Ujinga mtupu
JF-Expert Member
- Aug 16, 2017
- 852
- 1,905
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa wito kwa Watumishi wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa Waadilifu na utendaji wa haki katika kuwahudumia Wananchi wanaofika katika Mamlaka hiyo hususani wanaofika kupata huduma za kupima vinasaba (DNA).
Waziri Ummy amesema hayo, wakati alipofanya ziara ya uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na kuongea na Watumishi katika Ofisi hizo zilizopo Jijini Dodoma.
Waziri Ummy amenukuliwa akisema “Kazi yenu hii inauhusiano wa karibu na mambo ya kutenda haki, na Mimi kwasababu ni Mwanamke, kwahiyo katika suala la kuchunguza uhalali wa Baba wa Mtoto ni yupi napenda sana tuwe Waadilifu ili kutenda haki ya kweli bila kuonea yoyote”