Msomi hewa
JF-Expert Member
- Nov 17, 2016
- 768
- 1,066
...........Habari wanajamvi, Kama title inavyojieleza hapo juu leo ningependa kushare na nyie mambo Manne(4) Makuu Yaletayo Heshima Mbele Ya Jamii.
Nadhani Kila mtu anahitaji ama Anapenda kuheshimiwa katika Jamii.
Leo napenda ni share na nyinyi Juu na Sifa nne Ambazo Mtu akiwanazo(Angalau mbili) ataheshimiwa.
1-Elimu
Iko wazi Kua jamii nyingi za kiafrika zimekua zikiheshimu watu wenye elimu ama uelewa juu ya jambo flani.
Kwa hiyo kama unataka jamii ikuheshimu na ithamini mchango wako basi Angalau uwe na sifa hii.
2-Umri mkubwa(Mzee)
Ni ukweli usiopingika kua Jamii nyingi Za kiafrika zimekua zikiheshimu watu wenye Umri mkubwa(Wazee).
Jamii nyingi zinaamini kua mtu mwenye umri mrefu(mzee) huwa na busara,Hivyo basi Umri mrefu huongeza heshima ya mtu.
3-Dini
Watu wengi huheshimu na kuthamini mawazo ya watu wenye hofu ya mungu,Hivyo basi Dini Imekua chachu inayochangia kwa kiasi kikubwa kuleta heshima ya mtu katika jamii.
4-Pesa
Siku hizi ukiwa na pesa Unaweza kuamkiwa hata na mtu aliyekuzidi umri,Hii ni kumaanisha kwamba pesa pia huchangia katika kuleta heshima ya mtu.
Hayo ni Mambo Makuu Manne Ambayo huleta heshima ya Mtu.
Akhsanteni.