Mandela, Mkapa walivyomwangusha Nyerere

TOWASHI

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
294
181
[/FONT]
375_nyerere.jpg

  • Walimwangusha alipohitaji msaada
  • Alitabiri kifo cha taasisi yake
  • Siku zake za mwisho zilikuwa za huzuni

BABA wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alimaliza siku zake za mwisho katika hali ya masikitiko kutokana na vitendo vya mwisho vya watu aliowaamini, Raia Mwema limeambiwa.
Wakati Watanzania wakiadhimisha miaka 15 tangu kufariki kwa Mwalimu katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London, Uingereza mwaka 1999, taarifa mpya zimeibuka kuhusu namna alivyotumia siku zake za mwisho.
Katika mahojiano ambayo gazeti hili pamoja na gazeti lake dada la Raia Tanzania ambayo yamefanywa na watu waliokuwa karibu naye ikiwamo familia yake na watu aliokuwa akifanya nao kazi, mambo makubwa mawili yameelezwa kumuumiza Mwalimu.
Mambo hayo ni mchango mdogo wa serikali za Tanzania na Afrika Kusini kwa taasisi yake ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF) na ubinafsishaji wa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
Mmoja wa viongozi wa MNF aliyezungumza na Raia Mwema kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema Mwalimu alihuzunika sana wakati alipokwenda nchini Afrika Kusini kutafuta fedha za taasisi hiyo na kuambulia mchango kidogo sana.
“Wakati Nelson Mandela akiwa Rais wa Afrika Kusini, Mwalimu alikwenda kutafuta fedha kule akiwa na matumaini makubwa sana. Unajua Tanzania ilijitolea sana kwa ajili ya Uhuru wa Afrika Kusini.
“Afrika Kusini ina uwezo mkubwa wa kiuchumi. Mwalimu alitaraji makubwa sana kutokana na uhusiano baina ya nchi hizi mbili. Cha ajabu, alipokwenda kule serikali ilimpa kiasi cha dola 60,000 (takribani shilingi milioni 60 wakati huo).
“Hebu fikiria uwezo wa kiuchumi wa Afrika Kusini na mchango ambao Mwalimu na Tanzania kwa ujumla walikuwa nao kwa Taifa hilo na halafu Mwalimu anapewa dola 60,000. Nyerere returned a broken man (Nyerere alirudi akiwa amefadhaika sana),” alisema kiongozi huyo.
Kiongozi huyo alieleza pia kwamba kwa upande wa Serikali ya Tanzania, msaada pekee ambao MNF iliupata ni kiwanja kilichopo jirani na Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kilichotolewa wakati wa Serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi, na hawakuwahi kupokea fedha yoyote kutoka serikalini hadi leo.
“Hebu fikiria, serikali yake mwenyewe ya Tanzania haikumpa hata senti moja kwa ajili ya MNF. Serikali ya Rais Benjamin Mkapa haikuwahi kumpa kitu na nafahamu serikali ya Jakaya Kikwete pia haijawahi kuchangia MNF. Hilo ndiyo tatizo,” alisema kiongozi huyo.
Kutokana na hali hiyo, kiongozi huyo alimnukuu Mwalimu Nyerere akisema mwaka mmoja kabla ya kifo chake; “Siku nikifariki dunia, kesho yake tu MNF itakufa”.
Raia Mwema limeelezwa pia namna wasaidizi wa karibu wa Mwalimu walivyoshangazwa na ukweli kuwa katika kitabu cha Mandela cha The Long Walk to Freedom, Mwalimu alitajwa mara moja tu kwenye kitabu hicho.
Gazeti hili linafahamu kwamba, katika kitabu hicho, Mandela alimtaja Mwalimu wakati akieleza kuhusu harakati zake za kutafuta kuungwa mkono na nchi za Afrika katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, ambapo alitembelea Tanganyika huru kutafuta kuungwa mkono.
Wakati wa utawala wa Makaburu wa Afrika Kusini, ilikuwa marufuku kutaja hadharani jina la Nyerere au Tanzania kwa vile ilionekana kama ni uchochezi. Lakini pia Makaburu walitaka kuzuia ushawishi wa Nyerere kwa watu Weusi wa kule. Ndiyo maana Mwalimu alitaraji makubwa sana kutoka huko.
“Ni sawasawa na utawala wa Mkapa. Watanzania wote wanafahamu kuwa isingekuwa Mwalimu, Mkapa huenda asingeupata urais wa Tanzania. Alitaraji huyo ndiye angeisaidia MNF kuliko pengine rais yeyote. Cha ajabu, serikali ya Mkapa haikuchangia kitu. Afadhali hata Mzee Mwinyi ambaye alichangia kiwanja,” kilisema chanzo hicho cha gazeti hili.
Katika mahojiano mengine ambayo gazeti dada la hili, Raia Tanzania, lilifanya na aliyekuwa Katibu Myeka wa Mwalimu, Samwel Kassori, ilibainika pia namna Mwalimu alivyohuzunishwa na suala la kuuzwa kwa NBC kwa mojawapo ya makampuni kutoka nchini Afrika Kusini.
“Lakini moja kubwa ninalokumbuka ni kuhusu mchakato wa uuzwaji wa benki ya NBC mwaka 1997 mwezi Aprili wakati wa utawala Mkapa ambapo Mwalimu aliwahi kulengwalengwa na machozi akipinga benki hiyo kuuzwa kwa ABSA Group kutoka Afrika ya Kusini.
“Wakati huo nakumbuka serikali ilipanga kumwandalia Mwalimu sherehe ya kitaifa ya siku yake ya kuzaliwa (birthday) ya kutimiza miaka 75 ambazo zingefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee wa Jijini Dar es Salaam, na jambo hilo lilimshtua kidogo akaniagiza nichunguze fedha hizo zingetoka wapi na kwanini afanyiwe sherehe kubwa kiasi hicho na pia tetesi zilikuwa zimezagaa kuwa NBC inauzwa.
“Wakati huo Waziri wa Fedha alikuwa Daniel Yona, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alikuwa Peter Ngumbulu na Gavana wa Benki Kuu (BoT) alikuwa Dk. Idris Rashid.
“Baada ya kupata taarifa za kwamba benki hiyo iko mbioni kupigwa bei, Mwalimu aliomba maelezo kutoka kwa wahusika ambao ni Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu na Gavana wa BoT.
“Majibu ya serikali yalikuwa kwamba NBC inauzwa kwa sababu taasisi za fedha za Kimataifa za Fedha (IMF) na Benki ya Dunia (WB) ziliagiza Benki hiyo kuuzwa.
“Baada ya kupata maelezo hayo Mwalimu alikasirika kweli kweli, akaniita na tukiwa nyumbani kwake Msasani aliniagiza kumpigia simu Rais wa (WB) wakati ili azungume naye.
“Baada ya kumpata Rais huyo wa (WB) ambaye bado alikuwa akimwita Mwalimu Mr. President (Mheshimiwa Rais), alikana IFM pamoja na Benki ya Dunia kushinikiza au kutoa masharti kuuzwa kwa NBC.
“Namnukuu Rais huyo wa WB aliniambia:”Mr Kasori do me a favour could you request President Nyerere to come to our headquarters in Washington and read the documents from Tanzania government, they are too voluminous but will try to make executive summary of the same”
“Maana yake ni kwamba walitaka Mwalimu akajioonee mwenyewe nyaraka zilizotumwa katika taasisi hizo za kimataifa kuhusu uuzaji wa NBC na walisema wangelipa gharama zote muhimu za safari hiyo.
