Mambo ya Muungano kwenye Rasimu ya Katiba

Wakuu serikali ya Tanganyika is INEVITABLE AT THE CURRENT SITUATION kama mna hang over ya mawazo ya kale ndio mnang'ang'ania serikali mbili. Tanganyika ni nchi iliyokabidhiwa uhuru wake tarehe 9 Disemba 1961 mbona mnaipoteza historia yetu
 
Zanzibar si kuwa inataka kujiunga na hako kajumuiya kenu ka EAC ambako hakina cha maana kwa wananchi wa nchi jumuia, Zanzibar usiifananishe na timu zenu za Simba na Yanga (nadhani umenielewa), inahitaji mambo yaeleweke yapi Tanganyika inasimamia binafsi na si kwa mgongo wa muungano.

Mpendwa Jacobus; hayo yanayotegemewa kuwa ya muungano yametajwa yako saba tu na hayo ndiyo yaleyale yatakayokuwemo kwenye shirikisho la EA sasa shirikisho la serikali ya muungano wa Tanzania ya nini ?
 
Sioni faida za muungano na kanchi kadogo ka Zanzibar yenye watu 1.3 milioni na ukubwa wa wilaya ya Kinondoni lakini wenye ushawishi mkubwa katika siasa za nchi yenye zaidi ya watu 43 milioni.Fikiria Zanzibar ina wabunge 60 katika bunge la JMT ambao wanalipwa na hazina ya Dar sawa sawa na mbunge wa Kigoma anayewakilisha zaidi ya watu 1 milioni.Hii ni nini kama si unyonyaji.

Nakuunga mkono mkuu.
 
Mpendwa Jacobus; hayo yanayotegemewa kuwa ya muungano yametajwa yako saba tu na hayo ndiyo yaleyale yatakayokuwemo kwenye shirikisho la EA sasa shirikisho la serikali ya muungano wa Tanzania ya nini ?
Hata mimi mkuu nasangaa kwani 'Hati ya Muungano" tunaambiwa yalikuwa 11 sasa kuyapunguza na kuwa 7 tuu maana yake ni nini? Naweza kukubaliana nawe kuwa hakuna haja ya Tanzania kama hati ya muungano haikuheshimiwa!
 
Serikali za washirika hazitafanya jambo lolote la kimataifa bila ya kushirikisha jamhuri za muungano, ikiwemo kukopa nje, kuwa na mashirikiano na nchi za nje.
Katika kupitia rasimu ya katiba mpya nimeona kuwa katika mambo yanayoelezwa kuwa ni ya Muungano ni "Mambo ya Nje". Wakati huo huo, katika ibara ya 62 (2) ya rasimu hiyo kunaelezwa hivi (nanukuu)

"(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, kila Mshirika waMuungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano auushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mamboyaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Mshirika wa​
Muungano". (mwisho wa kunukuu)

Sasa kwa mujibu wa kifungu hicho bila shaka mshirika (yani Zanzibar au Tanzania Bara kama ilivyotumika humo) anaweza kuanzisha mahusiano na jumuiya au taasisi ya kimataifa bila pingamizi mfano kujiunga na jumuiya kama COMESA au hata kuzipa bendera meli za nchi za nje (ship flagging) hasa Zanzibar ambayo nadhani bendera wanayo. Je hapa hakuna kukinzana? Yani upande unaambiwa mambo ya nje ni ya Muungano, wakati huo huo unaruhusiwa kuwa na mahusiano/ushirikiano na taasisi za kimataifa! Wajuzi mkinielewesha nitashukuru.


 
Majimbo mawili tu Ndio suluhisho yaani ZNZ atawale Gavana au waziri Mkuu kisha Tanganyika atawale Gavana au Waziri mkuu na Raisi awe Mmoja tu aishi Dodoma hakika tutakuwa na muungano Digtal na kuondokana na muungano Anologia wa serikari tatu ambao marehemu Baba wa Taifa aliukataa .ama kweli kikulacho ki ngoni mwako ! Eti jaji Waryoba kausahau USIA wa Nyerere kupinga serikari tatu
we minyoo kweli bba wa taifa ndo nani pimbi wee
 
Wazanzibar wanahitaji usawa kwenye serikali ya muungano kuwa haiwezekani nchi huru (Zanzibar) ikatoa wabunge 20 na Tanganyika wabunge 50 kwenye bunge la muungano lakini sina hakika watakapopewa nafasi sawa kwa sawa watakubali pia kuchangia gharama za kuendesha serikali ya muungano kwa usawa??!!, huu ni mwisho wa muungano kwani watasema gharamieni mnaotaka muungano (I mean Tanganyika) na sielewi kama kutakuwa na chombo gani cha kungalia compliance ya kuchangia gharama za muungano na pia kama upande mmoja uki-default hatua gani itachukuliwa. Serikali tatu zinatupeleka kuuvunja muungano, na haitachukua muda mrefu sana kwani hilo wenzetu ndilo wanalolitaka. Katika mfumo wa serikali 2 ilikuwa ngumu kidogo lakini kwa mfumo huo mpya dalili za kuuvunja kabisa zitaonekana mapema. Serikali moja hawawezi kukubali na hizi mbili pia hawawezi kukukbali pia na ndiyo maana Mzee Warioba alisema kwamba walipata shida sana kulijadili ili kwani nafikiri wanzibar walisimama pamoja kutetea kile walichotumwa na zaidi ya hayo Maalim Sefu akachombeza wayatakayo zaidi kabla rasimu haijatangazwa and I think alishaambiwa rasimu ina kitu gani juu ya muungano.
nyinyi wanyika tunawaburuza tuuuu nyinyi.. mpaka kiama henu mkione..akili hamna hata kidogo.. sisi zanzibar tupo kidogoo tunaburuza ma milioni.. na tutaendelea. tulianza kuchange aina ya muungano mkawa mnajichekea now mko tele kwenye hili gurudumu... basi jitayarisheni...tunalotaka sisi ndo hilo hilo...
 
Back
Top Bottom