Mambo yaliyo kushangaza Mwaka 2018

kanonb

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
369
500
Hello wana jukwaa mpo wazima ni Imani yangu "Japo tunaendelea kulima mpunga kwenye lami" huu mwezi wa tatu tangu tumeuaga mwaka 2018 lakini nieona ni vyema tukumbushane mambo yaliyotushangaza mwaka uliopita mimi lililonishangaza sana ni hili
Uchaguzi wa urais Kenya kurudiwa, mahakama ya juu yaamuru
Mahakama ya juu nchini Kenya, siku ya Ijimaa ilitoa uamuzi uliokuwa umesubiriwa na Wakenya wengi na kusema kuwa ni sharti uchaguzi wa rais urudiwe katika kipindi cha siku sitini.

Wakiongozwa na jaji mkuu David Maraga, majaji hao walikuwa wakisikiliza kesi iliyowasilishwa mahakamani na aliyekuwa mgombea wa muungano wa upinzani wa NASA, Raila Odinga
Ijumaa, majaji wanne walikubaliana kwamba uchaguzi huo ulikuwa na dosari. Hata hivyo, majaji Njoki Ndung'u na Jackton Ojwang hawakukubaliana na wenzao. Jaji Mmoja Mohammed Ibrahim, hakushiriki kwenye uamuzi huo kwani alikuwa mgonjwa.
Akizungumza nje ya mahakama kuu mjini Nairobi muda mfupi baada ya uamuzi huo, aliyekuwa mgombea urais wa upinzani Raila Odinga alisema kuwa Ijumaa ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa Kenya na kwa Afrika.
"Kwa mara ya kwanza, Mahakama imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais naiImetoa mfano mwema," alisema Odinga.
"Tulisema tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa. Siku ya tarehe 8 Agosti tulivuka mto Jordan," aliongeza.
Aidha, mwanasiasa huyo alisema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki.
"Maafisa wengine wa tume hiyo wanatakiwa kuwa jela,' alsema Odinga.
Kwa mujibu wa sheria za Kenya, sasa wagombea wote wanane walioshiriki kwenye uchaguzi wa kwanza, watashiriki katika raundi ya pili ya uchaguzi.
Punde tu baada ya uamuzi kusomwa, Wakenya katika baadhi ya maeneo waliandamana barabarani kusherehekea.
Habari zaidi zitafuata hivi punde....
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,325
2,000
Kifo cha Ruge na Kibonde kupishana kwa siku kumi (10) pekee.
R.i.P Ruge...
R.i.P Kibonde...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom