Maneno ya Mzee Mahimbo yaelekea kutimia CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno ya Mzee Mahimbo yaelekea kutimia CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungurampole, Oct 16, 2011.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Amini usiamini yale aliyongea yule Mzee Mahimbo katika Mdahalo Dar na baadaye tukasikia ameaga dunia yanatabiriwa hata na makada wa CCM sasa- pata uhondo

  Leon Bahati Saturday, 15 October ‘11(MWANANCHI)


  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais Jakaya Kikwete ametekiwa kufumba macho na kufanya uamuzi utakaosababisha chama hicho kisambaratika ili kizaliwe upya.

  Bila hivyo, CCM ikiendelea na mwenendo wa sasa, imefananishwa na muathirika wa virusi vya Ukimwi ambaye hatumii dawa za kurefusha maisha, na matokeo yake kwenye uchaguzi mkuu, 2015, kitawaachia kiwepesi wapinzani kuichukua Ikulu.

  Hayo yamesemwa na Kada wa CCM ambaye aliwahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama na Serikali, Lepilal Ole Moloimet, kwenye mahojiano maalumu kuhusu miaka 50 ya uhuru wa Tanzania na mustakabali wa mvutano ndani ya chama hicho tawala.

  "Kama (CCM) inataka ishinde uchaguzi 2015 inatakiwa sasa izaliwe upya. Ipasuke, iundwe upya," alisema Ole Moloimet ambaye alisema yeye ni mwanachama wa kufa na kuzikwa CCM kwa kuwa anaamini ndicho chenye sera nzuri kuliko vyote.

  Alisema viongozi wengi waliopo serikalini pamoja na CCM ndio tatizo kwa sababu hawana maadili.Alipoulizwa kama haoni Rais Kikwete akitumia nguvu anaweza kusababisha mvurugano zaidi ndani ya chama na serikali yake, alisema:

  "(Baadhi ya) Viongozi waliopo sasa ndio tatizo, hivyo ni lazima Rais Kikwete kufumba macho na kutumia madaraka aliyo nayo, kuwaondoa wote."

  Alieleza hakuna la kuficha kwa sababu viongozi wonaolipeleka pabaya taifa pamoja na CCM wanafahamika."Anachotakiwa kukifanya Mheshimiwa Rais Kikwete ni kuwashangaza Watanzania kwa kusambaratisha wote maana wanafahamika," alilalamika Moloimet.

  Katika kutekeleza hilo akasema, "Lazima aanze ndani ya serikali na baadae CCM."

  Ole Moloimet ambaye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya na mbunge wa Monduli, kabla ya anayeishika nafasi hiyo kwa sasa, Edward Lowassa, alisema CCM isipokubali kupasuka na kuundwa upya, matatizo yakle ya baadae ni makubwa.Alielezea kuwa katiba ya CCM pamoja na sera zake ni nzuri kuliko za vyama vyote ila chama pamoja na serikali yake vinakabiliwa na wimbi kubwa la viongopzi wasiowaadilifu.


  Moloimet ambaye kwa sasa anaishi mkoa wa Arusha, alisema matatizo mengi yanayowakumba Watanzania yanatokana na viongozi wasio waadilifu."Angalia matatizo ya Dowans, anfalia matatizo ya ununuzi wa rada, angalia IPTL, angalia matatizo ya umeme, sukari, maisha magumu, yote hayo ni kukosekana uadilifu wa viongozi," alidai Moloimet.

  Chimbuko la mmomonyoko wa maadili
  Alisema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyeongoza Serikali ya awamu ya Kwanza, aliweka misingi imara ya umoja wa kitaifa na uadilifu.

  Alisema serikali hii ya awamu ya nne ndiyo iliyoonekana kufuta kabisa misingi hiyo kwa sababu tofauti na enzi za Nyerere, viongozi wa sasa wamekuwa wabinafsi kupindukia na wanajali maslahi yao tu.

  "Hivi leo, viongozi wengi ni watu waliokithiri katika umimi na siyo sisi... Nchi inaporwa," alisema huku akionya:

  "Hatutafika 2015 sababu kizazi cha sasa kimeamka. Wenyewe nao watakataa. Hii ni hatari. CCM lazima ichukua tahadhari mapema."

  Chimbuko la tatizo hilo linaloitafuna CCM pamoja na serikali yake, Moloimet alisema linatokana na serikali ya awamu hii kuingia madarakani ikiwa na kundi lililokuwa na urafiki pamoja na ulipaji wa shukurani kwa waliofanikisha ushindi.

  "Ni hatari sana kila mtu alikuja na marafiki zake. Ni athari kubwa kila mtu alikuja na marafiki zake. Baadhi ya walioshinda ndani ya CCM walitokana na kauli za chagua huyu, chagua yule. Wote ni wangu," alidai Moloimet.


  Atahari zake ndani ya CCM
  Hali hiyo aliielezea kuwa imeiathiri CCM hasa klwenye vikao vya kuamua mambo muhimu yenye mustakabali mzuri kwa chama hicho ambacho kimeitawala Tanzania tangu kilipozaliwa mwaka 1977.

  "Hivi sasa ndani ya vikao vya CCM hakuna anayethubutu kusema ukweli, wanasita, wanaogopana," alidai Moloimet ambaye anajivunia kuwa ni mmoja wa waasisi wa chama hicho ambacho anasema ataendelea kukipigania hadi kinyooke.

  "Wanaogopana kwa sababu waliingia kirafiki," alidokeza akitoa mfano wa mkoa wa Arusha kuwa ndio chama hicho kimesambaratika kutokana matatizo ya uongozi.

  Hali hiyo, alisema ndiyo ilisababisha CCM kukosa nguvu na kuiwezesha Chadema sasa kuwa na nguvu.

  Uvuaji gamba CCM

  Moloimet ambaye kwa sasa anajishughulisha na ufugaji, alimsifu Katibu wa Itikadi na Unezi, Nape Nnauye kwa kuwa kiongozi pekee wa juu anayethubutu kuwasema hadharani viongozi wasio waadilifu.

  "Nnauye ni kijana mwadilifu na ndiye pekee namuona huko juu anawanyooshea vidole. Pengine ni kutokana na uadilifu wake ndani ya chama," alisema.

  CCM mpya
  Moloimet alisema jambo la msingi baada ya CCM kuzaliwa upya ni kuweka misingi mipya ya kuhakikisha viongozi wote ndani ya chama hawawi na kofia mbili kwa wakati mmoja.

  Akatoa mfano kuwa "Mwenyekiti wa chama (Taifa) aiswe rais. Ukitenganisha vyeo hivyo itakuwa rahisi mmoja wao akikosea atabannwa."

  nawasilisha
   
 2. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kweli kwamba wengine wote ndo wabaya isipokuwa huyo JK. Chombo kinapokwenda mlama lawama ni kwa nahodha tusidanganyane bwana, JK ndo tatizo.
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Aende zake huyu dingi na roho mbaya yeke alipokuwa DC kule Rombo. Hivi huyu mzee ugonjwa wake wa mguu umepona? Na aache tabia yake ya kuomba omba ofa za bia. Anaboa sana huyu dingi kwa kudai ofa za bia hasa kwa anaojuana nao.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  ccm has reached a point of no return..............................there is nothing anyone can do to salvage what is left of her knowing she is already in the slaughterhouse by now............
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  wamuondoe na moloimet basi. Na katika kauli zake sijaona usafi wa jk wala umahiri wa nape. Aseme tu chama chote kimeoza na wala asiwatetee hao
   
Loading...