazi ya sekondari wala elimu bure kwa shule za msingi.

Misori alisema kuwa hakubaliani nao wote; wa Nasa wala wa Jubilee wanapozungumzia elimu bure kwa ngazi ya sekondari katika ilani zao. Kutenga Sh 1,300 kwa watoto wa shule za msingi kwa mwaka mzima, limekuwa jinamizi na na hivyo ameshindwa kujua ni vipi elimu bure ya sekondari itakavyotolewa.

Akaendelea kusema hawezi kuelewa ni namna gani serikali ijayo itatoa Sh 89,000 kwa kila mtoto kwa shule za sekondari za umma na kuwa ahadi hiyo inayotolewa na wagombea wa vyama hivyo vikuu imelenga kuwavuta wananchi kuwapigia kura, lakini haina uhalisia, kwamba wanasema tu kwa sababu wanajua Wakenya wamekata tamaa na wangependa vitu vya bure. Katika hali hii elimu haiwezi kuwa bure.

Je, madai haya ya walimu yana ukweli wowote?...

Hili la elimu ya bure inewezekana likatekelezwa, sema lengo lingekua kuwafikia Wakenya maskini. Sasa unakuta kuna wale wa uchumi wa kati tunachomeka watoto wetu humo na kufanya shughuli yote kuwa mzigo mkubwa. Wengi tunakosa uzalendo kwenye hili.

Japo NASA nawaona wana kauwongo fulani eti watatekeleza elimu ya bure ya sekondari ndani ya mwezi mmoja baada ya kuingia kwenye madaraka.

Hapo mwanzo utekelezaji wa elimu ya bure ulikumbwa na changamoto si haba, lakini taratibu zimezibwa na kumalizwa moja baada ya nyingine. Bajeti ya 2017/2018 imetenga Kshs 14b (Tshs 322b) kwa ajili ya elimu ya msingi ya bure.
 
Hii hapa chini video yake imeelezwa kwa kina, ila hilo la vita dhidi ya ufisadi ni uwongo kwa pande zote mbili maana ukiangalia kwa mfano kuna waziri anaitwa Ngilu alitupwa nje kwa ajili ya ufisadi, halafu Raila akampokea na sasa wanatembea naye wakiisema serikali. Pia hao waliomzunguka kila mmoja wao ana daftari iliyojaa tuhuma za kila aina.

Upande wa Jubilee pia hili la ufisadi limewashinda.

Hilo la kuendesha nchi bila kukopa halikwepeki, ndio maana manifesto huwa ni sound tu za kuongea ongea. Mengine naweza kubaliana nao, yanawezekana.

Halafu pande zote mbili hawana uwezo wa kupigana na ukabila, ukiangalia NASA, viongozi hao wote kila mmoja ni kiongozi wa kabila analotoka na ndio bargaining power yake, kwamba mimi nakuja na kura milioni moja za kabila langu, hivyo mamlaka lazima nipewe zaidi.
Ndio mchezo wa Jubilee pia, leo hii rais Uhuru athubutu kumtema Ruto ndio patachimbika, maana ataagwa na bonde la ufa lote.Nafkiri wote wawili, Raila na Uhuru wako na huo mtamanio kabisa ya kumaliza ufisadi, lakini hawawezi wakatekeleza hilo ikiwa wale waliowasadia kupata waadhifa huo, wale watakaowasadia kucampaign katika uchaguzi ujao, wale ambao ni ngunzo wa utawala wao wenyewe ni wafisadi.

Ni suala gumu hili.
 
Nafkiri wote wawili, Raila na Uhuru wako na huo mtamanio kabisa ya kumaliza ufisadi, lakini hawawezi wakatekeleza hilo ikiwa wale waliowasadia kupata waadhifa huo, wale watakaowasadia kucampaign katika uchaguzi ujao, wale ambao ni ngunzo wa utawala wao wenyewe ni wafisadi.

Ni suala gumu hili.

Afrika kupigana na ufisadi ni kazi ngumu sana, hata kama una uzalendo na utashi wa hali ya juu. Marais wote kabla hawajaingia kwenye uongozi wa nchi huwa kuna makada fulani ambao huwa wamegharamia shughuli yote. Chukulia Bongo kwa mfano, rais wao Magu huwa anaongea kwa ukali sana dhidi ya ufisadi, lakini mwenyewe alishasema hawezi kufukua makaburi (yaani ufisadi uliotendeka kabla yake), juzi gazeti fulani lilijaribu kutaja viongozi wa hapo awali likapigwa ban ya miaka miwili.

Ukimskliza Tundu Lissu anavyotaja ufisadi ulivyokithiri hadi leo pamoja na mikwara ya Magu hadi inakatisha tamaa.
 
It's very true!...

Huku kwetu sio kwamba Magufuli hataki kuwashughulikia waliomtangulia, lakini anaogopa kwa sababu anafikiria atakapotoka madarakani wanaweza kumshughulikia na yeye. Rejea issue ya Zambia, Chiluba alimshughulikia Kaunda, na yeye akaja akadhalilishwa na Mwanawasa. Au Malawi, Muluzi alimshitaki Banda, na yeye akaja kushitakiwa na Mutharika...
 
Back
Top Bottom