Maneno mazuri na Shule ya maisha katika biblia

Maneno mazuri na Shule ya maisha katika biblia

Vi rendra

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
3,313
Reaction score
5,730
Habari ya saa hiu wana jf
ningependa kwa yoyote mwenye mistari mizuri ya biblia yenye kutia moyo,kufundisha,hekima nk
aitupiemo kwenye mada hii


Mathayo 6 :25 - 35


25 “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi?26 Waangalieni ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si wa thamani zaidi kuliko ndege? 27 Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?

28 “Na kwa nini mnahangaikia mavazi? Angalieni maua ya mwi tuni yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayashoni nguo. 29 Lakini nawaambia, hata mfalme Sulemani katika ufahari wake wote hakuwahi kuvikwa kama mojawapo la maua hayo. 30 Lakini ikiwa Mungu anay avisha hivi maua ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavisha ninyi vizuri zaidi, enyi watu wenye imani haba? 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32 Mambo haya ndio yanay owahangaisha watu wa mataifa wasiomjua Mungu; na Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji yote hayo. 33 Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa.34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”
 
Kweli kabisa lakini kufanya kazi za halali ni muhimu wakati tukimtegemea MUNGU.

MUNGU anapenda tujitahidi kwa maarifa yetu yote na nguvu zetu zote aliyotujaalia kwenye maisha yetu halafu tunaposhindwa kabisa ndio huwa anafanya miujiza yake.

Lakini hata wakati wa tukitumia maarifa yetu na nguvu zetu lazma mwanzo tuwe tumeshamtanguliza MUNGU.
 
Kweli kabisa lakini kufanya kazi za halali ni muhimu wakati tukimtegemea MUNGU.

MUNGU anapenda tujitahidi kwa maarifa yetu yote na nguvu zetu zote aliyotujaalia kwenye maisha yetu halafu tunaposhindwa kabisa ndio huwa anafanya miujiza yake.

Lakini hata wakati wa kutumia maarifa yetu na nguvu zetu lazma mwanzo tuwe tumeshamtanguliza MUNGU.
ni kweli
ila mm napenda mistari ya mafunzo ya maisha
 
Kumb la torati 8: 10 Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa.
11 Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo. 12 Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; 13na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka; 14 basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; 15 aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, 16 aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako. 17 Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
 
Back
Top Bottom