Manati kubwa ya kurusha madawa ya kulevya yagunduliwa mpakani Marekani

Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,248
5,537
Wauza unga wanazidi kujiimarisha kimkakati. Baada ya maafisa wa marekani kudhibiti kwa kiasi fulani biashara ya mihadarati,wamegundua manatai itakayokuwa inasafirisha madawa ya kulevya kutoka mexico mpaka marekani.
Magwiji wa mihadarati East Africa na kati kina Ayubu mfaume *kiboko* na kinje pamoja na Kina Juma Pinto huenda wakaanza kuitumia manati hii kusafirisha MADAWA ya kulevya kutoka Tanzania kuelekea Kenya ni swala la muda tu.
======================================================== Maafisa wa Marekani wanaoshika doria mpakani, wamegundua manati kubwa ambayo ilikuwa imefungamanishwa na ua ulio kwenye mpaka wa taifa hilo na Mexico.

Manati hiyo inaonekana kuundwa mahsusi kwa ajili ya kurusha dawa za kulevya hadi Marekani.

Marekani imekuwa ikikabiliana sana na walanguzi wa mihadarati kutoka Mexico pamoja na wahamiaji.

Rais Donald Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu sana kuzuia hilo.

Manati hiyo kubwa iligunduliwa na maafisa kusini mashariki mwa Tucson, Arizona, wiki iliyopita.

Wanasema waliwaona wanaume kadha wakitawanyika na kutoroka walipogundua kwamba maafisa hao walikuwa wanafika.

Maafisa hao walipokagua eneo hilo, waligundua vifurushi viwili vya bangi, vilivyokuwa na bangi ya jumla ya kilo 21.

Vifurushi hivyo vilikuwa bado havijarushwa.

Manati hiyo ambayo ilikuwa imejengwa upande wa Mexico wa ua ilibomolewa.

Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

Takriban umbali wa maili 650 kati ya maili 1,100 (1,770km) za mpaka wa Mexico na Marekani tayari kumejengwa ua au ukuta.

Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu lakini walanguzi wamekuwa wakitumia ubunifu katika kutumia njia za kufikisha madawa Marekani.
Screenshot_2017-02-17-07-13-42.png

Miongoni mwa njia hizi ni kutumia ndege ndogo zisizo na marubani na wakati mwingine kuchimba njia za chini kwa chini zinazofika hadi Marekani.

Mwezi Machi, maafisa waligundua njia ya chini kwa chini ya umbali wa mita 380 ambayo ilikuwa imetoka kwenye mgahawa mmoja Mexico hadi kwenye jumba moja California.
Source: BBC
 
Baada ya haya mahandaki naona walikuja na manati.

Kweli hii biashara haramu ni hatari na inahitaji vita kubwa na vya kudumu.

One of the longest cross-border drugs-smugglingtunnels between Mexico and the US has been found by authorities in San Diego, American officials say. They say the 800m (874 yards) tunnel was used to transport an "unprecedented cache" of cocaine and marijuana.Apr 21, 2016
Huge US-Mexico drugs tunnel found in San Diego - BBC News
www.bbc.com/news/world-us-canada-36099336
 
Haya majitu ya Mexico nayo yanatia aibu; kila siku drugs na wao, wao na drugs! Funny enough hata serikali yao haionekani kuchukua hatua za maana kukabiliana na huu ujinga; yet it is a Catholic majority country > 80%. Wanakera sana.
 
Hahaaaa hii dunia inachekesha kwa watu wasio jua
Madawa yanauwezo wa kukuingizia pesa nyingi sana
Kuisha haiwezekani hata CIA pia huwa wanafanya hii biashara
Ila kwa uelewa mdogo wa watu wanafikiri CIA wanathibi wale huwa wana pretend.
 
US kuwa jirani na Mexico inaathirika sana. hii njia ya kupitisha dawa chini ya ardhi ndio iliniacha hoi sababu nilisikia jamaa waliweka bomba kabisa ardhini la kusafirishia!
 
_94661151_mediaitem94661150.jpg
Haki miliki ya pichaUSBP
Image captionManati hiyo kubwa ilikuwa imefungamanishwa na ua mpakani

Maafisa wa Marekani wanaoshika doria mpakani, wamegundua manati kubwa ambayo ilikuwa imefungamanishwa na ua ulio kwenye mpaka wa taifa hilo na Mexico.

Manati hiyo inaonekana kuundwa mahsusi kwa ajili ya kurusha dawa za kulevya hadi Marekani.

Marekani imekuwa ikikabiliana sana na walanguzi wa mihadarati kutoka Mexico pamoja na wahamiaji.

Rais Donald Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu sana kuzuia hilo.

Manati hiyo kubwa iligunduliwa na maafisa kusini mashariki mwa Tucson, Arizona, wiki iliyopita.

Wanasema waliwaona wanaume kadha wakitawanyika na kutoroka walipogundua kwamba maafisa hao walikuwa wanafika.

Maafisa hao walipokagua eneo hilo, waligundua vifurushi viwili vya bangi, vilivyokuwa na bangi ya jumla ya kilo 21.

Vifurushi hivyo vilikuwa bado havijarushwa.

Manati hiyo ambayo ilikuwa imejengwa upande wa Mexico wa ua ilibomolewa.

Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

_94661155_mediaitem94661154.jpg
Haki miliki ya pichaUSBP
Image captionManati hiyo ilikuwa imeunganishwa na ua
Takriban umbali wa maili 650 kati ya maili 1,100 (1,770km) za mpaka wa Mexico na Marekani tayari kumejengwa ua au ukuta.

Trump ameahidi kujenga ukuta mrefu lakini walanguzi wamekuwa wakitumia ubunifu katika kutumia njia za kufikisha madawa Marekani.

Miongoni mwa njia hizi ni kutumia ndege ndogo zisizo na marubani na wakati mwingine kuchimba njia za chini kwa chini zinazofika hadi Marekani.

Mwezi Machi, maafisa waligundua njia ya chini kwa chini ya umbali wa mita 380 ambayo ilikuwa imetoka kwenye mgahawa mmoja Mexico hadi kwenye jumba moja California,
 
Back
Top Bottom