“Baada ya mazungumzo ya simu siku mbili baadaye tulifunga safari na Mwalimu hadi Washington nchini Marekani ambapo tulikutana na Rais wa WB kwa kikao cha siku nzima na kupitia nyaraka muhimu zilizowasilishwa kwao na serikali ya Tanzania.
“Tulirudi nyumbani baada ya wiki moja na Mwalimu aliniagiza kwanza niwatafute Yona, Ngumbulu na Dk. Rashid ili azungumze nao kabla ya kukutana na Rais Mkapa.
“Basi baada ya mimi kufanya mawasiliano nao wote hakuna aliyeitikia wito wa Mwalimu “walimpuuza” na badala yake walimtuma Donald Kamori ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC.
“Nakumbuka vizuri kikao na Kamori kilifanyika Msasani nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, Aprili 13 mwaka huo 1997, na Kamori alikuwa mtaalamu aliyebobea katika masuala ya fedha na ndiye kati ya wataalamu wazawa walioanzisha BoT.
“Kamori akiwa na nyaraka na takwimu za kitaalamu. Alimweleza Mwalimu bila ya kuficha kuwa kuiuza NBC serikali ilikuwa inafanya makosa makubwa katika sekta ya fedha kwa kuwa Benki hiyo ilikuwa inaendeshwa kwa faida kubwa. Uuzwaji wake ungeleta athari ya moja kwa serikali pamoja na taasisi zake nyeti.
“Mwalimu alitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa, akasema ‘ooooh kweli nimesomesha Watanzania’ alikuwa amevutiwa sana na maelezo ya kitaalamu ya Donald Kamori.
“Baada ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa Kamori, Mwalimu aliomba kukutana na Rais Mkapa na kikao kilifanyika Ikulu ambapo alitetea NBC isiuzwe kwani ndiyo ilikuwa nguzo ya serikali hasa wakati inapoishiwa fedha katika mambo “nyeti yanayohusiana na usalama wa nchi” ilikuwa inakopa fedha NBC.
“Majadiliano na Mkapa yalichukua muda mrefu sana kuhusu suala hilo na itoshe kusema kwamba baada ya majadiliano hayo marefu likazaliwa wazo la kugawanywa kwa hiyo na kuanzishwa kwa Benki ya NMB ambayo serikali ina hisa hadi leo.
“Kilichomsikitisha zaidi Mwalimu ni kwamba baada ya juhudi zote hizo Kamori alifukuzwa kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa NBC na kurudishwa BoT bila kupangiwa kazi yoyote.Hakuwa na ofisi pale akifika anasoma magazeti aliyojinunulia na kurudi zake nyumbani.
“Alitishwa sana na kuhojiwa ni kwanini alikwenda kumweleza Mwalimu na kumwonyesha nyaraka za uuzwaji wa NBC kwa Benki ya ABSA ya Afrika ya Kusini?
“Kamori alinipigia simu akanieleza masahibu yaliyomkuta na mimi nikaufikisha ujumbe wake kwa Mwalimu, baada ujumbe huo Mwalimu alisikitika sana, akahoji ni kwanini wanafanya mambo hayo “kumfedhehesha” akiwa hai?
“Huyo Kamori alikuwa mzalendo kweli kweli ni kati ya Watanzania walioipenda nchi yao. Siku hiyo hiyo aliacha kazi akasema hawezi kupokea mshahara asioufanyia kazi na akaenda kufanya kazi zake sijui kwa sasa atakuwa wapi.
“Sakata la kuuzwa kwa NBC kwa kweli ni kati ya mambo yaliyowahi kumchanganya akili Mwalimu na kwa upande wangu uuzwaji wa benki ile ulifungua milango ya ufisadi mwingine uliokuja kufanyika miaka ya baadaye,” alisema.

