Elizabeth Dominic
Platinum Member
- Dec 7, 2007
- 4,555
- 3,658
Safi sana
Chadema ni msingi
Chadema ni msingi
Mkuu naona sasa umeamua kuhamishia kitanda humu.
teh teh,nchi ipi? Kigoma?Habari ya mjini ni zitto kuzidi kutikisa nchi
teh teh, nimeipenda hiyo, inaonekana ni division 5 huyo!Kakae na mwalimu wako wa hesabu za darasa la kwanza umuulize watu 85 wa Pangani + watu 70 wa kiomoni wilayani Tanga jumla yake ni ngapi?!
Ukipata jibu kameze panadol upumzike.
Wanachama 85 waliokuwa CUF, ADC na CCM wilayani Pangani wamehamia CHADEMA leo mara baada ya kukutana na katibu wa kanda ya kaskazini Bw Amani Golugwa alipo kuwa anafanya ziara ya kukagua zoezi la Chadema ni msingi wilayani humo.
Miongoni mwa wamachama hao alielezea namna walivyo wahi kupelekwa kisiwani Pemba wakiwa wamevalishwa mavazi ya kijeshi ili wakapigie kura chama tawala wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010.
Zoezi la chadema ni msingi linaendelea kwa kasi mkoani Tanga huku mamia ya wananchi wakizidi kujiunga na chadema, miongoni mwa wananchi hao amekemea propaganda mbaya za udini zilizokuwa zinatumiwa na ccm dhidi ya vyama vya upinzani kwa kusema kuwa zimechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta mgawanyiko na malumbano ya udini yasiyo kuwa na tija kwa taifa.
Alisema mara zote ccm wamewaaminisha watu wa Pangani kuwa CUF ni chama cha waislamu na chadema ni chama cha wakristo lakini hakuna hata siku moja ambayo ccm wamesha wahi kusema kuwa wao ni chama cha watu gani. "...Baada ya sisi kutumiwa sasa tumeamua kufuata chama chenye dhamira na nia ya dhati kutukomboa"
Jana wanachama zaidi ya 70 wa kata ya kiomoni wilayani Tanga ambayo hivi karibuni kwenye uchaguzi wa kitongoji chadema iliibuka mshindi wamejiunga na chadema na wako kwenye maandalizi ya kushinda kiti cha udiwani kilicho wazi kwenye uchaguzi mdogo unao tarajiwa kufanyika mapema mwezi Februari.
Kuna watu wajinga mnajifanya mna akili lakini kumbe kichwani ni mbulumundu plus plus. Umeambiwa mamia ya watu waamia chadema. Hao 85 ni wale waliotokea ADC, CUF na CCM tu. Angeanza kutaja wa NCCR,TLP Pona, SAU, Chaumma wangefika idadi ya mamia. Hao 85 ni wa CUF, CCM na ADC.
Mgosi Mohamedi Mtoi asante kwa taarifa ya kutia moyo kwenye harakati hizi za kumtoa mkoloni mweusi
Mtoi,
acha uongo, gharama ya uongo ni kubwa mana inaweza kukushushia heshima na thamani a utu wako
ktk taarifa yako umetoa takwimu za watu 85 na hapo hapo 70. Unapodanganya jitahidi kuwa na kumbukumbu
Hayo mamia ako wapi, mbona unaonekana peke yako?