GE2025 Manara afanya kampeni za mtaa kwa mtaa Kariakoo kuelekea Oktoba 29

GE2025 Manara afanya kampeni za mtaa kwa mtaa Kariakoo kuelekea Oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kariakoo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Haji Manara leo Oktoba 28, 2025, amefanya kampeni za kutembea mtaa kwa mtaa (walking campaign ) ndani ya Kata ya Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, akiwaombea kura wagombea wa chama hicho katika nafasi mbalimbali.Katika kampeni hizo, Manara aliwaomba wananchi wa Kariakoo kumpigia kura Mgombea Urais wa CCM, Dkt.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu, pamoja na yeye mwenyewe katika nafasi ya Udiwani wa Kata ya Kariakoo.Akiwa katika matembezi hayo, Haji Manara alitembelea mitaa mbalimbali ya kata hiyo na kuzungumza na wananchi, akiahidi kwamba endapo watamchagua kuwa diwani wao, atahakikisha wananchi hawasumbuliwi tena na mgambo, huku akiahidi kujenga Kariakoo yenye neema na ustawi kwa wote kuanzia kwa wafanyabiashara hadi kwa wakazi wa eneo hilo.

Kampeni hizo zimefanyika ikiwa ni siku moja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika kesho, Oktoba 29, 2025, ambapo wananchi nchini kote wanatarajiwa kwenda kupiga kura kuwachagua viongozi wao katika ngazi mbalimbali za uongozi.
 
Back
Top Bottom