Chanzo: Raiamwema
 
RAIA MWEMA NA ILE RAI YA ZAMANI.....MKAPA NA LOWASSA WAMEWAKOSEA NINI.? Nimelisoma gazeti hili jana na huko nyuma...Angle yao against hawa wawili kwakweli inaondoa credibility ya Newsprint hii. Is too much....
 
FDR.Jr
It is not Mkapa kalikosea nini Raia Mwema. Yanayosemwa hayana ukweli? Hilo ndilo swali tunalopaswa kujiuliza. Mimi nilimfahamu Kamori kwa muda mrefu. Tunasali kanisa moja. Sikujua kwa nini ghafla Mkapa alimwondoa NBC. Leo Raia Mwema imetupa jibu. Kuna tetesi niliwahi kusikia kuwa Mkapa alikuwa ameshapokea hongo ya Makaburu wakati Mwalimu anajaribu kunusuru benki hiyo isiuzwe. Ilikuwa ngumu kwake kurudisha hizo hela.
 
umeamua kuhabarisha ama umeamua kujipa kazi ya matangazo ya magazeti?kama mpaka habari husika imeandikwa na magazeti wewe unaogopa nini bado kutiririka mkuu,ondoa hofu weka hapa kama nyingine zote zinazowekwa hapa ili watu wasome
 
Mandela, Mkapa walivyomwangusha Nyerere

Mwandishi Wetu

Toleo la 375
15 Oct 2014

375_nyerere.jpg

  • Walimwangusha alipohitaji msaada
  • Alitabiri kifo cha taasisi yake
  • Siku zake za mwisho zilikuwa za huzuni

