Mambo ya Muungano kwenye Rasimu ya Katiba

  • Thread starter Mapango ya Amboni
  • Start date

M

Mapango ya Amboni

Senior Member
Joined
Apr 12, 2013
Messages
106
Likes
103
Points
60
M

Mapango ya Amboni

Senior Member
Joined Apr 12, 2013
106 103 60
Katika kupitia rasimu ya katiba mpya nimeona kuwa katika mambo yanayoelezwa kuwa ni ya Muungano ni "Mambo ya Nje". Wakati huo huo, katika ibara ya 62 (2) ya rasimu hiyo kunaelezwa hivi (nanukuu)

"(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, kila Mshirika waMuungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano auushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mamboyaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Mshirika wa​
Muungano". (mwisho wa kunukuu)

Sasa kwa mujibu wa kifungu hicho bila shaka mshirika (yani Zanzibar au Tanzania Bara kama ilivyotumika humo) anaweza kuanzisha mahusiano na jumuiya au taasisi ya kimataifa bila pingamizi mfano kujiunga na jumuiya kama COMESA au hata kuzipa bendera meli za nchi za nje (ship flagging) hasa Zanzibar ambayo nadhani bendera wanayo. Je hapa hakuna kukinzana? Yani upande unaambiwa mambo ya nje ni ya Muungano, wakati huo huo unaruhusiwa kuwa na mahusiano/ushirikiano na taasisi za kimataifa! Wajuzi mkinielewesha nitashukuru.

Kobello

Kobello

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2011
Messages
6,553
Likes
1,606
Points
280
Kobello

Kobello

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2011
6,553 1,606 280
Niliuliza swali hilo jana kwenye post ya Mwanakijiji, nikatukanwa.
 
OSOKONI

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Messages
10,985
Likes
4,046
Points
280
OSOKONI

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2011
10,985 4,046 280
Hii ilikuwa ina maana ya kuiruhusu Zanzibar kujiunga na OIC ili kunyamazisha kilio chao, cha muda mrefu!!Hii rasimu ni nzuri ila kuna sehemu kama inawabembeleza wazanzibar mfano wakati huku bara Mkoa mzima utachukuliwa kama jimbo la uchaguzi Zanzibar wao wilaya ndio Jimbo la uchaguzi, kuna uwiano gani hapo!! Mkoa wa Dar es salaam una idadi ya watu zaidi ya mara tatu ya wakazi wote wa Zanzibar lakini kwa mujibu wa rasimu Dar itakuwa na wabunge wawili tu(ME na KE) lakini Zanzibar ambayo wakazi wake wala hawafikii hata theluthi moja ya wakazi wa Dar watakuwa na wabunge ishirini! huku ni kuwabembeleza wazanzibar au vip??
 
OSOKONI

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Messages
10,985
Likes
4,046
Points
280
OSOKONI

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2011
10,985 4,046 280
Niliuliza swali hilo jana kwenye post ya Mwanakijiji, nikatukanwa.
Matusi ni elimu na ujuzi wa mjinga usijalli kamanda songa mbele endelea kutoa michango motomoto!!
 
Kobello

Kobello

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2011
Messages
6,553
Likes
1,606
Points
280
Kobello

Kobello

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2011
6,553 1,606 280
Katika kupitia rasimu ya katiba mpya nimeona kuwa katika mambo yanayoelezwa kuwa ni ya Muungano ni "Mambo ya Nje". Wakati huo huo, katika ibara ya 62 (2) ya rasimu hiyo kunaelezwa hivi (nanukuu)

"(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, kila Mshirika waMuungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano auushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mamboyaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Mshirika wa​
Muungano". (mwisho wa kunukuu)

Sasa kwa mujibu wa kifungu hicho bila shaka mshirika (yani Zanzibar au Tanzania Bara kama ilivyotumika humo) anaweza kuanzisha mahusiano na jumuiya au taasisi ya kimataifa bila pingamizi mfano kujiunga na jumuiya kama COMESA au hata kuzipa bendera meli za nchi za nje (ship flagging) hasa Zanzibar ambayo nadhani bendera wanayo. Je hapa hakuna kukinzana? Yani upande unaambiwa mambo ya nje ni ya Muungano, wakati huo huo unaruhusiwa kuwa na mahusiano/ushirikiano na taasisi za kimataifa! Wajuzi mkinielewesha nitashukuru.

