DOKEZO Mamlaka zifike Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC SAME) kuna mazingira ya rushwa na kutowajibika

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mdau niliye ndani ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC SAME)

Kumekuwa na changamoto ya Mkuu wa Chuo kutopenda kuhojiwa kuhusiana na masuala ya matumizi ya fedha.

Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa mgogoro mkubwa baina ya baadhi ya Watumishi, Mlinzi na Mkuu wa Chuo.

Kuna mambo mengi ya hovyo yanayofanyika lakini nitaje mawili ya mfano:-

1. Matumizi ya zaidi ya Shilingi milioni 2 yaliyotumika kutengeneza gari la Serikali kwa kushirikiana na Mkuu wa Idara ya Ufundi na bado halikupona lakini hakuna mwingine aliyeshirikishwa wala kikao kilichopitisha matumizi hayo.

2. Mkuu kwa kushirikiana na Mkuu wa Idara ya Ufundi, kununua gari la mafunzo ambalo halitembei wala halifanyi kazi (used) kwa zaidi ya shilingi Milioni 3.5.

Mambo kama hayo na mengine mengi yanasababisha akiwa anahojiwa na watu anatengeneza chuki.

Tunaomba Wizara kupitia maafisa Utumishi isaidie kutatua mgogoro huu wa Mlinzi na Mkuu wa Chuo, maana imesababisha hadi aandikiwe barua ya kumchafua na kumnyima likizo ambayo ni haki yake, hili tatizo ni kubwa hata kwenye vikao akitoa hoja anafokewa sana.

Waje wafuatilie na ikionekana Mkuu ana matatizo aonywe na ikionekana Mlinzi ana matatizo aonywe pia. Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom