Mandela, Mkapa walivyomwangusha Nyerere

IAfrika

JF-Expert Member
Oct 4, 2014
276
217
BABA wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alimaliza siku zake za mwisho katika hali ya masikitiko kutokana na vitendo vya mwisho vya watu aliowaamini, Raia Mwemalimeambiwa.Wakati Watanzania wakiadhimisha miaka 15 tangu kufariki kwa Mwalimu katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London, Uingereza mwaka 1999, taarifa mpya zimeibuka kuhusu namna alivyotumia siku zake za mwisho.

Katika mahojiano ambayo gazeti hili pamoja na gazeti lake dada la Raia Tanzania ambayo yamefanywana watu waliokuwa karibu naye ikiwamo familia yake na watu aliokuwa akifanya nao kazi, mambomakubwa mawili yameelezwa kumuumiza Mwalimu.

Mambo hayo ni mchango mdogo wa serikali za Tanzania na Afrika Kusini kwa taasisi yake ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF) na ubinafsishaji wa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).

Mmoja wa viongozi wa MNF aliyezungumza na Raia Mwema kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema Mwalimu alihuzunika sana wakati alipokwenda nchini Afrika Kusini kutafuta fedha za taasisi hiyona kuambulia mchango kidogo sana."Wakati Nelson Mandela akiwa Raiswa Afrika Kusini, Mwalimu alikwenda kutafuta fedha kule akiwa na matumaini makubwa sana. Unajua Tanzania ilijitolea sana kwa ajili ya Uhuru wa Afrika Kusini.

"Afrika Kusini ina uwezo mkubwa wa kiuchumi. Mwalimu alitaraji makubwa sana kutokana na uhusiano baina ya nchi hizi mbili. Cha ajabu, alipokwenda kule serikali ilimpa kiasi cha dola 60,000(takribani shilingi milioni 60 wakati huo)." Hebu fikiria uwezo wa kiuchumi wa Afrika Kusini na mchango ambao Mwalimu na Tanzania kwa ujumla walikuwa nao kwa Taifa hilona halafu Mwalimu anapewa dola 60,000. Nyerere returned a broken man (Nyerere alirudi akiwa amefadhaika sana)," alisema kiongozi huyo.

Kiongozi huyo alieleza pia kwamba kwa upande wa Serikali ya Tanzania, msaada pekee ambao MNF iliupata ni kiwanja kilichopo jirani na Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kilichotolewa wakati wa Serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi, na hawakuwahi kupokea fedha yoyote kutoka serikalini hadi leo.

"Hebu fikiria, serikali yake mwenyewe ya Tanzania haikumpa hata senti moja kwa ajili ya MNF. Serikali ya Rais Benjamin Mkapa haikuwahi kumpa kitu na nafahamuserikali ya Jakaya Kikwete pia haijawahi kuchangia MNF. Hilo ndiyo tatizo," alisema kiongozi huyo.

Kutokana na hali hiyo, kiongozi huyo alimnukuu Mwalimu Nyerere akisema mwaka mmoja kabla ya kifo chake; "Siku nikifariki dunia, kesho yake tu MNF itakufa".

Raia Mwema limeelezwa pia namnawasaidizi wa karibu wa Mwalimu walivyoshangazwa na ukweli kuwa katika kitabu cha Mandela cha The Long Walk to Freedom, Mwalimu alitajwa mara moja tu kwenye kitabu hicho.

Gazeti hili linafahamu kwamba, katika kitabu hicho, Mandela alimtaja Mwalimu wakati akieleza kuhusu harakati zake za kutafuta kuungwa mkono na nchi za Afrika katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, ambapo alitembelea Tanganyika huru kutafuta kuungwa mkono.Wakati wa utawala wa Makaburu wa Afrika Kusini, ilikuwa marufuku kutaja hadharani jina la Nyerere au Tanzania kwa vile ilionekana kama ni uchochezi.

Lakini pia Makaburu walitaka kuzuia ushawishi wa Nyerere kwa watu Weusi wa kule. Ndiyo maana Mwalimu alitaraji makubwa sana kutoka huko."Ni sawasawa na utawala wa Mkapa.

Watanzania wote wanafahamu kuwa isingekuwa Mwalimu, Mkapa huenda asingeupata urais wa Tanzania. Alitaraji huyo ndiye angeisaidia MNF kuliko pengine rais yeyote. Cha ajabu, serikali ya Mkapa haikuchangia kitu.