BABA wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alimaliza siku zake za mwisho katika hali ya masikitiko kutokana na vitendo vya mwisho vya watu aliowaamini, Raia Mwema limeambiwa.
Wakati Watanzania wakiadhimisha miaka 15 tangu kufariki kwa Mwalimu katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London, Uingereza mwaka 1999, taarifa mpya zimeibuka kuhusu namna alivyotumia siku zake za mwisho.
Katika mahojiano ambayo gazeti hili pamoja na gazeti lake dada la Raia Tanzania ambayo yamefanywa na watu waliokuwa karibu naye ikiwamo familia yake na watu aliokuwa akifanya nao kazi, mambo makubwa mawili yameelezwa kumuumiza Mwalimu.
Mambo hayo ni mchango mdogo wa serikali za Tanzania na Afrika Kusini kwa taasisi yake ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF) na ubinafsishaji wa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC).
Mmoja wa viongozi wa MNF aliyezungumza na Raia Mwema kwa masharti ya kutotajwa jina, alisema Mwalimu alihuzunika sana wakati alipokwenda nchini Afrika Kusini kutafuta fedha za taasisi hiyo na kuambulia mchango kidogo sana.
"Wakati Nelson Mandela akiwa Rais wa Afrika Kusini, Mwalimu alikwenda kutafuta fedha kule akiwa na matumaini makubwa sana. Unajua Tanzania ilijitolea sana kwa ajili ya Uhuru wa Afrika Kusini.
"Afrika Kusini ina uwezo mkubwa wa kiuchumi. Mwalimu alitaraji makubwa sana kutokana na uhusiano baina ya nchi hizi mbili. Cha ajabu, alipokwenda kule serikali ilimpa kiasi cha dola 60,000 (takribani shilingi milioni 60 wakati huo).
"Hebu fikiria uwezo wa kiuchumi wa Afrika Kusini na mchango ambao Mwalimu na Tanzania kwa ujumla walikuwa nao kwa Taifa hilo na halafu Mwalimu anapewa dola 60,000. Nyerere returned a broken man (Nyerere alirudi akiwa amefadhaika sana)," alisema kiongozi huyo.
Kiongozi huyo alieleza pia kwamba kwa upande wa Serikali ya Tanzania, msaada pekee ambao MNF iliupata ni kiwanja kilichopo jirani na Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kilichotolewa wakati wa Serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi, na hawakuwahi kupokea fedha yoyote kutoka serikalini hadi leo.
"Hebu fikiria, serikali yake mwenyewe ya Tanzania haikumpa hata senti moja kwa ajili ya MNF. Serikali ya Rais Benjamin Mkapa haikuwahi kumpa kitu na nafahamu serikali ya Jakaya Kikwete pia haijawahi kuchangia MNF. Hilo ndiyo tatizo," alisema kiongozi huyo.
Kutokana na hali hiyo, kiongozi huyo alimnukuu Mwalimu Nyerere akisema mwaka mmoja kabla ya kifo chake; "Siku nikifariki dunia, kesho yake tu MNF itakufa".
Raia Mwema limeelezwa pia namna wasaidizi wa karibu wa Mwalimu walivyoshangazwa na ukweli kuwa katika kitabu cha Mandela cha The Long Walk to Freedom, Mwalimu alitajwa mara moja tu kwenye kitabu hicho.
Gazeti hili linafahamu kwamba, katika kitabu hicho, Mandela alimtaja Mwalimu wakati akieleza kuhusu harakati zake za kutafuta kuungwa mkono na nchi za Afrika katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, ambapo alitembelea Tanganyika huru kutafuta kuungwa mkono.
Wakati wa utawala wa Makaburu wa Afrika Kusini, ilikuwa marufuku kutaja hadharani jina la Nyerere au Tanzania kwa vile ilionekana kama ni uchochezi. Lakini pia Makaburu walitaka kuzuia ushawishi wa Nyerere kwa watu Weusi wa kule. Ndiyo maana Mwalimu alitaraji makubwa sana kutoka huko.
"Ni sawasawa na utawala wa Mkapa. Watanzania wote wanafahamu kuwa isingekuwa Mwalimu, Mkapa huenda asingeupata urais wa Tanzania. Alitaraji huyo ndiye angeisaidia MNF kuliko pengine rais yeyote. Cha ajabu, serikali ya Mkapa haikuchangia kitu. Afadhali hata Mzee Mwinyi ambaye alichangia kiwanja," kilisema chanzo hicho cha gazeti hili.
Katika mahojiano mengine ambayo gazeti dada la hili, Raia Tanzania, lilifanya na aliyekuwa Katibu Myeka wa Mwalimu, Samwel Kassori, ilibainika pia namna Mwalimu alivyohuzunishwa na suala la kuuzwa kwa NBC kwa mojawapo ya makampuni kutoka nchini Afrika Kusini.
"Lakini moja kubwa ninalokumbuka ni kuhusu mchakato wa uuzwaji wa benki ya NBC mwaka 1997 mwezi Aprili wakati wa utawala Mkapa ambapo Mwalimu aliwahi kulengwalengwa na machozi akipinga benki hiyo kuuzwa kwa ABSA Group kutoka Afrika ya Kusini.
"Wakati huo nakumbuka serikali ilipanga kumwandalia Mwalimu sherehe ya kitaifa ya siku yake ya kuzaliwa (birthday) ya kutimiza miaka 75 ambazo zingefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee wa Jijini Dar es Salaam, na jambo hilo lilimshtua kidogo akaniagiza nichunguze fedha hizo zingetoka wapi na kwanini afanyiwe sherehe kubwa kiasi hicho na pia tetesi zilikuwa zimezagaa kuwa NBC inauzwa.
"Wakati huo Waziri wa Fedha alikuwa Daniel Yona, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alikuwa Peter Ngumbulu na Gavana wa Benki Kuu (BoT) alikuwa Dk. Idris Rashid.
"Baada ya kupata taarifa za kwamba benki hiyo iko mbioni kupigwa bei, Mwalimu aliomba maelezo kutoka kwa wahusika ambao ni Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu na Gavana wa BoT.
"Majibu ya serikali yalikuwa kwamba NBC inauzwa kwa sababu taasisi za fedha za Kimataifa za Fedha (IMF) na Benki ya Dunia (WB) ziliagiza Benki hiyo kuuzwa.
"Baada ya kupata maelezo hayo Mwalimu alikasirika kweli kweli, akaniita na tukiwa nyumbani kwake Msasani aliniagiza kumpigia simu Rais wa (WB) wakati ili azungume naye.
"Baada ya kumpata Rais huyo wa (WB) ambaye bado alikuwa akimwita Mwalimu Mr. President (Mheshimiwa Rais), alikana IFM pamoja na Benki ya Dunia kushinikiza au kutoa masharti kuuzwa kwa NBC.
"Namnukuu Rais huyo wa WB aliniambia:"Mr Kasori do me a favour could you request President Nyerere to come to our headquarters in Washington and read the documents from Tanzania government, they are too voluminous but will try to make executive summary of the same"
"Maana yake ni kwamba walitaka Mwalimu akajioonee mwenyewe nyaraka zilizotumwa katika taasisi hizo za kimataifa kuhusu uuzaji wa NBC na walisema wangelipa gharama zote muhimu za safari hiyo.
"Baada ya mazungumzo ya simu siku mbili baadaye tulifunga safari na Mwalimu hadi Washington nchini Marekani ambapo tulikutana na Rais wa WB kwa kikao cha siku nzima na kupitia nyaraka muhimu zilizowasilishwa kwao na serikali ya Tanzania.
"Tulirudi nyumbani baada ya wiki moja na Mwalimu aliniagiza kwanza niwatafute Yona, Ngumbulu na Dk. Rashid ili azungumze nao kabla ya kukutana na Rais Mkapa.
"Basi baada ya mimi kufanya mawasiliano nao wote hakuna aliyeitikia wito wa Mwalimu "walimpuuza" na badala yake walimtuma Donald Kamori ambaye alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC.
"Nakumbuka vizuri kikao na Kamori kilifanyika Msasani nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, Aprili 13 mwaka huo 1997, na Kamori alikuwa mtaalamu aliyebobea katika masuala ya fedha na ndiye kati ya wataalamu wazawa walioanzisha BoT.
"Kamori akiwa na nyaraka na takwimu za kitaalamu. Alimweleza Mwalimu bila ya kuficha kuwa kuiuza NBC serikali ilikuwa inafanya makosa makubwa katika sekta ya fedha kwa kuwa Benki hiyo ilikuwa inaendeshwa kwa faida kubwa. Uuzwaji wake ungeleta athari ya moja kwa serikali pamoja na taasisi zake nyeti.
"Mwalimu alitikisa kichwa kwa masikitiko makubwa, akasema ‘ooooh kweli nimesomesha Watanzania' alikuwa amevutiwa sana na maelezo ya kitaalamu ya Donald Kamori.
"Baada ya kupata maelezo ya kutosha kutoka kwa Kamori, Mwalimu aliomba kukutana na Rais Mkapa na kikao kilifanyika Ikulu ambapo alitetea NBC isiuzwe kwani ndiyo ilikuwa nguzo ya serikali hasa wakati inapoishiwa fedha katika mambo "nyeti yanayohusiana na usalama wa nchi" ilikuwa inakopa fedha NBC.
"Majadiliano na Mkapa yalichukua muda mrefu sana kuhusu suala hilo na itoshe kusema kwamba baada ya majadiliano hayo marefu likazaliwa wazo la kugawanywa kwa hiyo na kuanzishwa kwa Benki ya NMB ambayo serikali ina hisa hadi leo.
"Kilichomsikitisha zaidi Mwalimu ni kwamba baada ya juhudi zote hizo Kamori alifukuzwa kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa NBC na kurudishwa BoT bila kupangiwa kazi yoyote.Hakuwa na ofisi pale akifika anasoma magazeti aliyojinunulia na kurudi zake nyumbani.
"Alitishwa sana na kuhojiwa ni kwanini alikwenda kumweleza Mwalimu na kumwonyesha nyaraka za uuzwaji wa NBC kwa Benki ya ABSA ya Afrika ya Kusini?
"Kamori alinipigia simu akanieleza masahibu yaliyomkuta na mimi nikaufikisha ujumbe wake kwa Mwalimu, baada ujumbe huo Mwalimu alisikitika sana, akahoji ni kwanini wanafanya mambo hayo "kumfedhehesha" akiwa hai?
"Huyo Kamori alikuwa mzalendo kweli kweli ni kati ya Watanzania walioipenda nchi yao. Siku hiyo hiyo aliacha kazi akasema hawezi kupokea mshahara asioufanyia kazi na akaenda kufanya kazi zake sijui kwa sasa atakuwa wapi.
"Sakata la kuuzwa kwa NBC kwa kweli ni kati ya mambo yaliyowahi kumchanganya akili Mwalimu na kwa upande wangu uuzwaji wa benki ile ulifungua milango ya ufisadi mwingine uliokuja kufanyika miaka ya baadaye," alisema.

