Mimi ni Mnyama, na inawezekana mwamba hapo juu ni Uto lakini alichosema ni sahihi! Katiba yetu ni ya ovyo sana! Wakati katiba ya Uto inasema Klabu ipo upande wa wanachama na Rais ndie Bosi, katiba yetu inasema Klabu ipo upande wa Simba Sports Club Company Limited, wakati Mangungu hayupo upande wa Simba Sports Club Company Limited bali yupo upande wa Simba Sports Club! Maamuzi ya Simba Sports Club yanafanyika na Bodi ya Simba Sports Club Company Limited ambako Mangungu anaingia kama Mjumbe tu! Inawezekana hujawahi kusoma katiba ya Simba lakini jiulize tu hivi kuna raha kama Kiongozi wa Klabu kuhusika moja kwa moja na usajili?! Je, kwenye usajili wa Simba umeshawahi kuona Mangungu yupo front seat? Binafsi sijawahi kuona kwa sababu hata usajili unafanywa na upande wa Simba Sports Club Company Limited, na ndo maana wanaoonekana kwenye hilo ni wale walio upande wa Simba Sports Club Company Limited kama vile Mo na Try Again wakati Uto Rais ambae ndie Bosi wa Young Africans Sports Club ndie pia anashughulika na masuala ya usajili! Hivi unafahamu hata Ahmed Ally ambae ni Msemaji wa Simba Sports Club bosi wake yupo upande wa Simba Sports Club Company Limited na sio Simba Sports Club?
Sasa tusiwe tunaongea kama watu wa Instagram au akina mama wa mtaani na badala yake tuongee kama GTs! Kwa mazingira kama hayo Mangungu unamlaumu vipi na matokeo mabaya ya Simba?