GE2025 Mamilioni wanayolipwa Wabunge ndani ya Miaka mitano ndio chanzo cha kila mtu kutaka Ubunge?

GE2025 Mamilioni wanayolipwa Wabunge ndani ya Miaka mitano ndio chanzo cha kila mtu kutaka Ubunge?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,601
Wakati Bunge la Jamhuri ya Muungano litakapokuwa limevunjwa Agosti 3, 2025, kinachofuata baada ya hapo ni Wabunge kulipwa mafao yao baada ya kutumia nafasi zao kwa miaka mitano.

Hata hivyo, kumekuwa na minong’ono kuhusu mafao manono watakayovuna Wabunge hao. Japo malipo hayo hayajawahi kuwekwa wazi, lakini gazeti moja la Mtandaoni la kila wiki la Pambazuko limedai kuwa kila Mbunge anatarajiwa kulamba kitita cha zaidi ya Sh Milioni 400.

Kiasi hicho cha fedha kimedaiwa kulipwa kutokana na vyanzo, wakiwamo Wabunge wenyewe walinukuliwa na gazeti hilo.

Kama kiasi hicho cha mafao kitalipwa kwa Wabunge wanaofikia 393, basi Serikali itatumia zaidi ya Sh Bilioni 157.2 kulipa mafao hayo.

Kiasi hicho cha malipo kimezua mjadala miongoni mwa Wananchi, huku baadhi wakihoji, iweje mbunge alipwe mafao hayo, ilihali mtumishi wa umma aliyetumia nchi kwa zaidi ya miaka 30 aambulie kiasi cha Sh Milioni 100 anapostaafu na umri wa miaka 60?

Akizungumza kwenye kipindi cha Kunani Bungeni? Kilichorushwa na TBC Digital, wiki iliyopita Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia cha Dk Salim Ahmed Salim kilichopo Kurasini Dar es Salaam, Deus Kibamba, alisema sababu zinazochangia watu wengi kupigana vikumbo kusaka Ubunge ni pamoja na mishahara minono, posho maalum, posho za vikao, fedha za jimbo, matibabu daraja la kwanza na mkopo wa gari wenye masharti nafuu.

Soma pia: Mishahara minono ya wabunge

Kwa mujibu wa Kibamba, iwapo Tanzania haitarekebisha taratibu na kuzifanya nafasi za kisiasa kuwa na malipo makubwa ya mishahara na marupurupu, basi isahau suala la maendeleo.

Kibamba ameonya kuwa endapo hakutakuwa na udhibiti wa malipo na mishahara mikubwa kwenye kazi za Siasa, Taifa litachelewa kupata maendeleo tarajiwa.

Alisema kutokana na malipo hayo kwa Wabunge, haishangazi kuona Profesa wa Chuo Kikuu akitelekeza taaluma yake na kukimbilia Bungeni kukimbilia mafao manono.

“Sababu nyingine inayovutia watu kukimbilia bungeni ni mfumo wa kisiasa na uchaguzi, ambapo wabunge wana uwezo wa kupata wanachokitaka kupitia sheria na kanuni mbalimbali wanazozitunga kulinda maslahi yao.

“Nchi hii tusipodhibiti manono ya kisiasa ya wabunge, maendeleo tutasubiri sana. Leo hii profesa wa chuo kikuu, daktari bingwa wa upasuaji, wanaacha hospitali, wanaacha mikasi wanakwenda kugombea kuingia bungeni,” alisema.

Hata hivyo, mmoja wa Wabunge anayemaliza muda wake aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake, alisema wanacholipwa kwa mwezi ni mshahara ambao ni zaidi ya Sh Milioni 3 na posho ya jimbo Sh Milioni 8 ambazo kwa jumla ni zaidi ya Sh Milioni 11.

Kuhusu mafao ya Ubunge, amekanusha kulipwa Sh Milioni 400, bila kutajwa wamelipwa Shilingi ngapi.

“Unajua Mbunge anaruhusiwa kuchukua mafao yake hata baada ya mwaka wa kwanza? Kwa hiyo mimi nilishachukua nikazitumia, lakini siwezi kusema tumelipwa shilingi ngapi,” alisema Mbunge huyo.

Akizungumza katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Wasafi, Mei 9, 2025, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alisema mshahara wa Mbunge hauna utofauti na mishahara na Watu anaolingana nao katika kada ya utumishi wa umma, pengine Watu awafahamu kwamba Mbunge ni sehemu ya mtumishi wa umma.

“Mshahara wa Mbunge wala hauna tofauti na mishahara ya watu anaolingana nao katika Kada ya Watumishi wa Umma. Pengine watu hawafahamu kwamba Mbunge ni sehemu ya utumishi wa umma.

“Kwa hiyo hata ile mishahara iliyotajwa huko nyuma kwamba kwenye taasisi sijui wanalipana kiasi gani, Mbunge ni Mtumishi wa Umma,” alisema.

Alipoulizwa analingana na nani, alisema anaweza kulingana na Mkuu wa Wilaya.

Julai 15, 2025, akizungumza katika mahojiano na Wasafi FM, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amedai kuwa Wabunge wanaomaliza muda wao mwaka huu wamelipwa Sh Milioni 18 kila mwezi, ukiwemo mshahara na marupurupu ya jimbo.

Soma pia: Heche: Nikiwa Mbunge kwa mwezi tulilipwa Sh 12.7m

“Mbunge analipwa mshahara, mimi nilipokuwa Bungeni, mshahara wetu ulikuwa Sh Milioni 4, lakini hapa pembeni kuna kitu kinaitwa Jimbo Allowance, hiyo haikatwi kodi Sh Milioni 8 kila mwezi. Kwa hiyo Mbunge akichukua mshahara inakuwa Sh Milioni 12, sasa hivi ni Sh Milioni 18,” amedai Heche.

