Maneno ambayo sio mazuri kuyasema misibani

Mama mmoja mwenye umri wa miaka 27 aliyekuwa karibu kufa na kuacha watoto wake watatu alimwambia hivi mtawa Mkatoliki: ‘Usije hapa kuniambia eti haya ni mapenzi ya Mungu kwangu. Ninaudhika sana mtu anaponiambia hivyo.’ Lakini, hivyo ndivyo dini nyingi hufundisha kuhusu kifo—kwamba Mungu huchukua watu ili wakakae pamoja naye.

Lakini Je, Muumba ni mkatili sana hivi kwamba angetuua bila kujali, huku akijua kwamba kifo hutuhuzunisha? La, Mungu wa Biblia hawezi kufanya hivyo. Kulingana na andiko la 1 Yohana 4:8, “Mungu ni upendo.” Ona kwamba andiko hilo halisemi Mungu ana upendo wala halisemi Mungu anapenda, bali linasema Mungu ni upendo. Upendo wa Mungu ni mwingi, halisi, na mkamilifu. Upendo huo hudhihirishwa sana katika utu na matendo ya Mungu hivi kwamba tunaweza kusema kwa kufaa kwamba yeye ni mfano halisi wa sifa ya upendo. Mungu kama huyo hawezi kuchukua watu kupitia kifo ili wakakae pamoja naye.

Dini zisizo za kweli zimefanya watu wasielewe hali ya wafu na mahali wanapoenda baada ya kufa. Inaaminika kwamba watu huenda mbinguni, motoni, purgatori, au Limbo baada ya kufa. Baadhi ya sehemu hizo hazieleweki na huogopesha sana. Lakini Biblia hutuambia kwamba wafu hawajui neno lolote; ni kana kwamba wamelala usingizi. (Mhubiri 9:5, 10; Yohana 11:11-14) Hivyo, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kinachotupata tunapokufa, kama vile tu hatungekuwa na wasiwasi kuona mtu amelala fofofo.
We utakuwa shahidi wa yehova sio bure
 
We utakuwa shahidi wa yehova sio bure
hakuna mkatoliki mwenye imani hiyo_usitudanganye
Mkuu, mimi ni Mkatoliki kimsingi.
Lakini kuwa Mkatoliki hainifanyi nisijifunze ama kusoma makala pamoja na maandiko kadhaa yanayo muhusisha Mungu na kifo.

Kwamfano nilipo soma kitabu cha Death—kinasema The Final Stage of Growth. Maneno hayo yanadhihirisha ile imani kwamba kifo ni tukio la kawaida, mwisho wa viumbe wote walio hai. Imani hiyo imefanya watu wawe na tabia ya kutumia fursa yoyote inayotokea ili kujinufaisha.

Lakini je, kwa kweli kifo ni mwisho wa uhai? Si watafiti wote wanaoamini jambo hilo. Kwa mfano, Calvin Harley, mwanabiolojia anayechunguza hali ya kuzeeka kwa binadamu, alisema katika mahojiano fulani kwamba yeye haamini kwamba wanadamu “wamekusudiwa wafe.” Mtaalamu wa kinga ya mwili, William Clark alisema: ‘Si lazima tufe.’ Naye Seymour Benzer kutoka Chuo cha Tekinolojia cha California anasema, ‘hatuwezi kusema kwamba kuzeeka ni jambo lisiloweza kuzuiwa, bali ni mfululizo wa matukio tunayoweza kubadilisha.’

Wanasayansi hushangaa wanapochunguza maumbile ya wanadamu. Wanakuta kwamba tumeumbwa tukiwa na uwezo mwingi sana wa kufanya mambo. Tunatumia tu kiasi kidogo sana cha uwezo huo katika kipindi cha miaka 70 hadi 80 ambacho tunatazamia kuishi. Kwa mfano, wanasayansi wamegundua kwamba ubongo wa binadamu una uwezo mkubwa sana wa kukumbuka mambo. Mtafiti mmoja alikadiria kwamba ubongo wetu unaweza kuhifadhi habari ambazo “zingejaza mabuku milioni ishirini yanayoweza kutoshea mojawapo ya maktaba kubwa zaidi ulimwenguni.” Wataalamu fulani wa mfumo wa neva wanaamini kwamba mwanadamu hutumia sehemu ndogo sana ya ubongo wake katika maisha yake yote. Inafaa kuuliza, ‘Kwa nini tuna ubongo wenye uwezo mkubwa hivyo ilhali sisi hutumia sehemu ndogo sana katika maisha yetu?’

Pia fikiria jinsi ambavyo wanadamu hutenda kwa njia isiyo ya kawaida wanapokabiliwa na kifo! Kwa wengi, kifo cha mke, mume, au mtoto kinaweza kusababisha majonzi makubwa maishani. Mara nyingi, hali ya watu ya kihisia-moyo huvurugika kwa muda mrefu baada ya kifo cha mpendwa. Hata wale ambao hudai kwamba kifo ni tukio la kawaida kwa binadamu hushindwa kukubali wazo la kwamba kifo chao wenyewe kitamaanisha mwisho wa mambo yote. Gazeti British Medical Journal lilitaja ‘maoni ya kitaalamu kwamba kila mtu hutaka kuishi muda mrefu iwezekanavyo.’