Na kwa kuongezea tu,tukijenga bomba la gesi kwenda Mombasa, itabidi tupate idhini ya zanzibar. Ila Zanzibar will not be a state, so will Tanganyika.
 
Mr Denis

Mr Denis

Member
Joined
Jul 2, 2012
Messages
84
Likes
0
Points
0
Mr Denis

Mr Denis

Member
Joined Jul 2, 2012
84 0 0
japo sijapata mudA wa kutosha kuichambua rasimu hatua kwa hatua, kwa utangulizi wa jaji warioba suala linaloshika kasi ni habari ya muungano wa serikali tatu.
kiuhalisia muungano sijui ni kuupuuza pasipokujua ama kwa kujua tumekua tukiubeza ama kuujadili kwa ushabiki na mambo kama hayo

wengi wanapendelea muundo wa serikali 3 kama ilivopendekezwa na jaji warioba na tume yake,

mambo muhimu ya kujadili kwa makini sana,

1) kwa huu wa nchi mbili, gharama za matumizi ya kawaida hasa ktk kulipa posho mishahara na garama za viongozi na masuala mengine ambayo kwa nchi zingine kama rwanda na kenya ama uganda waohawana ila kwa tanzania gharama izo tunazo na hali ya uchumi wengi wetu tunaijua Hali inayopelekea kiasi kikubwa cha bajeti kuishia kwenye matumizi ya kawaida (over 70%) zaidi ya shughuli za maendeleo
2)naamini huu huu muungano wapo wanasiasa wanaonufaika kimaslahi mfano mzuri ni CCM (sina nia mbaya tafadhali) hivyo hivyo endapo muungano ukawa wa nchi tatu hali ya manufaa binafsi itashika kasi ya ajabu sana na hata KUPELEKEA MIGONGANO YA KIMASLAHI HIVYO VITA NA HATIMAE KUVUNJA MUUNGANO KTK HALI YA CHUKI.

3)nionavyo mimi tuwe na msmamo wa muungano wa uundwaji wa nchi moja tu. Tanzania ila ktk hili LAZIMA serikali ya majimbo iwepo ili kuepusha maginalization of zanzibar,
na kama haitawezekana basi muungano USIWEPO tutengane kwa AMANI
 
J

Jimy P

Senior Member
Joined
Dec 7, 2011
Messages
125
Likes
0
Points
0
J

Jimy P

Senior Member
Joined Dec 7, 2011
125 0 0
Muungano wa serikali tatu haukubaliki... tunawapa watu ulaji kwa kodi za watanganyikana kuongeza misafara...posho na mishahara minono
 
M

muchetz

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2010
Messages
866
Likes
522
Points
180
M

muchetz

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2010
866 522 180
japo sijapata mudA wa kutosha kuichambua rasimu hatua kwa hatua, kwa utangulizi wa jaji warioba suala linaloshika kasi ni habari ya muungano wa serikali tatu.
kiuhalisia muungano sijui ni kuupuuza pasipokujua ama kwa kujua tumekua tukiubeza ama kuujadili kwa ushabiki na mambo kama hayo

wengi wanapendelea muundo wa serikali 3 kama ilivopendekezwa na jaji warioba na tume yake,

