Manesi wa rufaa kutukana, kudharirisha wajawazito! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manesi wa rufaa kutukana, kudharirisha wajawazito!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwana wa Mungu, Mar 11, 2009.

 1. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Jamaniee, kwa wale ambao hamjaoa, tafuteni kwanza maisha hadi yawe mazuri ndo muoe, msikimbilie bila kuwa na pesa nyingi, kwasababu kwenye ndoa pesa zinahitajika sana hasa pale mwenzi wako akiwa mjamzito. kwa wale ambao wameoa, na pengine hawana pesa nyingi sana, au pengine wamezipata juzijuzi tu, wanaweza kukubaliana na mimi kuhusu lawama zangu kwa manesi wa hospitali za rufaa hapa tz.

  Kusema ukweli, tumechoka na watu hawa. wanatutukana na kutudharirisha sana wanawake tukienda kujifungua kule. Kwa wale ambao hawana habari na jinsi inavyotokea huko, ni balaa. ukienda kule, ukaona namna wamama walivyojipanga mstari kwenye vitanda vyao, wakiwa uchi wamepanua mapaja yao kule na kule huku nanihii ikiwa iko wazi kabisaa, na manesi wakiwa hata hawajali pale mmoja wao atakapokuwa tayari anatoa mtoto. mara nyingi huambiwa aendelee tu kusukuma na matusi juuu, na kuambiwa alifurahia nanilii ya mmewe kumbe hajui maumivu, anaweza akaachwa hadi mtoto anywe maji. wengine hujitahidi hadi wanachanika, si unajua tena. wenye uzazi wa kwanza ndo kabisaa, hajui, akijitahidi kama anakosea nesi anakuja anamtandika kibao kikali na kumsaidia ati anataka kuua mtoto kwanini wakati hajamsaidia hapo mwanzo. watoto wengi wanaokufa ni manesi wanasababisha hospitalini.wanaume waoneeni huruma wake zenu.

  Ukimpa Nesi kama alfu ishirini hivi, huwezi amini, wana njia zao za kusaidia kumtoa mtoto kwa mara moja tena kwa uangalifu mkubwa. utakuta wanasema huyo ni mdogo wao, na wanamtunza sana huyo mama.

  vitanda vyenyewe hamna, kitanda kimoja wanaweza wakalala wajawazito wawili. na si vitanda special kwa kujifungulia sehemu zilizo nyingi. damu zinaweza kuambukizana, ni balaa tupu. kwa wale ambao hawawezi kuwapeleka wake zao aghakan hospital kwenye malaki na maelfu huko, kwakweli wanapata shida sana. Nesi ni mfalme nchi hii kwa wanawake, hata huku majumbani tu, anaweza akakopa hadi hela kwa watu hakataliwi,kwasababu ukileta nyodo hujui utaenda hospital yao au vipi.

  hivi selikali imeshindwa kuwadhibiti hawa watu? kama hawataki kazi si waache waje manesi waadilifu na wacha Mungu? watu wanatafuta kazi kila siku mbona! hadi lini? tumechoka jamani. inasikitisha. kwanza ni udhalilishaji tosha. kwa wale wanawake ambao walishawahi kuzalia hospital za selikali wanajua hili. pamoja na kwamba humu ndani watakuwa wachache kwasababu wanawake waliomo humu wengi ni wasomi na wana afford hospital za garama. naomba selikali ilifuatilie hili.kama selikali imeshindwa, basi sisi wananchi tunaweza kulikomesha wenyewe hukuhuku mtaani...na hao manesi wataona kumbe wao ni watumishi sio mamwinyi.

