Maneno 2 yaliyoandikwa zaidi katika biblia: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno 2 yaliyoandikwa zaidi katika biblia:

Discussion in 'JF Doctor' started by Fadhili Paulo, Apr 18, 2012.

 1. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Habari great thinkers!!

  MANENO 2 YALIYOANDIKWA ZAIDI KATIKA BIBLIA:

  Inashangaza kidogo hii, hata hivyo habari ndio hiyo, ukimuuliza mtu anadhani ni maneno gani 2 yamejiruidia zaidi kuandikwa katika biblia, mara nyingi wengi wanaweza kukujibu pengine ‘Mungu au Yesu’. Utajiuliza kwanini maji yaliitwa ni UHAI?.


  Mistari miwili ya mwanzo kabisa ya biblia inasomeka hivi: ‘’Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikiuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya MAJI; ROHO ya Mungu ikatulia juu ya uso wa MAJI’’.  MAJI NDIYO KILA KITU MWILINI, BILA KUNYWA MAJI NI SAWA NA KWENDA DUKANI BILA HELA MFUKONI?!!. Si vema kuendelea kusubiri kiu ndipo tunywe maji.  ‘’Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji, hutoa ishara (indicators),tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu kwa madawa – dr. Batmanghelidj’’.  Kwamba maji tu yanaweza kukutibu, kukuponya au kukukinga usipatwe na magonjwa yote (isipokuwa tuyapatayo kwa bahati mbaya kwa ajali), linaweza kuwa kama ni maajabu hivi, bali ni ‘’common sense’’ (sipati Kiswahili chake fasaha), haihitaji kwenda chuo kikuu hii, ni kuwa tu: Bila maji, hakuna maisha.
  VITU 5 MHIMU ILI KUISHI


  1. Oksijeni 2. Maji 3. Chumvi 4. Potasiamu (chakula) 5. Mazoezi


  NI KWELI
  – Hakuna mtu anaweza kuishi bila vitu hivyo 5. Sayansi ya madawa mara nyingi hudharau namba 2 na 3 kwa malengo ya kuuza madawa na harakati za kutibu ishara za mwili kupungukiwa maji (magonjwa).  NI KWELI
  – Hakuna kitu kingine kinachoweza kuua haraka kama ukosefu wa maji mwilini.  NI KWELI
  – Watu wenye afya mgogoro mara nyingi ni wale ambao hawana mazoea ya kunywa maji mara kwa mara badala yake hupendelea kunywa vinywaji hatari vinavyokausha maji mwilini – kaffeina (chai, kahawa, soda) na/au alkoholi (pombe).  NI KWELI
  – Kiasi cha uchumvi (salinity) katika maji yaliyo nje ya seli za miili yetu ni sawa na kile kilicho ndani ya maji ya bahari!.  NI KWELI
  – Katika zama za kati za mawe, mahabusu au watu wakorofi katika jamii walisababishiwa vifo vibaya kwa kunyimwa chumvi katika vyakula vyao.  NI KWELI
  – Mahospitalini wanatengeneza pesa nyingi kwa kuuza maji yenye chumvi ndani yake (Saline 4) wanayoyaita madripu, lakini hawawaambii wagonjwa kuwa walikuwa wamepungukiwa maji na chumvi tu katika milo yao!!!  NI KWELI
  – Namna gani unaweza kutegemea makampuni ya madawa kufanya utafiti juu ya umhimu wa maji katika miili yetu wakati hawataweza kutengeneza pesa katika hilo?, nani wanafanya tafiti zitakazo wapelekea wao wenyewe kupotea katika biashara?.  NI KWELI
  – Hakuna maneno mengine 2 ambayo yameandikwa zaidi katika Biblia kama MAJI na CHUMVI.  NI KWELI
  – Mazingira ya mtoto akiwa tumboni ni MAJI na CHUMVI (amniotic fluid).  Maji ndiyo kiinilishe cha kwanza ambacho mwili hukihitaji, soma kazi 41 za maji mwilini hapa: kazi za maji mwilini | maajabu ya maji
   
Loading...