Maneno ambayo sio mazuri kuyasema misibani

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,803
Reaction score
60,649
Kuna baadhi ya maneno viongozi wa dini na watu wengi huyasema tunapokuwa misibani,Mimi naona maneno hayo sio sawa kabisa.maneno yenyewe Ni Kama "sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi","bwana ametoa bwana ametwaa"
Sababu inayofanya nione sio sawa Ni kwamba maneno hayo Ni Kama vile tunamtupia Mungu lawama kwamba ndiye amesababisha kifo lakini ukweli Ni kuwa yeye Hasababishi maovu yoyote japokuwa ameyaacha yatokee.tunasema yeye Ni mtakatifu kwa hio asingeweza kuwaua watu.lawama Ni juu yetu na ibilisi.kwa hiyo tusitumie hayo maneno ambayo yanaweza kumfanya Mungu aonekane Ana chuki na sisi.
 
Kama sio Mungu embu tuambie ni nani?
SI nimeshasema sio haki kumtupia Mungu lawama hizo.baba yetu wa kwanza na sisi na shetan ndio tumesababisha sisi.Mungu sio chanzo ingawa ameacha itokee hivo.kuna mambo mawili tofauti KUSABABISHA NA KUACHA ITOKEE
 
"Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe" haya maneno yako kwenye bible.
 
Mungu ndio chanzo cha yote, wewe, mimi, yule(shetani) hamna athari na wala hakuna mkifanyacho. Ukielewe hili hutajilaumu, hutalalamika katika maisha. Ikiwa Mungu anashukuriwa kwa mazuri kwa nini watu wasimpe lawama kwa mabaya? Majibu tafadhali
 
SI nimeshasema sio haki kumtupia Mungu lawama hizo.baba yetu wa kwanza na sisi na shetan ndio tumesababisha sisi.Mungu sio chanzo ingawa ameacha itokee hivo.kuna mambo mawili tofauti KUSABABISHA NA KUACHA ITOKEE
Yani IMESABABISHWA AU IMEACHWA ITOKEE...!! yote ni MIPANGO YA MUNGU..
 
Akifa mlevi pombe zimemuua
akifa mtumishi Mungu kampenda
sijui tunakisoea wapi ?
 
wengine wanasema "waliokuwa wanamdai marehemu wanyooshe mkono" hapo hata mzazi halisi wa marehemu atanyoosha mkono.
 
Angalia hii
Screenshot_20181209-161009.jpg
 
Ni kweli Mungu ndiye aliyekuleta na Mungu ndiye takayekuchukua. Kwa hyo Bwana ametoa bwana ametwaa ni sahihi
 
Mama mmoja mwenye umri wa miaka 27 aliyekuwa karibu kufa na kuacha watoto wake watatu alimwambia hivi mtawa Mkatoliki: ‘Usije hapa kuniambia eti haya ni mapenzi ya Mungu kwangu. Ninaudhika sana mtu anaponiambia hivyo.’ Lakini, hivyo ndivyo dini nyingi hufundisha kuhusu kifo—kwamba Mungu huchukua watu ili wakakae pamoja naye.

Lakini Je, Muumba ni mkatili sana hivi kwamba angetuua bila kujali, huku akijua kwamba kifo hutuhuzunisha? La, Mungu wa Biblia hawezi kufanya hivyo. Kulingana na andiko la 1 Yohana 4:8, “Mungu ni upendo.” Ona kwamba andiko hilo halisemi Mungu ana upendo wala halisemi Mungu anapenda, bali linasema Mungu ni upendo. Upendo wa Mungu ni mwingi, halisi, na mkamilifu. Upendo huo hudhihirishwa sana katika utu na matendo ya Mungu hivi kwamba tunaweza kusema kwa kufaa kwamba yeye ni mfano halisi wa sifa ya upendo. Mungu kama huyo hawezi kuchukua watu kupitia kifo ili wakakae pamoja naye.

Dini zisizo za kweli zimefanya watu wasielewe hali ya wafu na mahali wanapoenda baada ya kufa. Inaaminika kwamba watu huenda mbinguni, motoni, purgatori, au Limbo baada ya kufa. Baadhi ya sehemu hizo hazieleweki na huogopesha sana. Lakini Biblia hutuambia kwamba wafu hawajui neno lolote; ni kana kwamba wamelala usingizi. (Mhubiri 9:5, 10; Yohana 11:11-14) Hivyo, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kinachotupata tunapokufa, kama vile tu hatungekuwa na wasiwasi kuona mtu amelala fofofo.
 
"Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe" haya maneno yako kwenye bible.
Hapana haya maneno aliyasema ayubu lakini baadae alijutia akakiri kuwa amekosea
 
Mama mmoja mwenye umri wa miaka 27 aliyekuwa karibu kufa na kuacha watoto wake watatu alimwambia hivi mtawa Mkatoliki: ‘Usije hapa kuniambia eti haya ni mapenzi ya Mungu kwangu. Ninaudhika sana mtu anaponiambia hivyo.’ Lakini, hivyo ndivyo dini nyingi hufundisha kuhusu kifo—kwamba Mungu huchukua watu ili wakakae pamoja naye.

Lakini Je, Muumba ni mkatili sana hivi kwamba angetuua bila kujali, huku akijua kwamba kifo hutuhuzunisha? La, Mungu wa Biblia hawezi kufanya hivyo. Kulingana na andiko la 1 Yohana 4:8, “Mungu ni upendo.” Ona kwamba andiko hilo halisemi Mungu ana upendo wala halisemi Mungu anapenda, bali linasema Mungu ni upendo. Upendo wa Mungu ni mwingi, halisi, na mkamilifu. Upendo huo hudhihirishwa sana katika utu na matendo ya Mungu hivi kwamba tunaweza kusema kwa kufaa kwamba yeye ni mfano halisi wa sifa ya upendo. Mungu kama huyo hawezi kuchukua watu kupitia kifo ili wakakae pamoja naye.

Dini zisizo za kweli zimefanya watu wasielewe hali ya wafu na mahali wanapoenda baada ya kufa. Inaaminika kwamba watu huenda mbinguni, motoni, purgatori, au Limbo baada ya kufa. Baadhi ya sehemu hizo hazieleweki na huogopesha sana. Lakini Biblia hutuambia kwamba wafu hawajui neno lolote; ni kana kwamba wamelala usingizi. (Mhubiri 9:5, 10; Yohana 11:11-14) Hivyo, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu kinachotupata tunapokufa, kama vile tu hatungekuwa na wasiwasi kuona mtu amelala fofofo.
Huu mwandiko ni wa mashahidi wa jehova kabisa.
 
Back
Top Bottom