  madhara mengi watu wanapata kwasababu ya kuzaa kwa shida inayosababishwa na manesi kutofanya kazi yao kule leba. watu wanachanika hadi waume zao wanawakimbia kwasababu maumbile yao yanakuwa yamepanuka(kama hawatashonwa). why? watu wanapata hata fistula, watu wanalaani kuzaa, watoto wanakunywa maji hadi wanafia mlangoni. ati jamani tusiongee hili kwasababu ni taboo? hiii taboo ambayo hatu iaddress tutaificha hadi lini wakati wanawake wanazidi kufa na watoto wetu wanazidi kufa? imagine umetunza mimba miezi tisa afu mtoto anakufa wakati wa kujifungua, au waifu wako anakufa au anaharibika sehemu za siri? tuifanye tabooo? Mungu atawahukumu ninyi manesi.
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  aroo ndugu, hili jambo ni baya sana. mikoani wanawake wengi wanakufa kwasababu hiyo. au hata hapa bongo, uliza mwanamke yeyote hospitali ya Mwananyamala au hata muhimbili leba kwao wanafanya nini. huwezi amini unayoambiwa. mimi ni mwana ume, huwa tunapigiwa stori na wake zetu jinsi kulivyo huko. sijawahi kwenda ila naamini unachosema.

  kama ulivyosema, nadhani selikali imeshindwa hili. sasa, sijui tutafanya nini. kwasababu haliishi. hakuna asiyejua hili, lakini watu wanaendelea tu kuwanyanyasa wanawake zetu.mimi kwakweli, mke wangu akinyanyaswa na nesi, akija kuniambia, uyo nesi lazima nimfate, na lazima apate adabu yake. kwasababu selikali imeshindwa,mimi nitaweza kwa mmoja mmoja. nitahakikisha hata kazi anafukuzwa. ni kweli tumechoka. nashukuru kupata wazo hilo toka kwa mmama. nafikiri wanawake wengine watatuambia zaidi kulivyo humu. chao.
   
 3. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nani alishawai kwenda mwananyamala jamani? hahaha.
   
 4. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Manesi wengi hawana maadili na wito wa kazi hiyo wapo kwa maslahi yao binafsi ya utajiri wa haraka na wengine wamebebwa tu hawaijui kazi yenyewe,serikali ifanye utafiti ili kuondoa uozo huo.
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Serikali haijali kwa kuwa hakuna haa mke mmoja wa kiongozi anayeweza kwenda kujifungulia kwenye hospitali hiyo. Au hata akienda anapata huduma tofauti na wagonjwa wengine kitu kinachowafanya waheshimiwa wasione uharaka wa kuondoa tatizo hilo.
  Ukitaa serikali ifanye utafiri wanaweza kufurahi sana kwa kuwa hatua hiyo inahusika na wao kupata fedha fulani, lakini kuondoa hali hiyo inabidi tusubiri sana, labda wakoloni warudi.
   
 6. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wanaume tena? Si umesema manesi? Au wanaume wafanyeje/wasifanyeje?
   
 7. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hili swala ni gumu sana jamani, mimi ni mwanamke mwenye watoto wawili, adha tunayoipata kule kweli ni kwa uweza wa mole ukitoka salama. Kwanza uchungu hauna adabu, huwezi sema eti nina hela basi uchungu utakuja kifedha, uchungu ni ule ule mpaka muda ule mtoto atatoka. Huko agakhan wala msikusifie kuna manezi mafilauni huwezi amini.

  Hili swala ni hulka ya mtu, kuna watu wameumbwa makatili hata ungemlipa millioni wala hawezi kuwa na roho nzuri, bila kumfanyia mwanamke mjamzito ukatili basi yeye hasikii raha.

  labda ninachoweza kusema ni kwamba, wanaume mpiganie haki ya kuingia chumba cha kujifungulia ili nanyi muwe na experience kwenye mambo hayo. Nchi zilizoendelea wanaingia huko na wanafurahi hata katika malezi inasaidia.
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu mambo mengine ni utmaduni, sidhani kama ni kunyimwa haki hiyo unayidhani hapa tumenyimwa.
   
 9. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hahaha, nchi zingine wanaingia kweli, lakini ni hivi wanakuwa mgonjwa mmoja, chumba na kitanda kimoja. lakini hapa chumba kimoja wamama kumi na tano, wote wamekaa uchi. mwanaume ataingiaje huko? si nasikia wamama wengine unamshuhudia mwenzio anajifungua wewe unaona peupee ukisubiri zamu yako? wanaume hatuwezi kuja huko. ila kwakweli tunawaonea huruma kama alivyosema mwana wa mungu, wanaume tunatakiwa tuwaonee huruma tupambane pamoja nanyi au hata kuwatisha manesi ili wawe cautious kuwa wakifanya lolote baya wanaweza kujulikana.
   