Afadhali hata Mzee Mwinyi ambaye alichangia kiwanja," kilisema chanzo hicho chagazeti hili.

Katika mahojiano mengine ambayogazeti dada la hili, Raia Tanzania, lilifanya na aliyekuwa Katibu Myekawa Mwalimu, Samwel Kassori, ilibainika pia namna Mwalimu alivyohuzunishwa na suala la kuuzwa kwa NBC kwa mojawapo yamakampuni kutoka nchini Afrika Kusini."Lakini moja kubwa ninalokumbukani kuhusu mchakato wa uuzwaji wa benki ya NBC mwaka 1997 mwezi Aprili wakati wa utawala Mkapa ambapo Mwalimu aliwahi kulengwalengwa na machozi akipinga benki hiyo kuuzwa kwa ABSA Group kutoka Afrika ya Kusini.

"Wakati huo nakumbuka serikali ilipanga kumwandalia Mwalimu sherehe ya kitaifa ya siku yake ya kuzaliwa (birthday) ya kutimiza miaka 75 ambazo zingefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee wa Jijini Dar es Salaam, na jambo hilo lilimshtua kidogo akaniagiza nichunguze fedha hizo zingetoka wapi na kwanini afanyiwe sherehe kubwa kiasi hicho na pia tetesi zilikuwa zimezagaa kuwa NBC inauzwa.

"Wakati huo Waziri wa Fedha alikuwa Daniel Yona, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alikuwa Peter Ngumbulu na Gavana wa Benki Kuu(BoT) alikuwa Dk. Idris Rashid."Baada ya kupata taarifa za kwamba benki hiyo iko mbioni kupigwa bei, Mwalimu aliomba maelezo kutoka kwa wahusika ambao ni Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu na Gavana wa BoT."Majibu ya serikali yalikuwa kwamba NBC inauzwa kwa sababu taasisi za fedha za Kimataifa za Fedha (IMF) na Benki ya Dunia (WB)ziliagiza Benki hiyo kuuzwa."Baada ya kupata maelezo hayo Mwalimu alikasirika kweli kweli, akaniita na tukiwa nyumbani kwakeMsasani aliniagiza kumpigia simu Rais wa (WB) wakati ili azungume naye.

"Baada ya kumpata Rais huyo wa (WB) ambaye bado alikuwa akimwita Mwalimu Mr. President (Mheshimiwa Rais), alikana IFM pamoja na Benki ya Dunia kushinikiza au kutoa masharti kuuzwa kwa NBC.

"Namnukuu Rais huyo wa WB aliniambia:"Mr Kasori do me a favour could you request PresidentNyerere to come to our headquarters in Washington and read the documents from Tanzania government, they are too voluminous but will try to make executive summary of the same""Maana yake ni kwamba walitaka Mwalimu akajioonee mwenyewe nyaraka zilizotumwa katika taasisi hizo za kimataifa kuhusu uuzaji wa NBC na walisema wangelipa gharama zote muhimu za safari hiyo.

"Baada ya mazungumzo ya simu siku mbili baadaye tulifunga safari na Mwalimu hadi Washington nchini Marekani ambapo tulikutanana Rais wa WB kwa kikao cha siku nzima na kupitia nyaraka muhimu zilizowasilishwa kwao na serikali yaTanzania."Tulirudi nyumbani baada ya wiki moja na Mwalimu aliniagiza kwanza niwatafute Yona, Ngumbulu na Dk. Rashid ili azungumze nao kabla ya kukutana na Rais Mkapa.

"Basi baada ya mimi kufanya mawasiliano nao wote hakuna aliyeitikia wito wa Mwalimu "walimpuuza" na badala yake walimtuma Donald Kamori ambayealikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC."Nakumbuka vizuri kikao na Kamorikilifanyika Msasani nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, Aprili 13 mwakahuo 1997, na Kamori alikuwa mtaalamu aliyebobea katika masuala ya fedha na ndiye kati ya wataalamu wazawa walioanzisha BoT.

"Kamori akiwa na nyaraka na takwimu za kitaalamu. Alimweleza Mwalimu bila ya kuficha kuwa kuiuza NBC serikali ilikuwa inafanyamakosa makubwa katika sekta ya fedha kwa kuwa Benki hiyo ilikuwa inaendeshwa kwa faida kubwa. Uuzwaji wake ungeleta athari ya moja kwa serikali pamoja na taasisizake nyeti."Mwalimu alitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa, akasema ‘ooooh kweli nimesomesha Watanzania' alikuwa amevutiwa sana na maelezo ya kitaalamu ya Donald Kamori.

"Baada ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa Kamori, Mwalimu aliomba kukutana na Rais Mkapa na kikao kilifanyika Ikulu ambapo alitetea NBC isiuzwe kwanindiyo ilikuwa nguzo ya serikali hasawakati inapoishiwa fedha katika mambo "nyeti yanayohusiana na usalama wa nchi" ilikuwa inakopa fedha NBC.

"Majadiliano na Mkapa yalichukua muda mrefu sana kuhusu suala hilo na itoshe kusema kwamba baada ya majadiliano hayo marefu likazaliwa wazo la kugawanywa kwa hiyo na kuanzishwa kwa Benki ya NMB ambayo serikali ina hisa hadi leo."Kilichomsikitisha zaidi Mwalimu nikwamba baada ya juhudi zote hizo Kamori alifukuzwa kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa NBC na kurudishwa BoT bila kupangiwa kazi yoyote.Hakuwa na ofisi pale akifika anasoma magazeti aliyojinunulia na kurudi zake nyumbani.

"Alitishwa sana na kuhojiwa ni kwanini alikwenda kumweleza Mwalimu na kumwonyesha nyaraka za uuzwaji wa NBC kwa Benki ya ABSA ya Afrika ya Kusini?"Kamori alinipigia simu akanieleza masahibu yaliyomkuta na mimi nikaufikisha ujumbe wake kwa Mwalimu, baada ujumbe huo Mwalimu alisikitika sana, akahoji nikwanini wanafanya mambo hayo "kumfedhehesha" akiwa hai?"Huyo Kamori alikuwa mzalendo kweli kweli ni kati ya Watanzania walioipenda nchi yao.

Siku hiyo hiyo aliacha kazi akasema hawezi kupokea mshahara asioufanyia kazina akaenda kufanya kazi zake sijui kwa sasa atakuwa wapi."Sakata la kuuzwa kwa NBC kwa kweli ni kati ya mambo yaliyowahi kumchanganya akili Mwalimu na kwa upande wangu uuzwaji wa benki ile ulifungua milango ya ufisadi mwingine uliokuja kufanyikamiaka ya baadaye," alisema.

Source:
Raia Mwema
 
my friend, ukitaka kufadhili, usimfadhili mwanadamu, na kama utamfadhili usitegemee shukrani, shukrani ni kwa Mungu yeye ndiye atakulipa. ukimfadhili mwanadamu ukitegemea malipo, utasubiri sana na utalala mlango wazi. bora ufadhili hata kuku au ng'ombe kwasababu utakula nyama yake na kinyessi chao utatumia kwa mbolea ikukuzie mimea ya chakula, mwanadamu unaweza kumfadhili halafu yeye ndiye akaja kukuua (na zaidi sana hata kinyesi chake ukisikia harufu tu unakimbia, na nyama yake hailiwi).

mkapa kama hakumkumbuka fadhila za nyerere, malipo hapahapa tu. south african mandela hakumheshimu kabisa nyerere. waafrica kusini juzi hapa wamewaua watz na kuwafukuza souz kama vile wanawafukuza wasomali wanawakimbiza mtaani wamesahau kama wao juzi walikuwa manyang'au tu mbele ya mzungu na walikuwa wanang'atwa na mbwa wa kaburu na hawakutakiwa hata kujisaidia choo cha mzungu wakati tz ikiwa masikini kwasababu ya kupigania uhuru wao. usinikumbushe mimi nisije kulia mimi. tungejua, kipindi cha nyerere, tungeendeleza maisha ya raia wetu tuwaache tu wasouz wakanyagwe tu na kaburu. hawana faida kabisa kwa tz.
 
Nimesema hii kwenye uzi mwingine, Watanzania mnafaa mzinduke kutoka huu isingizi na wimbo wa jinsi mlikomboa Afrika. Tupo kwenye dunia mpya na isiyojali historia. Vijana wamezaliwa wapya ambao wanahitimu kila uchao na hamna ajira. Vijana wasiomjua Mandela wala Nyerere, wenye njaa na hasira na kila siku wanasoma kwenye magazeti kuhusu ufisadi, upendeleo na ubinafsi.

Kila siku mnatuhukumu Kenya eti hatukuhusika katika kukomboa Afrika kama nyie.
Ifahamike sisi uhuru wetu tuliupata kwa damu na jasho, tulipigana na mzungu, hatukupewa bure kama ninyi. Hivyo baada ya kuupata uhuru hatukua tena na muda kupigana na yeyote ila kuboresha uchumi.

