Mambo yatakayofanywa na CHADEMA siku 100 za kwanza

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
16,992
10,497
MAMBO YA SIKU 100 ZA KWANZA Ndani ya siku 100

tangu siku ya kuapishwa kwa Rais na Wabunge, watakaokuwa wamechaguliwa, Serikali ya Chadema itafanya taratibu zinazohusika ili kuhakikisha yafuatayo yanatendeka:

i) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano, ambayo pamoja na mambo mengine itaanzisha Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza Taifa letu.

ii) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi juu ya Utoaji wa Elimu Bure kuanzia elimu ya awali hadi Sekondari.

iii) Serikali itapunguza kiwango cha marejesho ya mikopo ya elimu ya juu hadi kufikia asilimia tatu (3) ya mshahara wa mnufaika na kutanua wigo wa muda wa marejesho hadi kufikia miaka 25 tangu mnufaika apate ajira. Aidha, Serikali itafuta riba na tozo zote zitokanazo na adhabu ya kuchelewesha marejesho ya mkopo wa elimu ya juu.

iv) Serikali itashirikiana na sekta binafsi kuweka utaratibu wa kutoa huduma za afya ya msingi kwa wananchi bila malipo.

v) Serikali itarejesha mchakato wa Katiba Mpya kuanzia ilipoishia Rasimu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba

vi) Serikali ya Chadema itatekeleza matakwa ya Katiba kuhusu Tume ya Pamoja ya Fedha ya Muungano ili kila nchi Mshirika wa Muungano ipate mgao wake wa fedha kwa mujibu wa Katiba na sheria.

vii) Serikali ya Chadema itarejesha uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kuruhusu vyombo hivyo kurusha moja kwa moja vikao vya Kamati za Bunge, Mikutano ya Bunge na Mwenendo wa Uendeshaji wa Mashauri Mahakamani.

viii) Serikali ya Chadema itapeleka miswada ya Sheria Bungeni kwa madhumuni ya kuzifuta Sheria zote kandamizi na zinazokiuka misingi ya haki za binadamu.

ix) Kuanzisha utaratibu wa mazungumzo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar kwa lengo la kufikia muafaka juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, uvuvi wa bahari kuu na usajili wa meli.

x) Serikali ya Chadema itaandaa mazingira rafiki na wezeshi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali kama vile ugonjwa, kukosa ada, mimba n.k. kurejea kwenye mfumo rasmi wa elimu na kumalizia masomo yao.

xi) Serikali ya Chadema itapeleka bajeti ya Nyongeza Bungeni katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya kuongeza Mishahara ya watumishi wote wa umma, kulipa malimbikizo; sambamba na kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa na kulipa mishahara inayoendana na madaraja yao.

xii) Serikali ya Chadema itaanzisha bima maalum ya afya kwa watumishi wote wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wawapo kazini na baada ya kustaafu vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zima moto na Uokoaji.

xiii) Serikali ya Chadema itarejesha maduka yasiyotozwa kodi (Duty free shops) katika vyombo vya ulinzi na usalama vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji.

xiv) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii ili kurekebisha kikokotoo cha UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU 10 Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wastaafu ili kiendane na mahitaji ya wastaafu. Aidha, Serikali ya Chadema itaruhusu wafanyakazi na watumishi waliochangia katika mifuko ya jamii kuchukua mafao yao wakati wowote (fao la kujitoa).

xv) Serikali ya CHADEMA itaweka utaratibu na kuwatafutia masoko wakulima, wavuvi na wafugaji ya kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi bila kizuizi.

xvi) Kurejesha utaratibu wa awali wa ukusanyaji wa kodi, ushuru na tozo mbalimbali kwa mamlaka ya serikali za MITAA.
 
Mmmmh
20200905_213022.jpg
 
Wananchi wa Bukoba naomba wawawekee sehemu maalumu Peponi . Leo wamemwambia Meko mubashara kabisa “Hatukutaki” wala hatutakupigia kura! TBC wamekata kipande Meko anabishana na wananchi mapovu yanammwagika tuu! Kwani ni lazima wananchi wakukubali mzee?
 
Duuuhhh, TBC kama kawaida yao kumbe wamefanya censorship
 
Sijaona kufutwa kwa chama chakavu na kurudisha serikalini mali zote walizopora na kujimilikisha. This should be priority #1.
 
Ofisi ya chadema imewashinda kujenga kwa zaidi ya miaka 30 sasa.
acha uzwazwa wa lumumba we mama wakati wa TANU ulikuwepo? unaikumbuka ilivoanza?
sasahivi CHADEMA inahangaika kuwahudumia wananchi kuwatafutia maisha bora kuwatoa kwenye umafia wa FISIEM wewe ni mmojawao unaehitaji kusadiwa kujitambua
 
Wananchi wa Bukoba naomba wawawekee sehemu maalumu Peponi . Leo wamemwambia Meko mubashara kabisa “Hatukutaki” wala hatutakupigia kura! TBC wamekata kipande Meko anabishana na wananchi mapovu yanammwagika tuu! Kwani ni lazima wananchi wakukubali mzee?
safi sana nona wananchi wameshajitambua tusubiri OCT 28 tum'bwage MTU
 
HATUTAWAPA KURA KWA SABABU MKIINGIA MTAANZA KUSEMA SERIKALI IMEVURUGWA SUBIRINI TUITENGENEZE KWANZA KUMBE MMESHINDWA KUKUSANYA PESA YA KUENDESHEA NCHI HAKUNA NCHI YA KUCHEZEA KUJARIBISHA KUONGOZA NENDENI MKAGOMBEE URAIS WA TFF
 
usyempenda leo umemuita akuombee KURA kwi kwi kwi kwi kwi.. wananchi wamezomeaaa
 
Comrade Tunaomba ilani yenu ya uchaguzi mtuwekee hapa tujiridhishe kama hayo unayosema yapo. Isije kuwa unatulisha matango pori baada ya kuvimbiwa kiporo.
 
