Mambo yanayofungua tabasamu la penzi kwa mwanamke

Mambo yanayofungua tabasamu la penzi kwa mwanamke

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,193
^^
Tukiweka kando wale wanawake ambao wakiona pesa ya mwanaume ndio hutoa tabasamu la upendo,,wapo wachache sana (wanahesabika) ambao wakifanyiwa mambo yafuatayo na wanaume wawapendao basi nyuso zao hukunjuka na kung'aa kama mwezi angavu.
....
KUKUBALIKA
Wanawake wanapenda sana kukubalika namna walivyo.Awapo nyumbani,njiani,au kazini hujisikia vema pale mwanaume anapotoa kauli za dhati juu ya namna anavyomkubali mpenzi wake. Mpe pongezi kwa bidii yake,mwambie namna unavyofarijika kumpata yeye! Hakika utapata tabasamu lake.
Mwanamke anapokosa kukubalika si ajabu akatumia nguvu mf hudai wanaumwa vichwa,kizunguzungu,au malalamiko madogo madogo ambayo tiba yake ni hitaji la kukubalika.
....
KUONYESHWA HUBA
Mara nyingi wanaume wamekuwa wakionyesha pendo kwa wanawake pale tu wanapotaka ngono au tendo la ndoa.Laiti kama tungejua wanapenda sana kuthaminiwa kihisia tangu mwanzo na bila wakati maalum basi wanaume wangevuna faraja nyingi toka kwa wanawake.
....
ZAWADI ZA KUSHITUKIZA
Zawadi ndogo ndogo ambazo hakuzitarajia ndio sumaku inayoteka hisia ya mwanamke.Ifanye ya kawaida ambayo haina gharama sana na uwe umejua anapenda nini na hataki nini.. Ni jambo dogo lakini litakufungulia mengi.
....
JINSI GANI NI MZURI,,ANAHITAJI KUSIKIA TOKA KWAKO
Huko njiani,kazini amesikia wanaume wengi wakimsifia kuwa yeye ni mzuri (hata kama kwa kweli hana jipya) Lakini lipo hitaji la kusikia kwa kinywa chako kuwa yeye ni mzuri. Wanaume wengi hubeba mashairi mengi kichwani mwanzo wa uhusiano,akishampata mwanamke,neno "u mzuri kipenzi" husikika kwa bahati mbaya.Hata kama amezeeka,anahitaji kuguswa uzuri ni haki
yake,mpe.
....
AWE WA KWANZA KATIKA BAJETI
Inawezekana una mipango kadhaa juu ya mahusiano yenu.Anafurahi kukuta ktk bajeti ya mwezi huu umeanza na jina lake.Hata kama ulichopanga ni kidogo sana,,ajabu ni kuwa wanaume hutaja orodha hata ya kurasa mbili,lakini mpango juu ya mwanamke wake haupo..Hili linawaumiza.. Uwe makini si kila jambo anatakiwa alijue vinginevyo una uhakika na akili yake.. Hapo tabasamu lake utalipata likichanua taratibu.
....
Ruth Peale mwanasaikolojia na mjuzi wa masuala ya wanawake aliwahi kusema "Women need to be loved in small signs,Men need admiration in great signs"
^^
 
Ukitaka kufeli mtihani kaa na uanze kumsom mwanamke by mfalme selemani
 
Wenyewe wanachokihitaji hua hawatambui whom one do you expect to know?
 
Ila kweli me mwenyewe vitu vidogo sana hunifanya nitabasamu..
 
umesema vyema Himidini . Je wewe hayo unafanya?
 
Last edited by a moderator:
Akirudi nyumbani aje na chochote ata pipi...,visms kama nimekumiss,..ikifika kwenye bajeti tuchanganye mapato na kupanga nini kifanyike..napokua naongea nae nione ananisikiliza .etc etc....
 
umesema vyema Himidini . Je wewe hayo unafanya?

^^
Nina moyo wa kuyafanya ila nakatishwa tamaa na heart breakers!! Sijui ka mkosi au ni ka baraka
^^
 
Last edited by a moderator:
Nimepapenda hapo kwenye vijizawadi vya kushtukiza. Mpenzi wangu aliniletea kijizawadi cha Dola tatu tu ila kila nukiiona namfeel
 
^^
Nina moyo wa kuyafanya ila nakatishwa tamaa na heart breakers!! Sijui ka mkosi au ni ka baraka
^^

Chill man ipo siku utakutana nae mwenyekustahili kufanyiwa haya! Kwa kipindi hiki unachosema unakutana na heartbreaks amini ni kipindi cha kukukomaza.
 
^^
Ha ha Mashaxizo
sikupenda kugusia hilo maana nilishawahi kuijadili kwenye threads zangu.
Btw: Karibu tena na pole kwa ban
^^

Hahahahahaaaa!
Usijali kaka niko poa!
Nilikua nawachungulia fresh tu!
...
Hope u a cool too!
 
Last edited by a moderator:
Chill man ipo siku utakutana nae mwenyekustahili kufanyiwa haya! Kwa kipindi hiki unachosema unakutana na heartbreaks amini ni kipindi cha kukukomaza.

^^
Kweli kabisa.. Ndio maana sina papara wala hasira,
Mola akipenda atanipa, Mengine mengi keshanipa ndio maana nipo hapa.
Cc: Blue G christine ibrahim Chujio annito
^^
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom