Mambo yote ya CCM sasa yalianzishwa na Mzee Kikwete hakuna

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Wanabodi kuna mambo yanafikirisha sana yote wanayosema awamu ya tano imefanya mbona ni mambo yaliyopo kwenye hotuba ya kikwete ya kufunga bunge mwaka 2015

Hivyo Kikwete alibuni mambo mengi sana na kuanza kuyatekeleza mfano Flyover za Ubungo na TAZARA ingawa sasa zimejengwa kama daraja tu

Mwaka 2015 wakati anafunga bunge kwenye hotuba yake Kikwete vijiji zaidi ya 5,000 vilipata umeme ,Sasa hii idadi ya 8000 mnajumlisha na ya Kikwete au?

Hotuba hii ya kufunga bunge chini inathibitisha hayo mwaka 2015 kikwete alipohutubia

Soma

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Hotuba ya Rais Kikwete kuliaga Bunge - 09, Julai 2015
 
Tuna tatizo mahali.

Si ndiyo sisi tunaolalamika kila siku serikali ya Tanzania haina utaratibu wa kupokezana vijiti?

Kila anayekuja anakuja na vyake?

Maendeleo yanaenda hivi sio kila anayekuja anayatupilia mbali ya mwenzake. Nilidhani tutawasifu kumbe limekuwa tatizo tena.
 
Mkuu hawa wa awamu ya tano wanasema toka uhuru wao ndio kiboko lakini

Moja,Hotuba ya kikwete alieleza uchumi unakuwa na bado kidogo uchumi ufike uchumi wa chini wa kati

Pili,Miradi ya Flyover,Mwendokasi na umeme ,Miradi ya barabara mitaani kwa msaada wa world Bank yote ameongelea kwenye hotuba

Sasa kipi kipya ambacho wamekibuni awamu ya tano?
 
Bwawa la umeme, reli, viwanja vya ndege ukarabati, Msalato & Chato.

Vituo vya Afya, wafanyakazi hewa, kufufua reli, Elimu sawa na bure, ATC, kuikataa mikataba ya hovyo kama ule wa ujenzi wa bandari n.k

Lakini kikubwa hajatupilia mbali yaliyokwishaanzishwa na wenzake...kayaendeleza.
 
Huyu wa sasa yeye ni nyapara
Wanabodi kuna mambo yanafikirisha sana yote wanayosema awamu ya tano imefanya mbona ni mambo yaliyopo kwenye hotuba ya kikwete ya kufunga bunge mwaka 2015

Hivyo Kikwete alibuni mambo mengi sana na kuanza kuyatekeleza mfano Flyover za ubungo na Tazara ingawa sasa zimejengwa kama daraja tu

Mwaka 2015 wakati anafunga bunge kwenye hotuba yake kikwete vijiji zaidi ya 5,000 vilipata umeme ,Sasa hii idadi ya 8000 mnajumlisha na ya kikwete au?

Hotuba hii ya kufunga bunge chini inathibitisha hayo mwaka 2015 kikwete alipohutubia

Soma

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
Hotuba ya Rais Kikwete kuliaga Bunge - 09, Julai 2015
 
Back
Top Bottom