Mambo yatakayoing'oa CCM madarakani October 2015

emmanuel1976

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
301
Reaction score
80
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini CCM imekuwa ikikabiliana na changamoto kali kutoka vyama pinzania wakati wa chaguzi isipokuwa uchaguzi wa uliomweka madarakani Mh. Dr. Jakaya Kikwete mwaka 2005 ambao angalau ulikuwa na unafuu. Watanzania wamekuwa wakilalamikia baadhi ya mambo ambayo wanadhani yalihitaji marekebisho kutoka chama tawala. Wamekipa muda wa kutosha chama tawala ingawa ni kama vile sikio la kufa huwa halisikii dawa. Mambo yale yale yaliyolalamikiwa na kupigiwa kelele yameendelea kufanyika ndani ya serikali ya chama tawala.

BAADHI YA MAMBO YATAKAYOING'OA CCM MADARAKANI 2015

  1. Makundi yaliyojenga uadui na uhasama ndani ya chama.
  2. Ufisadi uliokithiri. Hii haihitaji tafsiri.
  3. Rushwa iliyopindukia.
  4. Kukosekana kwa huduma za jamii za lazima kwa wananchi. Mfano; Elimu duni, huduma za afya, nishati ya umeme na maji, nk.
  5. Ukosefu wa ajira kwa vijana wengi.
  6. Mahakama ya kadhi. Hiki ni kisu chenye makali kuwili. Upande mmoja kuna wakristu na upande wa pili waislamu. Walioingiza jambo hili kwenye ilani ya ccm hawakuwa wanaona mbali.
  7. Migogoro ya wakulima na wafugaji.
  8. Kutupwa kwa rasimu ya katiba ya jaji Joseph Sinde Waryoba ambayo ndiyo maoni ya wananchi.
  9. Dai la jeshi la polisi kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia. Dai hili linaambatana na wananchi kubamkikiziwa kesi za uongo.
  10. Dai la udhaifu wa wengi wa wabunge wa ccm kutokusimamia mambo muhumu yenye maslahi ya taifa bungeni badala yake wengi wao wamekuwa watu wa ndiyoooooooooooooo!
  11. Kupuuzwa kwa madai ya maslahi ya wafanyakazi wa umma.
  12. Muungano wa ukawa ambao ni zao la kupuuzwa kwa rasimu ya katiba ya jaji J.S.Waryoba
  13. Kupitishwa kwa sheria ya makosa ya mtandao???????
  14. ​Migogoro ya ardhi
  15. Mengine ongezea

16. Kuanguka kwa thamani ya shilingi imesababisha hasara kubwa kwa mabenki, wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji
17 kupeana wao kwa wao nafasi za uongozi (uswahiba)
18. watoto na jamaa wa vigogo kulindwa-Kumesababisha matabaka katika nchi
19. kushamiri kwa madawa ya kulevya pamoja na uvunaji wa maliasiri zilizopo bila ya woga kwa maslahi yao
20. Usimamizi mbaya wa mapato ya taifa
 
16. Kuanguka kwa thamani ya shilingi imesababisha hasara kubwa kwa mabenki na wafanyabiashara wakubwa
17 kupeana wao kwa wao nafasi za uongozi (uswahiba)
18. watoto na jamaa wa vigogo kulindwa-Kumesababisha matabaka katika nchi
19. kushamiri kwa madawa ya kulevya pamoja na uvunaji wa maliasiri zilizopo bila ya woga kwa maslahi yao

Mkuu Freedom Tomorrow! kumbe kinaweza andikwa kitabu cha sababu zitakazo fanya ccm ing'olewe madarakani 2015 ikiwa wapinzani/ UKAWA watacheza karata vizuri?
 
16. Kuanguka kwa thamani ya shilingi imesababisha hasara kubwa kwa mabenki, wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji
17 kupeana wao kwa wao nafasi za uongozi (uswahiba)
18. watoto na jamaa wa vigogo kulindwa-Kumesababisha matabaka katika nchi
19. kushamiri kwa madawa ya kulevya pamoja na uvunaji wa maliasiri zilizopo bila ya woga kwa maslahi yao
20. Usimamizi mbaya wa mapato ya taifa

intetesting!
 
Kuteuliwa na kushika nyadhifa viongozi wasiokubalika katika jamii
 
19.Kuanzisha mahospital ya maraisi na vigogo wa nchi hii pia itawatoa madarakani so waweka ubaguzi.
 
16. Ukabila uliopitiliza
17.Udini
18.Kupeana madaraka kwa kujuana na sio weledi/ujuzi wa kazi
19. Kukiuka maelekezo ya mwasisi wa Taifa hili
 
emmanuel haya ni mawazo yako ila kwa taarifa yako na kwa kuwa husomi magazeti ningekushauri uanze kusoma uangalie jinsi wabunge wa ccm wanavyopokelewa majimboni na kuchangiwa fedha za kugombea tena. ninyi mnazunguka na chopa mnakusanya watu wanaoshangaa chopa mnajiaminisha kuwa mtaing'oa ccm madarakani. inawabidi mjipange haswa kwani ajenda hizo ulizotaja wananchi wameelewa ukweli kwamba serikali sio fisadi bali mtu mmojammoja ndio fisadi, rasimu wameisoma na kuielewa na wataipigia kura ya ndiyo, mahakama ya kadhi waislamu wameeleweshwa namna mchakato ulivyo na wameelewa. mimi nadhani tusiandikie mate wakati wino ni oktoba 2015. tusubiri tutajua mbivu na mbichi

Back
Top Bottom