Tunapofikiria jinsi mwanadamu anavyokiona kifo, uwezo wake wa pekee wa kukumbuka na kujifunza, na tamaa yake ya moyoni ya kuishi milele, je, si wazi kwamba aliumbwa aishi? Kwa kweli, Mungu aliwaumba wanadamu wakiwa na taraja la kuishi milele, bali si wafe. Ona wakati ujao ambao Mungu aliwaandalia wenzi wawili wa kwanza wa kibinadamu: “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.” (Mwanzo 1:28) Huo ulikuwa wakati ujao wa kudumu ulio mzuri kama nini!
 
Hahaa_Yaani ni kama nasoma Amkenj au mnara wa mlinzi..[emoji3][emoji1][emoji1]

mwili tu ndio wa kwao wakatoliki lakini roho ya Mashahidi
 
Kuna baadhi ya maneno viongozi wa dini na watu wengi huyasema tunapokuwa misibani,Mimi naona maneno hayo sio sawa kabisa.maneno yenyewe Ni Kama "sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi","bwana ametoa bwana ametwaa"
Sababu inayofanya nione sio sawa Ni kwamba maneno hayo Ni Kama vile tunamtupia Mungu lawama kwamba ndiye amesababisha kifo lakini ukweli Ni kuwa yeye Hasababishi maovu yoyote japokuwa ameyaacha yatokee.tunasema yeye Ni mtakatifu kwa hio asingeweza kuwaua watu.lawama Ni juu yetu na ibilisi.kwa hiyo tusitumie hayo maneno ambayo yanaweza kumfanya Mungu aonekane Ana chuki na sisi.
Mimi ambaye sijawahi kuambiwa maneno haya nitaandikaje sasa?
 
Mtu unywe gongo lililochanganywa na maji ya betri hala ufe , wewe unauliza………….Kama sio Mungu embu tuambie ni nani??? Kwa hiyo una maana ni Mungu ndo kampenda Zaidi?
Mungu anaujua mwanzo wako na mwisho wako hivyo karuhusu unywe gongo na yeye ndiye aliyekuumba uwe mnywa gongo.. maana alijua kabla ata haja kuumba...

Hutaki futa
 
Una uhakika mungu hasababishi maovu
 
SI nimeshasema sio haki kumtupia Mungu lawama hizo.baba yetu wa kwanza na sisi na shetan ndio tumesababisha sisi.Mungu sio chanzo ingawa ameacha itokee hivo.kuna mambo mawili tofauti KUSABABISHA NA KUACHA ITOKEE
Kwa mujibu wa kitabu chako cha biblia, Mungu alimwambia adam kuanzia sasa utakula kwa jasho, utaugua alafu utaishi maisha mafupi hatimae utakufa

Hapo unamsingizia shetani tu, hakuna mahali shetani akitamka kua lazima binadamu nitawaua
 
Kama sio Mungu embu tuambie ni nani?
Biologically, kila chenye uhai, lazima kitafutika ktk uso wa dunia.. Hiyo ni science tu ya kawaida..! Hata miti inakatwa na kupandwa mingine.. samaki tunavua kila siku, na wengine wazaliwa.. ndio ecolojia ya viumbe hai..

hata kwa binadamu pia, tunapitia ikolojia hiyo hiyo
 
Pamoja na kuzunguka kotee kuhusu sayansi bado hujaeleza anaesimamia hiyo nidhamu ya kisayansi ni nani????

Kwa kuwa lazima awepo wa kusimamia hiyo sayansi kama unavyosema(kibaolojia)
Je huyo msimamizi wa hadi hayo yote ya uhai na kufa kutokea je anasimamia nan?
 
Ni sawa na mfano ndege idondoke na kuua watu na wengine watoto wadogo ambao ni inocent kabisa!
Halafu mtu anasema mungu anataka tujifunze kupitia hili!!

Hivi kweli Mungu awe mkatili kiasi hicho kwaajili ya kuwapa funzo watu wengine?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
umenikumbusha kitabu moja " When bad things happen to good people "

Amehoji sana hayo mambo ni kizuri mno
 
Pamoja na kuzunguka kotee kuhusu sayansi bado hujaeleza anaesimamia hiyo nidhamu ya kisayansi ni nani????

Kwa kuwa lazima awepo wa kusimamia hiyo sayansi kama unavyosema(kibaolojia)
Je huyo msimamizi wa hadi hayo yote ya uhai na kufa kutokea je anasimamia nan?
Nature ndio controller ..!
 
SI nimeshasema sio haki kumtupia Mungu lawama hizo.baba yetu wa kwanza na sisi na shetan ndio tumesababisha sisi.Mungu sio chanzo ingawa ameacha itokee hivo.kuna mambo mawili tofauti KUSABABISHA NA KUACHA ITOKEE
Kwanini aache itokee? Hajui jinsi gani tunaumia?
 
Biologically, kila chenye uhai, lazima kitafutika ktk uso wa dunia.. Hiyo ni science tu ya kawaida..! Hata miti inakatwa na kupandwa mingine.. samaki tunavua kila siku, na wengine wazaliwa.. ndio ecolojia ya viumbe hai..

hata kwa binadamu pia, tunapitia ikolojia hiyo hiyo

Science ni uwezo mdogo kwenye ulimwengu halisi
 
Mtu unywe gongo lililochanganywa na maji ya betri hala ufe , wewe unauliza………….Kama sio Mungu embu tuambie ni nani??? Kwa hiyo una maana ni Mungu ndo kampenda Zaidi?

Gongo haina uwezo wa kumuua mtu mkuu, hata risasi, sumu na kadhalika. Kifo ni zaidi na ujuavyo.
 
Back
Top Bottom