Afisa aliyeshitakiwa kwa kupokea rushwa ili kutoa Kitambulisho cha Taifa kwa Raia wa Uganda si mtumishi wa NIDA

Aug 15, 2011
30
11
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kukanusha taarifa iliyoandikwa katika mtandao huu leo ikiwa na kichwa cha Habari kisemacho "AFISA NIDA ASHTAKIWA KWA KUPOKEA HONGO KUTOA KITAMBULISHO KWA RAIA WA UGANDA"

Tunapenda kuufahamisha Umma na watanzania wote kwa ujumla kuwa NIDA haina Mtumishi aitwaye Lilian Stanslaus Mwangwa katika ofisi ya Usajili wilaya ya Ilemela au mahali pengine popote.

Aidha tunatoa onyo kwa mtu yeyote atakaye bainika na kuthibitika kujifanya ni Afisa wa NIDA huku akijua fika kuwa si Mtumishi wa NIDA, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO
MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA
 
Kuna uwezekano mkubwa wa raia wengi kutoka nchi jirani, kumiliki vitambulisho vya Taifa. Maana watendaji wengi serikalini, siyo wazalendo.
 
Back
Top Bottom