Dunia ya sasa ina maisha magumu kwa kila mtu na nchi, serikali zinahangaika kutafuta mbinu ya kuwathibiti vijana wake kwa ukosefu wa ajira. Vijana hawa hawapo tayari kuskiliza hadithi za Mandela wala Nyerere ila wanataka ajira ama mtaji. Na ndio mnaona serikali zetu za Kenya, Uganda na Rwanda tupo mbioni kutafuta mbinu za kuungana bila kuburuzana, hamna muda wa hadithi. Nyie mumekimbilia SADC eti kwa ajili mliwasaidia kupata uhuru, mnadhani hiyo wanajali tena. Sasa hivi serikali ya Afrika Kusini ipo katika michakato kuingia kwenye biashara za hali ya juu na Kenya maana sisi hatuchelewi. Tunazunguka na kutafuta mbinu na jinsi ya kupiga hela hadi Botswana, Zambia, Musumbiji, hata Tanzania yenyewe. Ndio dunia ya sasa ilivyo.

Hivyo muache hizi hadithi na jazba, muwe wajanja wa kisasa la sivyo mfahamu vijana wenu wanaendelea kuongezeka halafu na ukosefu wa ajira, ardhi mnayo kubwa, madini, vivutio na mengi mazuri, hivyo vitumike hamna haja ya kibakuli nje kila wakati. Halafu tatizo lenu mnapenda sana kulaumu, kila wakati mnalaumu kila mtu na kila kitu badala ya kutenda. Mumetulaumu Wakenya, mara mnalaumu uongozi wenu, mara Kagame mara sasa naona mnalaumu SADC.
Siku moja nikiwa Bongo nilihudhuria mkutano wa CHADEMA (napenda kufuatilia siasa za EAC yote), kwenye huo mkutano jamaa walitaja sana CCM, hadi ikawa nashangaa kama mkutano wa CCM ama CHADEMA. Yaani wanalaumu tu, hawaelezei wananchi wao ni lipi watafanya wakipata uongozi, ila ni lawama tu.

kadoda11 Geza Ulole Bulldog Kimweri NairobiWalker hbuyosh Askari Kanzu Baba Kiki waltham bagamoyo Habari ya Mujini Ngongo ralphtz Hute
 
Last edited by a moderator:

wewe punguani uuzwaji wa NBC unaweza fananisha na Goldenberg scandal au Anglo leasing nyie Wakenya wapumbavu sana ujuaji mwingi hamna chochote unafiki unawasumbua! Kuna taasisi kubwa zaidi ya MNF hapa East Africa? Tukianza na bitega uchumi?
 
By Lawmaina78,
Siku moja nikiwa Bongo nilihudhuria mkutano wa CHADEMA (napenda kufuatilia siasa za EAC yote), kwenye huo mkutano jamaa walitaja sana CCM, hadi ikawa nashangaa kama mkutano wa CCM ama CHADEMA. Yaani wanalaumu tu, hawaelezei wananchi wao ni lipi watafanya wakipata uongozi, ila ni lawama tu.

Kuhusu suala la vyama CCM, CHADEMA, CUF au NCCR-MAGEUZI kutajwa sana ni kwamba siasa za Tanzania ni kupitia vyama ya kisiasa vya kweli na siyo kama Kenya ambapo hakuna vyama halisi vya siasa bali ni magenge ya watu wenye uroho wa madaraka kuanzisha vyama-feki kwa ajili tu ya uchaguzi na ndiyo maana muda wote ni majina RAILA, KENYATTA yanatajwa na wala vyama vyao feki havina muundo wa kiuongozi unaofahamika mfano mwenyekiti au katibu wa vyama n.k hakuna.

Kukosekana kwa vyama vya kisiasa - tajwa nchini Kenya kumepelekea watu maarufu kuwa miungu-watu katika vyama-feki vya siasa na kukaribisha vikundi vya kikabila kuchukua nafasi ya kisiasa Kenya.
 
Muache kulia lia .Alitaka kupewa mabilioni? South Afrika bado ni nchi inayoendelea sio Tajiri hivyo ashukuru kwa kidogo alichopata sababu South Afrika bado ina majukumu mengi kwa raia wake.

Muache kulia lia,Tanzania ina rasilimali nyingi sana.Ni ukosefu wa akili kulia lia umu eti tulipewa msaada kidogo na South Afrika.Acheni hizo mambo.

Kila siku misaada tunapata tena mikubwa ya mabilioni mbona atupigi hatua kubwa.Jambo kubwa ni kudhibiti matumizi mabovu ya pesa na rushwa.Siyo kulia lia na misaada tena kwa nchi kama South Afrika.

Mnatia aibu
 
Sijawai kusikia Tanzania inarely on any country, be it SA or Kenya. Uwepo wetu kwa SADC haumaanishi kwamba SA ndio our lord and master. By that logic then the EAC is likewise reduced to nothing more than a Kenyan area of influence, and i'd rather die than see Tz succumb to a fellow dwarf! Shida yenu tukijaribu kutetea maslahi yetu mnatusema vibaya. January Makamba, ambaye ni mgombea urais 2015 alishatangaza kwamba TZ should join the EAC as the leader that it rightly is and not less. National interests will always be protected above all else. lawmaina78
 
Last edited by a moderator:
Tatizo taasisi ya mwalimu nyerere kama imekaa kifamilia,only butiku,labda ingejumuisha wanazuoni na marais wastaafu na timu kubwa ya wataalamu kwa ajili ya analysis za uchumi siasa na jamii,
 
Kuhusu suala la vyama CCM, CHADEMA, CUF au NCCR-MAGEUZI kutajwa sana ni kwamba siasa za Tanzania ni kupitia vyama ya kisiasa vya kweli na siyo kama Kenya ambapo hakuna vyama halisi vya siasa bali ni magenge ya watu wenye uroho wa madaraka kuanzisha vyama-feki kwa ajili tu ya uchaguzi na ndiyo maana muda wote ni majina RAILA, KENYATTA yanatajwa na wala vyama vyao feki havina muundo wa kiuongozi unaofahamika mfano mwenyekiti au katibu wa vyama n.k hakuna.

Kukosekana kwa vyama vya kisiasa - tajwa nchini Kenya kumepelekea watu maarufu kuwa miungu-watu katika vyama-feki vya siasa na kukaribisha vikundi vya kikabila kuchukua nafasi ya kisiasa Kenya.

Naona uko mbioni kuharibu na kubadilisha mada ili iwe ligi kati ya Kenya na Tanzania kuhusu demokrasia. Ila hata hivyo Watanzania demokrasia hamuezi kutufundisha chochote aidha itakua jina democracy lina maana nyingine. Kwani nyie tangu uhuru mna chama kimoja uongozini, na kila siku mnalalamika sana kukihusu, huwa sipati picha inakuaje kama hamkipendi lakini mpo bado mnakichagua siku zote.

Sisi Kenya tumebadilisha uongozi kupitia vyama nne sasa tangu uhuru. Hiyo ndio inaitwa demokrasia, kuwa na uwezo wa kuchagua baina ya uongozi. Sasa hivi tumefaulu kuwa na katiba mpya na bora Afrika. Si kwamba hatuna changamoto mbali mbali lakini huwa hatuchoki na hatutoki, tunabanana hadi kinaeleweka.
 
Sijawai kusikia Tanzania inarely on any country, be it SA or Kenya. Uwepo wetu kwa SADC haumaanishi kwamba SA ndio our lord and master. By that logic then the EAC is likewise reduced to nothing more than a Kenyan area of influence, and i'd rather die than see Tz succumb to a fellow dwarf! Shida yenu tukijaribu kutetea maslahi yetu mnatusema vibaya. January Makamba, ambaye ni mgombea urais 2015 alishatangaza kwamba TZ should join the EAC as the leader that it rightly is and not less. National interests will always be protected above all else. lawmaina78

Tanzania should earn its leadership position and not cry around. It deserves to be EAC leader, has everything that it takes, but wants to be dragged around. In African cultures, siblings are forbidden to marry and build homes before their first born has made a move. But if the older sibling slows down, the society allows the other members to move on. Tanzania has taken into complaining instead of actions. You chose to run to SADC after claiming Kenya was overshadowing you in EAC, now here you're complaining against South Africa.

Unless you people take a standstill and evaluate yourselves before making a new step, you'll run forever. In Kenya, we have hd our calculations in order, we know what we want and are forging forth strategically and majestically. We are having deals with every SADC member as well as entrenching ourselves in EAC and while not forgeting separate arrangements with ECOWAS and Ethiopia. Brother, this is a game and what matters is how you prepare your players.
 
Sijaona cha kulalamika.

Kwa nn tz tunapenda tufanyiwe vitu 'just because'....
The world runs in business mode.

Choose wisely
 
Back
Top Bottom