DullyJr
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 13,979
- 11,816
Ameandika Mwanaharakati Yericko Nyerere
"Hii haikubaliki, hii ni dhihaka, dharau na kutweza utu wa Msemaji Mkuu wa @yangasc ndugu @alikamwe na Mkuu wa Digital ndugu @privaldinho ambao ndio wana ithibati ya kuisemea Yanga na kubuni falsafa ya uongozi wa kiusemaji na mwelekeo wautakao.
Anachokifanya Ndugu Haji Manara ni kuwaingilia uhuru na ubunifu wao katika kazi na kuwafanya wajinga, akiwalazimisha wafanye kazi vile anavyotaka yeye. Hii haikubaliki. Haji si mfanyakazi wa Yanga, Bali ni rafiki wa GSM ama tuseme ni (influencer) tu, asivuke mipaka kwenda kuwavuruga vijana hawa Ali Kamwe na Privadinho ambao kwa miezi kadhaa waliyokaa pale Yanga wemeleta falsafa yao nzuri ya kiuongozi (ryrithim), ambayo imeifanya klabu ya yanga kuongeza hamasa na kuongeza uwingi wa mashabiki mitandaoni kwa sasa.
Manara aelezwe ukweli na uwazi akubali kupokea ukweli huo kwamba sio msemaji tena wa Yanga, yaani yuko nje kabisa ya mfumo wa yanga. Bado anatembea na Apedomia kichwani akiamini kwamba mafanikio ya Yanga yametokana na yeye. Anaamini kwamba yeye bado ni msemaji wa Yanga. Hii ni mbaya sana. Leo anawafanyia hivi Wasemaji wa klabu, Kesho atamfanyia utovu wa nidhamu Rais wa Yanga Boss @caamil_88 na akichekewa siku atamnyea mbovu Tajiri Gharib Mohamed. Ndio! Huyu hana dogo, anaweza kufanya chochote huyu kijana. Rejaa utovu wa nidhamu na udharimu aliomfanyia aliyekuwa Mtendaji wa @simbasctanzania @bvrbvra na tajiri na mwekezaji @moodewji
Ndugu na rafiki yangu Kaka yangu @caamil_88 nakuomba sana liangalieni kwa makini hili, Mwelezeni wazi Manara kuwa sio msemaji wa Yanga, azungumze kama shabiki wa kawaida huko vichochoroni, sio kutweza watendaji na viongozi wa timu. Vijana hawa Ali Kamwe na Priva klabu imewekeza pesa nyingi kwao, na wameanza kuleta matunda mengi kwa klabu, leo makampuni makubwa yanakuja kuwekeza kwasababu mtandao wa mashabiki umekuwa mkubwa kupitia vijana hawa wenye nidhamu, ucheshi na adabu mbele za kila mpenda soka"