Manchester UNITED hoi kwa Liverpool | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manchester UNITED hoi kwa Liverpool

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, Sep 14, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Manchester hoi kwa Liverpool

  LONDON, Uingereza
  KOCHA wa Liverpool, Rafael Benitez amepata ushindi wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu dhidi ya Manchester United, kwa bao la dakika za mwisho la Ryan Babel aliyetokea benchi.

  Mechi hiyo iliyochezwa jana Uwanja wa Anfield na kuhudhuriwa na mashabiki 44,192 ilimalizika kwa wenyeji Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 2-1

  Carlos Tevez aliwashitua Liverpool baada ya dakika tatu tangu filimbi ya kuanzisha pambano hilo ilipolia akimalizia wavuni pasi ya Dimitar Berbatov.

  Makosa yaliyofanywa na kipa wa Manchester United, Edwin van der Sar ya kupangua ovyo dakika ya 26 yaliipatia Liverpool bao baada ya mpira huo kumgonga mguuni beki Wes Brown na kujaa wavuni.

  Bao lililoifanya Liverpool iondoke na pointi zote tatu lilifungwa dakika ya 76 na Babel kwa shuti la mguu wa kulia ndani ya eneo la penelti baada ya kupata pasi ya Dirk Kuyt.

  Vidic alitolewa nje dakika ya 89 baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu Xabi Alonso.

  Huo ni ushindi wa kwanza kwa Benitez dhidi ya Manchester United tangu alipoanza kuifundisha Liverpool mwaka 2004 na ulipatikana bila Steven Gerrard na Fernando Torres ambao hawakuwemo katika kikosi kilichoanza mechi hiyo. line-up.

  Liverpool: Jose Reina, Alvaro Arbeloa, Martin Skrtel, Jamie Carragher, Fabio Aurelio, Yossi Benayoun/Steven Gerrard, Xabi Alonso, Javier Mascherano/Sami Hyypia, Albert Riera/Ryan Babel, Dirk Kuyt na Robbie Keane.

  Manchester: Edwin Van der Sar, Wes Brown, Rio Ferdinand, Nemanja Vidic, Patrick Evra, Wayne Rooney, Paul Scholes/Owen Hargreaves, Michael Carrick/Ryan Giggs, Oliveira Anderson/Luis Nani, Carlos Tevez na Dimitar Berbatov
   
 2. Manda

  Manda JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 2,075
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mama mia there were no need kuanzisha thread nyingine as much as kuna thread nyingine ya Manutd-Red Devils, nafikiri ingekuwa vyema zaidi kuhamishia hii thread kule kwenye kijiwe chetu 'mashetani' ili kuepuka duplication za thread.

  Anyway ni mtizamo tu Mama mia, MOD...if buy my idea them fanya mambo basi.

  Karibu kijiweni Mama mia!!

  One Love....One United!!
   
 3. W

  WAIKORU JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2017
  Joined: Dec 9, 2015
  Messages: 1,002
  Likes Received: 965
  Trophy Points: 280
  Klopp for Kop...viva Liver
   
 4. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2017
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Mmmh wafukua makaburi naona mmemsahau Diego Forlan
   
Loading...