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kuna siku mambo yote haya yataisha yenyewe.
   
 11. p

  p53 JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  lawama kubwa itupiwe serikali kwa kutoijali sekta hii muhimu kwa maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii.Hawa watu wa afya ni muhimu sana.Kwa wenzetu ni watu wanaothaminiwa sana.Wanalipwa mishahara mizuri,wanawekewa mazingira mazuri ya kufanya kazi na nafasi nyingi za kujiendeleza zaidi katika fani zao.Sisi Tanzania messenger wa TRA anapokea mshahara mkubwa kuliko daktari MD wa muhimbili aliyekula msoto shuleni kwa miaka mingi(na kumbuka tunao wachache sana),sasa acha hawa manesi na hiyo mishahara yao.Mwisho wa siku huko kwenye hospitali na vituo vya afya hakutakuwa na ari ya kufanya kazi.Utafanyaje kazi kwa moyo mkunjufu huku hujui bajeti ya jioni nyumbani ikoje?
  Mnasema serikali iwafukuze,sasa ikiwafukuza hao wengine wakuja kuwa replace watatoka wapi?Cha ajabu serikali inaweza kufanya hivyo kama kipindi kile walipogoma madaktari na (kutishia) kuagiza madaktari wengine kutoka egypt/cuba kwa gharama kubwa.Kwanini msiwalipe mishahara mizuri hawa wazawa ili wachape kazi zao kwa ufanisi?
  Juzi tumeona hospitali ya temeke kinamama wazazi walivyojijaza kwenye kachumba kamoja wakati huohuo serikali iko katika mchakato wa miradi ya mabilioni ya shilingi ya vitambulisho na dowans.ndipo hapo utakaposhangaa priorities za serikali yetu!
   
 12. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33

  Mh, seems inakuuma sana, but you dont know what is happenning there, if you want to know, somea unesi huo, kafanye kazi huko wk moja, then urudi ureview article yako. Otherwise utalalamika milele. Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza!
   
 13. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Acha ujinga wewe, nani kakwambia kazi hiyo ni wito?
  Hiyo ni kazi sawa na ya kwako unayofanya, una haki ya kulipwa sawa na nguvu ulizotumia, sasa kama unamtuma mke wako akajifungulie m'mala ili usilipe hata senti, malipo ndo hayo! Usilalamike! Jiulize; uliwahi kuona nesi wa Agha Khan anamtukana mgonjwa? Watch out baby! matusi ni jadi yetu wabongo, nenda wizara zote hapa bongo ni msururu kuanzia getini, ukifika kwa bosi ndo unamsubiri masaa 4 huku umesimama, akifika hata shida yako haisikilizwi! Kwa nini mnapenda kuwa-attack watu wachache? Inawezekana baadhi yenu ndo mnakula mapato ya serikali mpaka hospitali zinakosa madawa pesa za mishahara n.k, then leo mnakuja mnalalamika!! usiwe na jazba au hasira eti utawaonyesha mmoja mmoja, umewaajiri wewe? Unawalipa? Kama unasema kodi yako, basi kawadai akina Liyumba, hakuna nesi anayekula kodi yako, kwa hiyo hata huo msaada mdogo unaoupata inabidi ushukuru, la kama hutaki mpeleke mkeo akajifungulie Tumaini ao agha khan uone kama atatukanwa. Tatizo watz tunapenda miteremko! ndo maana haya mambo yote yanatokea!
   
 14. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33

  Big up Man!

  we ndo unajua kufikiria solution ya tatizo kuanzia kwenye mzizi. Hayo malalamishi mengine ya hao wanaolalamika hayataisha mpaka serikali ikiamka na kuona umuhimu wa kuwekeza huko. Hivi kama hospitali haina vitanda,je nesi atapata wapi kitanda cha kumpa mkeo ili alalie baada ya kujifungua? Mbona watu mnafikiri kitoto kitoto jamani???????? Ah Miafrika ndivyo mlivyo!!!
   
