Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yakiri ubovu wa barabara kinyume na kauli ya RC Arusha

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mkuu wa mamlaka hiyo akiwa na timu ya askari amaedai wamehamishia shughuli zao katika eneo lililoaribiwa na mvua zinazoendelea kunyesha na kwamba hawatatoka hadi miundombinu itengamae.

Wakati hayo yakijiri RPC wa Arusha ameeleza kwamba wapo katika hatua za kuwasaka wahujumu uchumI waliopiga picha barabara hiyo na kusambaza mitandaoni huku akimwelekeza Mbunge wa Arusha Mjini kukaa mbali na jambo hilo na asitafute mtaji wa kisiasa.

Haya yanajiri baada ya video kusambaa zikionesha ubovu wa barabara katika hifadhi hiyo jambo lililopelekea Mkuu wa Mkoa wa Arusha kukemea tabia ya watu kusambaza taarifa zinazochafua taswira ya nchi kwenye mitandao badala ya kuripoti matatizo yao katika mamlaka husika yaweze kupatiwa ufumbuzi. RC Gambo alikwenda mbali zaidi na kufananisha kitendo cha kusambaza taarifa hizo kama kosa la uhujumu uchumi.

Baada ya mamlaka kujitokeza na kueleza madhara yaliyoletwa na mvua zinazodaiwa kuanza kunyesha septemba hadi sasa, wadau mbalimbali wameibua majadiliano wakihoji ni nani yupo sahihi kati ya mchukua video aliyeisambaza mitandaoni na kuzifikia mamlaka za serikali, RC aliyepiga vita tabia ya kusambaza picha na Muhifadhi Mkuu aliyekiri uwepo wa tatizo na kulitaftia ufumbuzi.

Baadhi ya wadau wameendelea kuhoji, je kitendo cha Mamlaka kukiri na kupeleka timu huku wakitumia vyombo vya habari kuwahabarisha wananchi juu ya kile serikali inafanya haiwezi kuibua msuguano wa kiutendaji na kuwafanya waonekane wamekwenda kinyume na maelekezo au mtizamo wa RC?

Wengine wanahoji, kwanini RC hakujikita katika kutafuta suluhisho la tatizo kwani ni ukweli ulio wazi kwamba eneo la hifadhi halijengwi barabara za lami na ni jambo la kawaida barabara za vumbi kuaribiwa na mvua au hata magari na kila wakati hufanyiwa ukarabati, kwanini aliona kama njia iliyotumika ililenga kuhujumu uchumi na si kuujenga uchumi?

Wadau wengine wanahoji wizara yenye dhamana ilikuwa wapi hadi uharibifu kama huo unatokea na hawakuchukua hatua? Mamlaka ilikuwa wapi hadi kero inakuwa kubwa kwa kiasi hiki?

Je, njia sahihi za kufikisha ujumbe kwa serikali ni ipi na imeandikwa wapi? Tumezoea wananchi wakiibua hoja dhidi ya changamoto wanazokabiliana nazo, hoja hizi uibuliwa katika mikutano ya adhara mbele ya vyombo vya habari, je huu ni uhujumu uchumi?
 
Mimi nadhani mwenye kupiga picha hakuwa na nia mbaya ila alitaka ujumbe uwafikie wahusika na hivyo wahusika wameanza kuchukua hatua za haraka.
 
Bila ile video wasingekarabati hapo. AR wamepata RC zwazwa sana

Waziri mwenye dhamana nae anashinda twitani na instagramu kujibu "mafans" wake.
Umenichekesha sana hapo uliposema, bwana yule kazi yake kubwa ni kushinda twitan na kuwafurahisha fans wake!

Hahahaaaaa :D 😆

Kama alivyowahi kukiri hadharani Jiwe, katika moja ya ziara zake kule kanda ya ziwa, kuwa yeye anateua wendawazimu wenzake!
 
Jeshi la polisi litumie weledi, si kila maelejezo ya kisiasa ni ya kutekeleza.

Uwezekano mkubwa picha zilipigwa na wahanga madereva wa tour, kitendo cha kuwachokonoa kitaamsha hasira kwa wadau sector utalii wahanga. Mwisho wa siku kuharibu sector muhimu.

Kubwa Mwenyekiti bodi Tanapa msizibane sana maamlaka mafungu ujenzi na uboreshaji barabara.
 
Vitu vingine vya kijinga sana,ivi barabara ikiwa mbovu nayo ni siri? Viongozi wengi saizi wanakosa quality of leadership..........yaani hata taarifa za habari za local television binafsi siangalii maana unaweza sikia ujinga siku yako ikaharibika kabisa
 
Jeshi la polisi litumie weledi, si kila maelejezo ya kisiasa ni ya kutekeleza. Uwezekano mkubwa picha zilipigwa na wahanga madereva wa tour ,kitendo cha kuwachokonoa kitaamsha hasira kwa wadau sector utalii wahanga. Mwisho wa siku kuharibu sector muhimu.
Kubwa mwenyekiti bodi Tanapa msizibane sana maamlaka mafungu ujenzi na uboreshaji barabara.



Sent using Jamii Forums mobile app
Weledi upi huo polisi wanao
Majority reasoning yoa ipo chini kwenye mambo yenye tija

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu vingine vya kijinga sana,ivi barabara ikiwa mbovu nayo ni siri? Viongozi wengi saizi wanakosa quality of leadership..........yaani hata taarifa za habari za local television binafsi siangalii maana unaweza sikia ujinga siku yako ikaharibika kabisa
Hatuangalii reasoning bali uwezo wako binafsi wa kuumiza upinzani ndio CV yako.
 
Back
Top Bottom