Wananchi wa Bukoba naomba wawawekee sehemu maalumu Peponi . Leo wamemwambia Meko mubashara kabisa “Hatukutaki” wala hatutakupigia kura! TBC wamekata kipande Meko anabishana na wananchi mapovu yanammwagika tuu! Kwani ni lazima wananchi wakukubali mzee?
Unafikiri uongo utakusaidia comrade?
 
MAMBO YA SIKU 100 ZA KWANZA Ndani ya siku 100

tangu siku ya kuapishwa kwa Rais na Wabunge, watakaokuwa wamechaguliwa, Serikali ya Chadema itafanya taratibu zinazohusika ili kuhakikisha yafuatayo yanatendeka: i)
Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano, ambayo pamoja na mambo mengine itaanzisha Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza Taifa letu.

ii) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi juu ya Utoaji wa Elimu Bure kuanzia elimu ya awali hadi Sekondari.

iii) Serikali itapunguza kiwango cha marejesho ya mikopo ya elimu ya juu hadi kufikia asilimia tatu (3) ya mshahara wa mnufaika na kutanua wigo wa muda wa marejesho hadi kufikia miaka 25 tangu mnufaika apate ajira. Aidha, Serikali itafuta riba na tozo zote zitokanazo na adhabu ya kuchelewesha marejesho ya mkopo wa elimu ya juu.

iv) Serikali itashirikiana na sekta binafsi kuweka utaratibu wa kutoa huduma za afya ya msingi kwa wananchi bila malipo.

v) Serikali itarejesha mchakato wa Katiba Mpya kuanzia ilipoishia Rasimu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba

vi) Serikali ya Chadema itatekeleza matakwa ya Katiba kuhusu Tume ya Pamoja ya Fedha ya Muungano ili kila nchi Mshirika wa Muungano ipate mgao wake wa fedha kwa mujibu wa Katiba na sheria.

vii) Serikali ya Chadema itarejesha uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kuruhusu vyombo hivyo kurusha moja kwa moja vikao vya Kamati za Bunge, Mikutano ya Bunge na Mwenendo wa Uendeshaji wa Mashauri Mahakamani.

viii) Serikali ya Chadema itapeleka miswada ya Sheria Bungeni kwa madhumuni ya kuzifuta Sheria zote kandamizi na zinazokiuka misingi ya haki za binadamu.

ix) Kuanzisha utaratibu wa mazungumzo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar kwa lengo la kufikia muafaka juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, uvuvi wa bahari kuu na usajili wa meli.

x) Serikali ya Chadema itaandaa mazingira rafiki na wezeshi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali kama vile ugonjwa, kukosa ada, mimba n.k. kurejea kwenye mfumo rasmi wa elimu na kumalizia masomo yao.

xi) Serikali ya Chadema itapeleka bajeti ya Nyongeza Bungeni katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya kuongeza Mishahara ya watumishi wote wa umma, kulipa malimbikizo; sambamba na kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa na kulipa mishahara inayoendana na madaraja yao.

xii) Serikali ya Chadema itaanzisha bima maalum ya afya kwa watumishi wote wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wawapo kazini na baada ya kustaafu vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zima moto na Uokoaji.

xiii) Serikali ya Chadema itarejesha maduka yasiyotozwa kodi (Duty free shops) katika vyombo vya ulinzi na usalama vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji.

xiv) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii ili kurekebisha kikokotoo cha UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU 10 Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wastaafu ili kiendane na mahitaji ya wastaafu. Aidha, Serikali ya Chadema itaruhusu wafanyakazi na watumishi waliochangia katika mifuko ya jamii kuchukua mafao yao wakati wowote (fao la kujitoa).

xv) Serikali ya Chadema itaweka utaratibu na kuwatafutia masoko wakulima, wavuvi na wafugaji ya kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi bila kizuizi. xvi) Kurejesha utaratibu wa awali wa ukusanyaji wa kodi, ushuru na tozo mbalimbali kwa mamlaka ya serikali za MITAA.
Yote hayo yana mwelekeo wa kuongeza matumizi ya serikali pasipo kuboresha makusanyo ya serikali.

Mfano utakaporuhusu wafanyakazi kuchukua pesa zao NSSF wakati wowote ilihali pesa ziko kwenye miradi ya serikali, hiyo serikali ya CHADEMA itapata wapi pesa za kurejesha NSSF mara moja?

Napenda kusikia mkizungumzia PPP kwa upana zaidi badala ya kulenga afya na elimu pekee.
 
Ofisi ya chadema imewashinda kujenga kwa zaidi ya miaka 30 sasa.
Hii kitu inaleta utata kama ahadi wanazotoa watatimiza, licha ya kupata ruzuku ya zaidi ya bilioni tatu kila mwaka lakini wameshindwa hata kujenga ofisi ya makao makuu ya chama.
 
Back
Top Bottom