Manesi jirekebisheni

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,280
6,684
Nakumbuka miaka mingi nyuma nikiwa mdogo, Naenda hospitali kuchoma
sindano. Nesi anakuchoma sindano huku anakubembeleza "Pole... eeh, pole
Baba'angu... utapona tu"

Manesi walikuwa wapole wenye maneno ya kuliwaza, waliwajali na kuwapenda
wagonjwa wakiwa na MAVAZI YAO MEUPE yenye kuvutia. Wengi wao walikuwa
ni manesi wenye elimu ya Darasa la saba tu lakini ajabu walikuwa vizuri utafikiri
wamepitia vyuo vya udaktari.

Walihudumia wagonjwa na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi, kama ulikuwa
hujazaliwa kipindi hicho basi nikueleze tu kuwa kipindi hicho hospitali za serikali
hazikuwa chafu kama unavyoziona leo.

Wale Manesi ambao walikuwa wanavaa mavazi meupe wakanyang'anywa mavazi
yao wakapewa hawa wa kizazi kipya, FORM FOUR ikawabeba, hapo ndipo nilipoanza
kushuhudia tabia za manesi hawa WASOMI, hawana heshima wala nidhamu
wengi wao ni wakali na wakatili. Mavazi meupe wanayovaa hayaendani na tabia zao
waulize kina mama wanaoenda kujifungua kwanza........ ni mabingwa wa matusi
Lakini nimalizie kwa kusema sio wote, wapo wastaarabu wanaotambua misingi ya kazi
zao.

Yote kwa yote lazima wakubali kuwa walimu wao halisi ni hawa wanaowakuta
maofisini hivyo musiwadharau.
 
Na ndo wanapelekea akina mama wengi kupoteza watoto wao na maisha yao wakiwa labour, ni janga sana hawa manesi wa voda fasta
 
Mleta Mada Umenena Kweli Wengine Viburi Mpaka Wanafukuzwa Kwenye Majumba Ya Kupanga.Wanavaa Suruali Zinabana Na Makalio Yenyewe Wameweka Yeast Yameumuka Wanajichubua Mpaka Mishipa Ya Damu Inaonekana.Jamani Manesi Kama Tatizo Ni Wanaume Pakeni Lotion Za Kawaida Mtapendwa Mnaharibu Ngozi Mpaka Mtu Unasisimkwa Damu.Es
 
Hii nchi list ya wenye roho mbaya ipo hivi
1:wanasiasa
2:polisi
3:manesi
4:walimu

Ila manesi wakiamua wanaweza kuwa na roho mbaya kuliko wanasiasa,ni watu wa ajabu sana.
 
DSC_5304.jpg
 
yaani haya majipu kwakweli balaa tupu
juzi kati nilifika shambani kidogo sasa wakati naenda shamba na pikipiki kutokana na utelezi nikaanguka na kuungua na exost
kuna mzee akanipa dawa ya kienyeji bahati mbaya haikunisaidia hatimaye nikarudi hapa mjini nikaona sasa niende hospitali lakini ili huduma iwe nzuri niende hospitali binafsi
nikafika hospitali moja ipo tabata aroma naihifadhi kwa jina Ebwana eeh gharama ni kubwa nikasema hilo si tatizo muhimu huduma, Nilijuuuta yaani yule nesi anasafisha kidonda kama anapiga msasa kwenye ubao wa mninga,
haangalii namna mgonjwa anavotaabika ni sura mbuzi na utadhani uliwahi kumpiga kibuti, kwakweli hawa watu wajirekebishe kabisa
 
Hii nchi list ya wenye roho mbaya ipo hivi
1:wanasiasa
2:polisi
3:manesi
4:walimu

Ila manesi wakiamua wanaweza kuwa na roho mbaya kuliko wanasiasa,ni watu wa ajabu sana.
Nakinzana na wewe mkuu, namba 1 ndo tatizo la roho mbaya..hao 2 hadi 4 wanapandikizwa roho mbaya na hawa namba 1.
 
Nakumbuka miaka mingi nyuma nikiwa mdogo, Naenda hospitali kuchoma
sindano. Nesi anakuchoma sindano huku anakubembeleza "Pole... eeh, pole
Baba'angu... utapona tu"

Manesi walikuwa wapole wenye maneno ya kuliwaza, waliwajali na kuwapenda
wagonjwa wakiwa na MAVAZI YAO MEUPE yenye kuvutia. Wengi wao walikuwa
ni manesi wenye elimu ya Darasa la saba tu lakini ajabu walikuwa vizuri utafikiri
wamepitia vyuo vya udaktari.

Walihudumia wagonjwa na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi, kama ulikuwa
hujazaliwa kipindi hicho basi nikueleze tu kuwa kipindi hicho hospitali za serikali
hazikuwa chafu kama unavyoziona leo.

Wale Manesi ambao walikuwa wanavaa mavazi meupe wakanyang'anywa mavazi
yao wakapewa hawa wa kizazi kipya, FORM FOUR ikawabeba, hapo ndipo nilipoanza
kushuhudia tabia za manesi hawa WASOMI, hawana heshima wala nidhamu
wengi wao ni wakali na wakatili. Mavazi meupe wanayovaa hayaendani na tabia zao
waulize kina mama wanaoenda kujifungua kwanza........ ni mabingwa wa matusi
Lakini nimalizie kwa kusema sio wote, wapo wastaarabu wanaotambua misingi ya kazi
zao.

Yote kwa yote lazima wakubali kuwa walimu wao halisi ni hawa wanaowakuta
maofisini hivyo musiwadharau.
Thread hii ipo biased,umezungumzia wauuguz kuwa wa kizazi kipya ila haujazungumzia kuwa pia wagonjwa na wao pia ni wa kizazi kipya
Wauguuz chapen kaz,mteja akiwa mkorofi usimwache akatamba
Kwa kukumbusha tu ujue kuwa kwa idadi ya wagonjwa kwa muuguz mmoja kuhudumia kwa siku ni kubwa sana tena sana so obviously watapata work overwhelmed na ukiwa nayo hii huku ukiendelea na kaz lazima uwe na hasira
 
Mbona Hospitali binafsi wako vizuri?
 
Kazi ya uhudumu wa afya hapo zamani ilikua ni wito lkn siku hizi wapo kutafuta pesa wito hakuna tena...
 
Thread hii ipo biased,umezungumzia wauuguz kuwa wa kizazi kipya ila haujazungumzia kuwa pia wagonjwa na wao pia ni wa kizazi kipya
Wauguuz chapen kaz,mteja akiwa mkorofi usimwache akatamba
Kwa kukumbusha tu ujue kuwa kwa idadi ya wagonjwa kwa muuguz mmoja kuhudumia kwa siku ni kubwa sana tena sana so obviously watapata work overwhelmed na ukiwa nayo hii huku ukiendelea na kaz lazima uwe na hasira
Jumlisha na mineno mbofumbofu ya wagonjwa wa siku hizi sasa,zamani nani alithubutu kumtusi nesi? Ukiingia tu unaanza "nihududumie bana,bila sisi utakula wapi,nitampigia simu mkuu wa mkoa sasa hivi" anyway aliyewahi kumwambia nesi asante kwa huduma anyooshe mkono juu.
 
Mbona Hospitali binafsi wako vizuri?
Najua hata wewe huko hautaweza kuwa mgonjwa mkorofi kwa sababu unatoa pesa ndefu.Vituo vya afya na zahanat vya serikali ndo sis huwa wakorofi kwa sababu bei ya matibabu n ndogo
Pili kule wapo kipesa zaid wakat serikalin wanatoa huduma so utabembelezwa sana na kumbuka private kuachishwa kaz haitaj kikao cha madiwan
 
Back
Top Bottom