Mangula: Ndoa ya UKAWA ni feki

Mangula: Ndoa ya UKAWA ni feki

TOMEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
588
Reaction score
118
MAKAMU Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula amesema, hatua ya vyama vya upinzani vya kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuungana rasmi , Dar es Salaam si jambo jipya.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mangula alisema hii si mara ya kwanza kwa vyama hivyo kuungana na kwamba hatua hiyo haitaweza kubadilisha uwezo wa chama tawala cha CCM.

Alisema mwaka 2000 waliungana katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam na kurusha njiwa na mara ya pili walikutana hoteli ya Travertine, Magomeni katika kikao chao cha ndani na kupeperusha bendera za kuungana.

"Katika kikao hicho nilialikwa…kila mmoja alikuwa na bendera na wakakubaliana kuungana," alisema Mangula akisisitiza kuwa kama muungano huo utakuwa na nguvu ni mzuri, kwani hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema Tanzania inahitaji upinzani imara.

Alisema muungano huo wa Ukawa hauwezi kupunguza idadi ya mashina, matawi na hata kata zinazoongozwa na CCM, kwani hata katika matokeo ya uchaguzi kuanzia mwaka 1995, matokeo yake yako wazi kuwa hawakuweza.

Mangula alitoa mfano uchaguzi wa mwaka 1995 katika nafasi ya Urais, kwamba alishinda mgombea wa CCM kwa asilimia 61.8, mwaka 2000 mgombea wa CCM alishinda kwa asilimia 71 na mwaka 2005 kwa asilimia 80, jambo linaloonesha wazi kuwa muungano huo wa wapinzani, hauwezi kubadilisha chochote.

Aidha, alisema hatua hiyo ni faida kwa CCM, ambayo itakutana na wagombea wachache, wakiwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo, jambo litakalowapa urahisi zaidi wa kuchuana.

Mangula alisema CCM inatoa ofa kwa Ukawa, kuwa endapo watashindwa kumpata mgombea wa ngazi ya Urais mwenye vigezo vinavyotakiwa, wao wako tayari kuwaazima ili kuweza kujaza nafasi hiyo.

Vyama vilivyoungana juzi ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD.


Chanzo: Habari leo

My take: CCM wanajifariji lakini sasa hivi wanahaha tu sababu wanajua mwakani ndio mwisho wao.
 
Hivi vizeee vya ccm vina zeeka vibaya sana.Aendelee kuota tu.

*team ukawa*
 
CCM inaangushwa na hivi vikongwe vichumia tumbo wasipojitahidi kuwaondoa itafutika kwenye historia ya vyama vya siasa kama kanu
 
Sidhani kama suala ni uzee hapo, nadhani ni hekima ya mtu tu; kwani vinepi naunye vimeonyesha nafuu gani? Hata kuiona sura tu kwenye gazeti mimi nafunika ukurasa wote na jirani ya ukurasa huo wala sisomi chochote tena, si riziki!
 
Mimi naona kama anaongea tu,maana nakumbuka kuna kipindi amewahi toa miezi sita kwa viongozi wa ccm waliopita kwa rushwa waachie ngazi kabla hajawashughulikia leo ni mwaka wa 3 kwa hiyo kauli yake haina impact
 
Mimi naona kama anaongea tu,maana nakumbuka kuna kipindi amewahi toa miezi sita kwa viongozi wa ccm waliopita kwa rushwa waachie ngazi kabla hajawashughulikia leo ni mwaka wa 3 kwa hiyo kauli yake haina impact

Labda alitoa Miaka 6, na sio miezi 6!!
 
Hamna mtu ccm anayeweza kuongea kitu cha maana
 
Hivi mbona watu tangu juzi imekuwa UKAWA UKAWA UKAWA? Hii inamaanisha nn? Duhhhhhhh imewabamba kwa kweli!
 
Achana na Mangula, amechoka akili na mwili. Kama UKAWA si lolote si chochote si afadhali yao? Wana haja gani ya kuweweseka?
 
Mangula hana ubavu huo. Hao anaotaka watoke ndiyo waliomtoa kutoka kwenye kilimo cha nyanya mpaka kurudi mjini, halafu awatoe! Thubutu!

Mimi naona kama anaongea tu,maana nakumbuka kuna kipindi amewahi toa miezi sita kwa viongozi wa ccm waliopita kwa rushwa waachie ngazi kabla hajawashughulikia leo ni mwaka wa 3 kwa hiyo kauli yake haina impact
 
Kwa mini anakatika huku mtiwaji mwingine? Ikivunjika si ndo furaha kwake?
 
Back
Top Bottom