Soma zaidi kuhusu:

- See more at: Raia Mwema - Mandela, Mkapa walivyomwangusha Nyerere
 
Jasusi, hebu tuheshimu viongozi wetu jamani....huyu Mkapa ni mlafi kiasi hicho cha kupokea hongo ya ABSA,! Marehemu kaka yangu ni victim wa NBC kugawanywa...inaniumiza sana hii kitu lakini mimi simlaumu Ben au Mwinyi ktk ubinafsishaji...maana 4yrs yangu STAMICO yamenifanya niwe nilivyo...Waswahili wenzetu wameporomoa State firms....Niliajiriwa kwa Basic 18,500/= retrenchment letter ikaja Basic ya 16,500/=! Tulidhulumiwa just bcoz STAMICO HQ haikuwa na mapenzi na GM wetu....tulilalamika kwa maandishi aash wapi, waliotufanyia hivi ni PSRC na Stamico....hiki kimetokea 2000 Kisarawe Pugu Kaolin Mine... Waswahili wanajisifia oooh org iko ktk good shape kumbe wao ndio walaji na mambo hayaendi accordingly. ...Kamori n team wanajua NBC ilikuwaje lakini kamwe hawatasema the deadly position waliyokuwa nayo...

Kama NBC ilikuwa such strong Bank MKOMBOZI kwa nchi mbona NMB na CRDB wamewapiku
 
FDR.Jr,
Mimi sijui NBC ilikuwa strong kwa kiasi gani, ninachojua ni kwamba ni benki pekee iliyokuwa na matawi kila sehemu za Tanzania. Labda NMB na CRDB wameipiku sasa kwa sababu inajulikana si benki yetu tena. Iliuzwa kwa benki ya Afrika kusini kwa hela za kutupwa na benki hiyo wakageuka na kuiuzia Barclays kwa mabilioni ya dola. Siwezi kumheshimu Mkapa kwa madudu aliyoyafanya hasa katika ugawaji wa mashirika ya umma ambayo yalijengwa kwa hela ya walipa kodi na yeye kuwagawia wawekezaji kwa hela za kutupwa. Hata hivyo, pole sana kwa yaliyokusibu.
 
Mwalimu alikuwa mtu muhim sana endapo wangemuacha akapumuwa kwa miaka mitano tu !
Nimekubali kweli ukila nyama ya mtu huwezi kuacha chakilicho mkuta mwalim ndicho kilicho kinacho wakuta watu wengi muhim sana kwa taifahili akiwemo dr mvungi mungu awalaze mahala pema kunasiku yatajulikana mengi laana za kuku zina anza taratibu kumtafuna mwewe!!
 
Mw. Nyerere ndio alimpigia chapuo huyu mtu awe Rais, kwa hiyo unaweza kusema Nyerere ndio aliwaangusha Watanzania.

Lakini nataka kumsamehe kwa hili kwa sababu mwaka ule wa 1995 hakukuwa na credible figures to lead the nation out of the morass of Mwinyi years, ambae nae ni yeye alimleta . Alimpaisha Mkapa ili kuwazima kina Lowassa na Kikwete. Ambao kweli wamekuja kutuliza Mwalimu alipokufa. Alikuwepo labda Mwandosya, too aloof and unproven pamoja na Salim Salim, Mzanzibari, hazikuwa zam zao. Upande wa pili ulikuwa na kina Mrema, Mtikila, Mapesa, wote ma douche bags wa kisiasa ambao aliwaomba wakagombee ubunge, si urais.
 
RAIA MWEMA NA ILE RAI YA ZAMANI.....MKAPA NA LOWASSA WAMEWAKOSEA NINI.? Nimelisoma gazeti hili jana na huko nyuma...Angle yao against hawa wawili kwakweli inaondoa credibility ya Newsprint hii. Is too much....

Mbona unataka kutetea udhalimu? Mkapa alifanya mabaya yake na ndo hayo na yale ya kuleta wezi wa kutuibia madini, aliibinafsisha Tanesco kwa wale washenzi wa South Afrika aka netgroup, akawaleta wakaguzi wa madini kutoka ulaya. Yaani kwake watanzania wahakuweza.
JK nampongeza kwa kujitahidi kufukia mashomo ya mtangulizi wake ingawa nae baadhi yamemzamisha na kuibua mengine. Hivyo Rais ajaye naye atakutana na mashimo.
 
Mw. Nyerere ndio alimpigia chapuo huyu mtu awe Rais, kwa hiyo unaweza kusema Nyerere ndio aliwaangusha Watanzania.

