Rajab_Omar
JF-Expert Member
- May 15, 2016
- 16,477
- 27,176
Simba inamaliza mwaka ikiwa kileleni mwa msimamo baada ya takribani miaka 4 kuwahi kufanya hivyo huko nyuma
Msemaji wa klabu ya Wekundu wa Msimbazi Haji Sunday Manara amewakashifu watani wao wa jadi klabu ya Yanga kwa kitendo chao cha kutowalipa mishahara na posho wachezaji wake hivyo kuishi kwa kutanga tanga tanga tu
Kupitia akaunti yake ya instagram Haji Manara amewapiga kijembe Wana Jangwani kwa kitendo chao cha kujiita wa kimataifa wakati ili hali wana shindwa kuwalipa wachezaji mishahara na posho zao kwa wakati
Haji Sunday Manara ameandika " Timu inayojiita ya kimataifa wachezaji wake hawajalipwa mishahara mpaka sasa wanaish kwa vifurushi vya siku huku wakilia njaa"
Hali kadhalika msemaji huyo wa Msimbazi Haji Manara amezungumzia bahati waliyo kuwa nayo klabu ya Simba kuwa ndiyo timu pekee duniani kushabikiwa na Raisi wa nchi pamoja na Waziri Mkuu wake katika awamu mmoja ya uongozi Serikalini ".Tanzaniani nchi pekee ambayo ina Rais na Waziri Mkuu wote mashabiki wa Simba"
Kwa muda mrefu Yanga kupitia msemaji wao aliye fungiwa na TFF Jerry Muro, wamekuwa wakiwatania wapinzani wao klabu ya Simba kwa kuwaita wa mchangani huku wao wakiji nasibu ni kimataifa, hasa kutokana na ushiriki wao wa mara kwa mara kwenye michuano ya kimataifa kama klabu bingwa Afrika au Shirikisho.
Tunapomaliza mwaka 2016 1.Simba inaongoza ligi 2.Trump ni mwanaume pekee katika historia ambaye ameshinda ubishi na mwanamke 3.Tanzaniani nchi pekee ambayo ina Rais na Waziri Mkuu wote mashabiki wa Simba. 4.Neno Simba limetajwa zaidi kuliko wanyama wote. 5.Timu inayojiita ya kimataifa wachezaji wake hawajalipwa mishahara mpaka sasa wanaish kwa vifurushi vya siku huku wakilia njaa 2017 Tutaona mengi.