pmwasyoke
JF-Expert Member
- May 27, 2010
- 4,594
- 2,981
Hivi sasa kuna mgomo wa wafanyakazi karibu wote wa serikali wa ngazi za kati na chini nchini Malawi.
Wanaoendelea na kazi, ni madaktari na manesi tu ambao pia wanasema watajiunga na mgomo huo baada ya siku kadhaa iwapo madai ya wafanyakazi hayatekelezwi.
Viwanja vya ndege vimefungwa, mipaka haipitiki, shule zote za serikali zimefungwa, maofisi ya serikali yamefungwa nk.
Wafanyakazi wanataka nyongeza ya mshahara ya asilimia 67 na mambo mengine kadha wa kadha yahusianayo na kuboreshwa vipato na mazingira ya kazi.
Rais Banda, mara alipochukua madaraka mwaka jana baada ya kifo cha Bingu wa Mutharika, alidevalue kwacha na kuachia thamani yake ifloat. Hii ilikuwa kukubaliana na masharti ya IMF. jambo hili limesababisha hali ngumu sana kwa watu wa kawaida kwa sasa - japo wanaambiwa huko mbele hatua hizi zitasababisha recovery nzuri ya uchumi.