 15. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio BONGO DALESALAMA maana sio mchezo vitu kama hivyo hawachukulii serious sijui kwa nini....Alafu mnasema bongo tambalare alaaaaa!!
   
 16. p

  p53 JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  tuko pamoja mkuu.Unajua wabongo wamezoea ile 'ngonjera' ya kazi za uuguzi na utabibu ni wito.Yaani wame cram kuwa ukitaka kufanya kazi hospitali lazima uwe na wito.Na subiri utaona watakuja hapa wito wito wito inabidi wawe na wito hata kama serikali haiwajali wito wito bla bla!wito?nini wito bana?kwenye hela kuna wito?nyinyi mbona hamna wito kwenye ofisi zenu mnakwiba kama hamna akili nzuri ila wenzenu wito,ala?wito mkubwa si ingebidi uonyeshwe na kina Chenge wenye mabilioni ya shilingi ambazo zingetumika kujenga hospitali safi za kisasa?
  acheni hizo bana!
   
 17. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  ninyi mnaosema tusiwalaumu, hivi mnafagilia utumbo wa manesi kama huo? tusiwalaumu wakati wanatuulia watu wetu? mbona nchi zingine ukienda hospitali unatamani uhamie huko huko? kuna lugha nzuri, wanakufariji, hadi unapona kwa maneno kwanza. kwani hapa bongo upigwe kwa matusi,hofu na manyanyaso? ndio utanzania? fikiri kwanza kabla ya kujadili hili. tunahitaji kubadilika. ukatili mwingine Mungu ataingilia kati siku moja. mtu huvuna kile anachopanda, ukipanda ukatili wewe au watoto wako watakuja wafanyiwe ukatili na watu wengine, ukipanda ukaribu na wema wewe au watoto wako watakuja warehemiwe au wapate mema toka kwa watu wengine. laana zingine watu wanasababisha hadi kizazi chao chote kwasababu ya roho mbaya wanazowafanyia watu wengine. Mungu anawapenda watu aliowaumba, ukiwaonea Mungu anachukia, hawezi akakuacha bila adhabu,labda utubu.
   
 18. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Mh, ni kweli kabisa mtu huvuna ulichopanda. Watanzania tumepanda wizi, ufisadi dharau na kutojali fani za kisayansi ambazo ndo zimeleta mabadiliko makubwa duniani kote, na nchi zilizoendelea 'zimetoka' kwa kuthamini wanasayansi(na si kuwakumbatia wanasiasa wezi mafisadi n.k) Sasa mavuno yake ndo hayo! Mnalalamika nini??? Tulia mnyolewe!! Ala!!!!
   
 19. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  tuzidi kuwafichua hawa watu, wanauwa wanawake wetu mno hapa tz. siku ya utepe mweupe ihakikishe inaweka mikakati kulikabili hili. nafikiri iko karibu.
   
 20. Novatus

  Novatus JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 28, 2007
  Messages: 331
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hoja hii ni nzito. Sikatai kuwa kuna adha hospitali kuhusu manesi. Ila kujumlisha moja kwa moja kuwa hii ni tabia ya manesi nikutowatendea haki. Mazingira yenyewe ya kazi nimagumu isivyo kifani. Nawauliza nyie wasomaji kam unaona kichefu chefu kugusa kinyeshi chako mwenyewe je huy nesi ambaye kucha anakutana na vinyeshi mablimbali, Siku hizi kuna ukimwi manesi hawa wanapambana na madamu ya watu wanahatarisha maisha yao. haya yote hawajakataa kufanya kazi, tafadahali acha kukatisha tamaa watu kwa sababu ya wachache wanaofanya ndivyo sivyo. Hivi mtoa haja anataka nesi aapanue hospitali?? Kwa taarifa kuna hospitali zinazalisha hadi wanawake 50 kwasiku na ni wsatani wa manesi wsiozidi 10tu. Matatizo mengine ni ya serikali kwa kutotoa kipaumbele kwa matumizi. shangingi moja lina uwezo wa kujwnga wodi ya kutosha wanawake hamsini.

  pongezeni manesi kwa kazi yao sio kuwatwisha lawama sizo na msingi
   
Loading...