Sheria inampa mamlaka makubwa Rais
Sheria ya Mishahara na Marupurupu ya Mawaziri na Wabunge, Sura ya 234 inampa Rais mamlaka ya mwisho ya kuamua mishahara na marupurupu ya viongozi wa juu wa serikali, ikiwa ni pamoja na wabunge, mawaziri, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais.

Sheria hiyo inaweka mfumo rasmi wa malipo lakini pia inaacha nafasi kwa Rais kubadili au kurekebisha viwango kulingana na mazingira na majukumu.

Hatua hiyo inaacha maswali kuhusu uhuru wa mhimili wa Bunge ikiwa mhimili wa utawala ndio unaamua masilahi yote.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mishahara na Marupurupu ya Mawaziri na Wabunge, Sura ya 234 Wabunge na Mawaziri watalipwa mishahara kulingana na viwango vya mishahara vya Utumishi wa Umma na kwa kiwango ambacho Rais ataamua kwa amri rasmi.

“Rais anaweza kuamua viwango tofauti vya mishahara kulingana na uzito wa majukumu ya kila ofisi.”

Kifungu cha 4 kinasema, “Mmiliki (mbunge, waziri) anaweza kuchagua mshahara wa juu,” huku kifungu cha 3 kikisema, “mtu anayeshika ofisi chini ya Sheria hii na ambaye kwa mujibu wa sheria nyingine au cheo kingine anastahili mshahara wa juu, anaweza kuchagua kulipwa mshahara huo wa juu badala ya ule wa kawaida.”

Kuhusu marupurupu ya mawaziri kifungu cha 5 kinasema, wamiliki wa ofisi za mawaziri watalipwa marupurupu kwa mujibu wa maandishi rasmi ya rais na rais anaweza kuweka viwango tofauti vya marupurupu kulingana na uzito wa majukumu ya kila ofisi.

Kwa marupurupu ya wabunge Kifungu cha 6 kinasema, mbunge atalipwa marupurupu kwa viwango vitakavyoamuliwa na Rais kwa maandishi, kulingana na vyeo ambavyo ni pamoja na Spika, Naibu Spika na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu watakuwa na marupurupu ya uwajibikaji.

Kwa Mbunge wa jimbo, watakuwa na posho ya jimbo, mbunge asiye wa jimbo atalipwa posho maalum, na kwa mbunge yeyote atakuwa na posho ya usafiri au posho ya mafuta kwa gari binafsi, posho ya kujikimu, marupurupu mengine yoyote kama Rais atakavyoamua.

Kifungu cha 7 kinasema, rais anaweza kupitia upya mishahara na marupurupu na kila mara anapoona inafaa, kupitia na kubadilisha mishahara au marupurupu yaliyowekwa chini ya sheria hiyo.

Kifungu cha 8 kinasema mishahara na marupurupu yote chini ya Sheria hii yatatolewa kutoka kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali (Consolidated Fund).

Maswali kuhusu malipo ya wabunge yamekuwepo kwa muda mrefu. Januari 2014, Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) lilihoji sababu ya wabunge kujipitishia malipo ya mafao ya ubunge ya Sh Milioni 256 kwa kila mmoja.

Malipo hayo yalikuwa yameongezeka kwa asilimia asilimia 274 ikilinganishwa na yale yaliyotolewa mwaka 2010 na yalikuwa yameidhinishwa na hazina mwishoni mwa Mwaka 2013.

Kwa mujibu wa BBC, wabunge hao ambao wakati huo walikuwa 375 walikuwa wakilipwa mshahara wa Sh18.28 milioni kwa mwezi na walikuwa wakipokea Sh57.99 milioni kwa kuhudhuria vikao vya bunge pamoja na posho ya matunzo ya kila mwaka ya takriban Sh33.96 milioni.

Pia soma ~ Deus Kibamba: Mbunge akimaliza miaka mitano Bungeni anapewa kiinua mgongo Sh Milioni 380+
 
Katika vitu vinavyoitia umasikini hi nchi ni pamoja mishahara , marupurupu na mafao ya wabunge

Alafu Cha kushangaza Kila siku bado wanaomgeza idadi ya majimbo Ili kuendelea kuchoma Kodi za wananchi
 
Hii nchi inawezi sana Mbunge kwa kazi gani anayofanya kiasi kwamba yeye achukue milioni 400 ni mda, wananchi tuamke tutoke usingizi kwa kazi gani anayofanya mbunge kugonga Meza?
 
Sababu ndiyo hiyo,wapunguze pesa tuone wazalendo wa kweli.
 
Kiukweli huo mshahara wa wabunge sio mkubwa kivile ni Kwa sababu sisi wengine tunalipwa kidogo sana hivyo tunaona wabunge wameula. Hebu fikiria 18M ni Dola ngapi?
 
Sababu za kila mtu hizi hapa:
1. Mamilioni wanayolipwa.
2. Ukosefu wa ajira (ubunge na udiwani vikegeuka kuwa ajira).
3. Kufanikisha illegal deals (ukishakuwa mhe kila deal linawezekakana).
 
Isingekua ubunge Mo Dewji asingepata taarifa mpaka kufikia mchakato wa kununua mashamba ya mkonge aliyoyakopea pesa na kuendeleza biashara zake.

Kuna maslahi mapana kwenye ubunge.
 
Ndio rais wa chura ame dabo KK anatafuta ubunge kwa hali na mali hadi akaenda kuchangia ccm dinner gala 100 millions bila ridhaa ya wanachama wa klabu.
 
Back
Top Bottom