Lakini nataka kumsamehe kwa hili kwa sababu mwaka ule wa 1995 hakukuwa na credible figures to lead the nationn out of the morass of Mwinyi years, ambae nae ni yeye alimleta . Alimpaisha Mkapa ili kuwazima kina Lowassa na Kikwete. Ambao kweli wamekuja kutuliza Mwalimu alipokufa. Alikuwepo labda Mwandosya, too aloof and unproven pamoja na Salim Salim, Mzanzibari, hazikuwa zam zao. Upande wa pili ulikuwa na kina Mrema, Mtikila, Mapesa, wote ma douche bags wa kisiasa ambao aliwaomba wakagombee ubunge, si urais.

Kijana Nyerere hakupenda Mwinyo awe Rais yeye alimtaka Salim Ahmed Salimu kilichomwangusha Salimu ni umri kwani wao CCM katiba uao ilitaka rais awe na miaka 45 na kuendelea. Thabiti Kombo ndiye aliyemlazimisha Mwinyi jina lake likitajwa asikatae uteuzi.
 
FDR.Jr
It is not Mkapa kalikosea nini Raia Mwema. Yanayosemwa hayana ukweli? Hilo ndilo swali tunalopaswa kujiuliza. Mimi nilimfahamu Kamori kwa muda mrefu. Tunasali kanisa moja. Sikujua kwa nini ghafla Mkapa alimwondoa NBC. Leo Raia Mwema imetupa jibu. Kuna tetesi niliwahi kusikia kuwa Mkapa alikuwa ameshapokea hongo ya Makaburu wakati Mwalimu anajaribu kunusuru benki hiyo isiuzwe. Ilikuwa ngumu kwake kurudisha hizo hela.

Hii habari nillisoma jana nikawa baridi kabisa kwa huzuni licha kwamba nilikua na taarifa hizi miaka sasa! Nashukuru Mungu ujambazi wa Benjamin Mkapa unaanza tolewa hadharani bila kificho. Utafuata wa Kikwete na genge lake. Alikua Rais Mbeki alipo ingia madarakani alianza kuenzi mchango wa Mwalimu na Tanzania ktk ukombozi wa SA.

Kwasababu nina akili nzuri niliuliza mwaka jana watawala wetu walipo jipeleka Congo DRC kwamba wameenda kuokoa maisha ama kufanya biashara ambayo haitakuwa na faida yoyote kwa nchi bali kwenda ktk mifuko ya watawala?! Siku hizi tunaona Wakongo wamejazana Dar kama vile ni Watanganyika wenzetu na hakuna mtawala mwenye majibu!!!
 
Hili gazeti limenipa mawazo mengi sana kwa kweli. Nikajaribu kuunganisha na threads za humu ndani JF ya kuwa Mwalimu alipumzishwa mapema kabla ya wakati wake ili mambo mengine kama haya na aliyosema Jasusi yafanikiwe.....Anyway...naamini hakuna siri ya watu waili...itafahamika tu
 
Oh yeah. Mwalimu aliuawa na Majambazi wa CCM. Siku watz wakiamka na kujua nchi yao imeongozwa na wahuni wezi na washenzi ndio kutawaka moto.
Cha ajabu hawa watu hawasomi history sijui. For years mianguko ya serikali,falme kubwa zimeshawahi kutokea sembuse CCM?
Its a matter of time. Mtu mbaya kuliko wote ni mkapa. Ndie aliyelete ufisadi wa ajabu.
 
..... Ndie aliyelete ufisadi wa ajabu.

the Mr. Clean successors ,capitalized on that...as the NBC was downed by elite financial murders, it was clear that there was no way our country could had survived on the ...the drying which hit our water reservoirs intended for running power plant. Despite the warning which was put forward to rulers on the danger of drought, the ruler proceeded to channel water to the plantations, Nyumba ya Mungu Power plant is a good example. The 2008 power crisis was inevitable, the formation of Richmond was also inevitable....you can continue to join dots. NBC was no longer there to support our financial capability...
 
Back
Top Bottom