The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,911
- 2,891
Inashangaza kuona serikali haina sera madhubuti inayosimamia elimu hivyo kila waziri anayekuja wizarani analeta mawazo yake binafsi na hivyo kuyumbisha misingi ya elimu yetu.
Nitoe mifano michache
1. Mungai - Alifuta michezo mashuleni
2. Dr. Kawambwa - Alifuta division
3. Prof. Ndalichako - Ameondoa GPA
Hiyo ni mifano michache tu lakini inadhihirisha jinsi waziri anavyokuwa na nguvu kubwa ya kufanya chochote.
Wote tunajua jinsi vitabu vinavyoandikwa hovyo hovyo na kulazimisha kufundishia.
Nina mashaka kuwa ipo siku tutapata waziri mvuta bangi akaamua kuingiza mawazo yake ya kibangi bangi wizarani.
Serikali lazima ije na muongozo ambao kila waziri anayekuja anapaswa kuusimamia na si kila waziri kuja na kuonesha ufundi wake kwenye elimu yetu.