Mamlaka Jiji la Arusha hamuoni haya matuta barabarani?

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
5,050
5,078
Nnawasalimu sana wakuu,

Hapa Arusha barabara za katikati ya mji zimejaa matuta yaliyotokana na kuzibwa kwa mashimo. Inashangaza sana kuona Mamlaka zipo tena ndizo zinatoa tenda kwa wakandarasi hawa wanaoziba mashimo na badala ya kuziba mashimo husika wanatengeneza matuta makubwa barabarani.

Hivi kweli hawa wakandarasi wazawa wanaolalamika kukosa kazi ndio wanaofanya mambo kwa kulipualipua namna hii? Kama kipimo chao ndio haya matuta wanaweza kupewa kweli barabara za kilometa kuanzia 30?

Jambo la kishangaza kabisa RC na timu yake wapo na wanapita kwenye njia hizohizo, ina maana hata kusimamia uzibwaji wa viraka mpaka Rais aseme?

Barabara zote zinazoingia katikati ya mji kuanzia Mianzini-Stand Kuu, kutokea Azimio kupita ofisi ya RC kwenda mpaka Njiro na Moshi hovyo. Kipande cha Barabara ya kutokea mjini kwenda Ungalimited mpaka geti la Sunflag mashimo matupu na hakuna jitihada zozote za kuondoa kero hiyo.

Hili swala lipo pia Dodoma viraka vikizibwa shimo linaondoka na kuwekwa tuta. Mnaohusika chukueni hatua ili tusioshie kusema mnakula ten percent kwenye hizo tenda.

Aibu yenu
 
Mkuu,Gambo yupo busy akigawa bima za afya kutokana na 10% alizochukua kwenye hiyo miradi ya barabara
Pili ukisubiri Jiwe aingilie kati utakuwa unapoteza muda wako bure hana habari na Chuga
 
Alooo yaani unaendesha gari katikati ya Jiji lkn unaweza fikiri uko Mbulu huko ndanindani, mashimo, matuta kila mahali hakuna unafuu, yaani ukiona shimo unajua tu kinachofuata ni tuta.

Mkuu,Gambo yupo busy akigawa bima za afya kutokana na 10% alizochukua kwenye hiyo miradi ya barabara
Pili ukisubiri Jiwe aingilie kati utakuwa unapoteza muda wako bure hana habari na Chuga
 
Alooo yaani unaendesha gari katikati ya Jiji lkn unaweza fikiri uko Mbulu huko ndanindani, mashimo, matuta kila mahali hakuna unafuu, yaani ukiona shimo unajua tu kinachofuata ni tuta
Siku za hizi karibuni niliwaona wanaweka alama kwa baadhi ya barabara(friends corner- uswahilini, clock tower - kijenge, njiro) then wakapotea baada ya kurudi wakaanza kuchimba chimba tn then wakasepa tena.

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom