Maneno matamu;utekelezaji dororo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
CCM kama chama tawala Tanzania kina mvuto wake. Hasa katika misemo, kauli mbiu na majina ya ajenda za kimaendeleo. Nitagusia chache chamani na Serikalini. Laiti kama uvutizi wa mambo hayo ungefanyika ipasavyo ardhini,nchi hii ingekuwa mbali kimaendeleo na kisiasa.

Kulikuwa na MKUKUTA na MKURABITA. Kwasasa hata virefu vyake nimesahau. Mniwie radhi kwa hilo. Ni kwakuwa programu hizo zimedorora na kusahaulika-hasa na wananchi. Programu hizi 'ziliuzwa' sana mwanzoni hadi kuonekana ni mkombozi wa wananchi wa kawaida. Halafu,kimyaaaaaaaaaaaa

CCM yetu ilishinda kwa wingi wa kura 2005 na 2010 kwa misemo vutizi ya kikampeni. 2005 ilikuwa:Ari Mpya,Nguvu Mpya na Kasi Mpya.2010 ikawa: Ari Zaidi,Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi. Kimsingi,misemo tajwa ilimaanisha kuimarishwa kwa nyanja za kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni. Lakini,kila mtanzania ni shuhuda wa kinachoonekana na kuendelea nchini. Vivutio vinageuka vilio!

Chamani kulikuwa na 'kuvua gamba'. Kwamba, chama kinajiweka kwenye muonekano mpya. Muonekano wa kukubalika upya kwenye jamii kwa kujisafisha.Kujisafisha kwa kujiondoa madoa na mawaa juu yake. Kwa kuwatoa chamani waharibu-taswira wa chama. Mafisadi papa. Watatu kwanza. Taifa linawajua.Siku 90 zikatolewa. Hadi leo kimyaaaaaaa

Kilimo Kwanza. Hata sijui nini hasa kinachoendelea na kilichotokea. Samahanini watanzania wenzangu kwakuwa nimekuwa mzembe 'kuappreciate' juhudi za chama changu na Serikali yangu za kutuletea maendeleo kupitia kilimo. Lakini, angalau bado nasikia kugawiwa kwa mbolea ya Minjingu. Kilimo lakini bado duni. Hakiko mbele. Si cha kwanza. Ningeruhusiwa ningesema: Kilimo Nyuma

Kati ya vipyavipya, ipo 'Big Results Now'. Ni juu ya uimarishaji wa elimu katika nyanja zake zote muhimu. Wahadhiri/Wakufunzi/Walimu, wanafunzi, miundombinu ya kieleimu na kadhalika. Sielewi 'Now' ni 'Now' ninayoijua au nyingineyo. Kama kwa miaka yote mipango ya kuendeleza elimu imesuasua,itakuwaje 'Now' kwa haraka hivi?

Pia, kuna Sera ya Mafuta na Gesi. Hii imezaliwa na changamoto zilizoibuka Mtwara. Sera inadadavua jinsi nchi itakavyosimamia sekta ya mafuta na gesi kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla. Jinsi vitalu vitakavyopatikana. Hata kabla ya utekelezaji hasa,tayari kuna sarakasi juu ya Sera husika. Sarakasi za kitajiri.Za kimamlaka. Watanzania wa kawaida wanatazama tu.Hawana msemo. Hawashangilii wala hawachukii.

Juzijuzi hapa imeibuka ya 'Mawaziri Mizigo'.Hii imeibuliwa chmni tena kwenye mkutano mmojawapo wa hadhara wa Sekretarieti ya CCM yetu. Kwamba,kuna Mawaziri hawafai.Si watendaji wazuri. Ni mizigo. Chama kimependekeza kwa Rais awaondoe madarakani. Tunasubiri

Nimejaribu kutafakari tu waungwana.Nanyinyi mwaweza kuwa na yenu. Karibuni tujadili kwa mustakabali wa Taifa letu

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
umejiandaaje kungolewa kucha na meno bila ganzi Xmas hii mzee wetu..
hao CCM hawaeleweki na kwa sasa wameshaona wako ukingoni
mbinu zao za kudanganya zimeshaisha.
Kinasubiri kuzikwa.
 
elimu bure kwa kila wtz= uzembe wa kufikiri
treni ya dakika5 mpaka 30 dar-mwz mmhh!!
Mitambo ya gongo kwa maendeo ya walevi na kulipa fadhila kwa wazee wa viroba kwa kutoa kampani kwa mzee wa mdomo upande
ruzuku hatuchui ila watu wachangie kama kanisa mmh!! Tukitakia kilale mahala pema chama hichi.
 
Back
Top Bottom