Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepotezazaidi ya shilingi bilioni moja

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imepoteza
zaidi ya shilingi bilioni moja kutokana na wauzaji
wa kanda za muziki na filamu kutobandika stempu
halasi za kodi.

Richard Kayombo, Mkurungezi wa
Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
amesema hayo wakati
akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam,
MwanaHALISI Online lilikuwepo.

Kayombo amesema, stempu za kodi katika muziki
na filamu hutolewa na TRA kwa ajili ya kuhakikisha
bidhaa hizo ili kulinda kazi za wasanii nchini na
baada ya hapo ndipo huingizwa sokoni.

“Kwa mujibu wa sheria ya ushuru wa bidhaa kanuni
za ushuru wa stempu kwenye bidhaa za filamu na
muziki ya mwaka 2012 inasema, watakaobainika
watatozwa faini isiyopungua shilingi milioni tano au
kifungo kisichopungua miaka mitatu jela,” Kayombo
amesema.

Pamoja na hayo TRA imewatahadharisha wananchi
kuwa makini wakati wa kununua bidhaa halali
ambazo zimebandikwa stempu za kodi na kuwa,
kinyume cha hapo, watoe taarifa katika ofisi yoyote
ya TRA.
 
Back
Top Bottom