News Alert: Mamlaka alopewa polisi

permist

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
615
360
Habari zenu? Leo napenda tukumbushane mambo muhimu kidogo ya kisheria kwa ajili ya utendaji wa kazi kitaalamu wa polisi.
1.k/f 19 CPA,CAP 20 1985 R:E 2002. Kinampa mamlaka askari polisi kumkamata mtuhumu yoyote aliyekimbilia ndani ya nyumba yoyote isipokuwa mahakamani,bungeni na ubalozini ampapo kuna taratibu nyingine.

2. K/f 20 CPA hiyohiyo inampa mamlaka askari polisi kufunja nyumba yoyote wakati akiwa anafanya kazi zake za kipolisi.

3.K/f 21 CPA Hiyohiyo inampa mamlaka polisi kutumia nguvu wakati wa ukamataji,nguvu hiyo ifanane na hali halisi.

4. K/f 25 CPA hiyohiyo inampa mamlaka polisi kusimamisha,kupekua na kushikilia chombo cha moto chochote kukiwa na sababu ya msingi.
 
Back
Top Bottom