mambo muhimu ya kujadili kwa makini sana,

1) kwa huu wa nchi mbili, gharama za matumizi ya kawaida hasa ktk kulipa posho mishahara na garama za viongozi na masuala mengine ambayo kwa nchi zingine kama rwanda na kenya ama uganda waohawana ila kwa tanzania gharama izo tunazo na hali ya uchumi wengi wetu tunaijua Hali inayopelekea kiasi kikubwa cha bajeti kuishia kwenye matumizi ya kawaida (over 70%) zaidi ya shughuli za maendeleo
2)naamini huu huu muungano wapo wanasiasa wanaonufaika kimaslahi mfano mzuri ni CCM (sina nia mbaya tafadhali) hivyo hivyo endapo muungano ukawa wa nchi tatu hali ya manufaa binafsi itashika kasi ya ajabu sana na hata KUPELEKEA MIGONGANO YA KIMASLAHI HIVYO VITA NA HATIMAE KUVUNJA MUUNGANO KTK HALI YA CHUKI.

3)nionavyo mimi tuwe na msmamo wa muungano wa uundwaji wa nchi moja tu. Tanzania ila ktk hili LAZIMA serikali ya majimbo iwepo ili kuepusha maginalization of zanzibar,
na kama haitawezekana basi muungano USIWEPO tutengane kwa AMANI
Mwanzo nimeogopa "comment" zako. Kwenye 3) yako huo ndo ukweli. Muungano uwe na serikali moja au tuuvenje!!!!!
NB: Angalizo mwalimu alishaonyesha wasiwasi wake kuhusu aina ya muungano tunayotaka.... wa aina huu ni wa kuuvunja ... sasa basi tuamue kuuvunja ama kuukuza!!
 
nahavache

nahavache

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2009
Messages
869
Likes
5
Points
35
nahavache

nahavache

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2009
869 5 35
Basi tuwe na serekali nne, Ya Tanganyika, Ya Unguja, Ya Pemba na ya Muungano
 
Fasouls

Fasouls

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2011
Messages
920
Likes
62
Points
45
Fasouls

Fasouls

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2011
920 62 45
Muungano bora uende we are now tired talking about you everytime
 
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2013
Messages
11,062
Likes
6,759
Points
280
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined May 25, 2013
11,062 6,759 280
japo sijapata mudA wa kutosha kuichambua rasimu hatua kwa hatua, kwa utangulizi wa jaji warioba suala linaloshika kasi ni habari ya muungano wa serikali tatu.
kiuhalisia muungano sijui ni kuupuuza pasipokujua ama kwa kujua tumekua tukiubeza ama kuujadili kwa ushabiki na mambo kama hayo

wengi wanapendelea muundo wa serikali 3 kama ilivopendekezwa na jaji warioba na tume yake,

mambo muhimu ya kujadili kwa makini sana,

1) kwa huu wa nchi mbili, gharama za matumizi ya kawaida hasa ktk kulipa posho mishahara na garama za viongozi na masuala mengine ambayo kwa nchi zingine kama rwanda na kenya ama uganda waohawana ila kwa tanzania gharama izo tunazo na hali ya uchumi wengi wetu tunaijua Hali inayopelekea kiasi kikubwa cha bajeti kuishia kwenye matumizi ya kawaida (over 70%) zaidi ya shughuli za maendeleo
2)naamini huu huu muungano wapo wanasiasa wanaonufaika kimaslahi mfano mzuri ni CCM (sina nia mbaya tafadhali) hivyo hivyo endapo muungano ukawa wa nchi tatu hali ya manufaa binafsi itashika kasi ya ajabu sana na hata KUPELEKEA MIGONGANO YA KIMASLAHI HIVYO VITA NA HATIMAE KUVUNJA MUUNGANO KTK HALI YA CHUKI.

3)nionavyo mimi tuwe na msmamo wa muungano wa uundwaji wa nchi moja tu. Tanzania ila ktk hili LAZIMA serikali ya majimbo iwepo ili kuepusha maginalization of zanzibar,
na kama haitawezekana basi muungano USIWEPO tutengane kwa AMANI
Muungano bila serikari tatu inawezekana taifa kubwa dhidi ya taifa dogo Hapo mkanganyiko ktk maamuzi makuu hususana uwiano wa mapato ni lazima kitimu timu
 
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2013
Messages
11,062
Likes
6,759
Points
280
minyoo

minyoo

JF-Expert Member
Joined May 25, 2013
11,062 6,759 280
Majimbo mawili tu Ndio suluhisho yaani ZNZ atawale Gavana au waziri Mkuu kisha Tanganyika atawale Gavana au Waziri mkuu na Raisi awe Mmoja tu aishi Dodoma hakika tutakuwa na muungano Digtal na kuondokana na muungano Anologia wa serikari tatu ambao marehemu Baba wa Taifa aliukataa .ama kweli kikulacho ki ngoni mwako ! Eti jaji Waryoba kausahau USIA wa Nyerere kupinga serikari tatu
 
T

timbilimu

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2010
Messages
4,808
Likes
175
Points
160
T

timbilimu

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2010
4,808 175 160
Muungano wa serikali tatu haukubaliki... tunawapa watu ulaji kwa kodi za watanganyikana kuongeza misafara...posho na mishahara minono
Unawapa watu ulaji gani? Natarajia tuwe na serikali ndogo sana kwa mambo yanayohusu Muungano. Na ninatarajia ktk katiba mpya ya Tanganyika kuondolewa tawala za mikoa,badala yake tuwe na majimbo kama sita ama saba. Tutapunguza sana gharama za kuhudumia wanasiasa 30 wanaopewa vyeo vya hisani wkt hawaelewi hata wajibu wa madaraka yao.
 
M

mshunami

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2013
Messages
3,811
Likes
462
Points
180
M

mshunami

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2013
3,811 462 180
Unawapa watu ulaji gani? Natarajia tuwe na serikali ndogo sana kwa mambo yanayohusu Muungano. Na ninatarajia ktk katiba mpya ya Tanganyika kuondolewa tawala za mikoa,badala yake tuwe na majimbo kama sita ama saba. Tutapunguza sana gharama za kuhudumia wanasiasa 30 wanaopewa vyeo vya hisani wkt hawaelewi hata wajibu wa madaraka yao.
Kwa mfano unaonaje kama inavyopendekezwa majimbo ya uchaguzi yawe 25 ziwe ndo wilaya zenye kutengeneza majimbo lets say matano?
 
N

Nonda

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Messages
13,329
Likes
2,049
Points
280
N

Nonda

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2010
13,329 2,049 280
Ngatele

Ngatele

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2011
Messages
498
Likes
67
Points
45
Ngatele

Ngatele

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2011
498 67 45
Wazanzibar wanahitaji usawa kwenye serikali ya muungano kuwa haiwezekani nchi huru (Zanzibar) ikatoa wabunge 20 na Tanganyika wabunge 50 kwenye bunge la muungano lakini sina hakika watakapopewa nafasi sawa kwa sawa watakubali pia kuchangia gharama za kuendesha serikali ya muungano kwa usawa??!!, huu ni mwisho wa muungano kwani watasema gharamieni mnaotaka muungano (I mean Tanganyika) na sielewi kama kutakuwa na chombo gani cha kungalia compliance ya kuchangia gharama za muungano na pia kama upande mmoja uki-default hatua gani itachukuliwa. Serikali tatu zinatupeleka kuuvunja muungano, na haitachukua muda mrefu sana kwani hilo wenzetu ndilo wanalolitaka. Katika mfumo wa serikali 2 ilikuwa ngumu kidogo lakini kwa mfumo huo mpya dalili za kuuvunja kabisa zitaonekana mapema. Serikali moja hawawezi kukubali na hizi mbili pia hawawezi kukukbali pia na ndiyo maana Mzee Warioba alisema kwamba walipata shida sana kulijadili ili kwani nafikiri wanzibar walisimama pamoja kutetea kile walichotumwa na zaidi ya hayo Maalim Sefu akachombeza wayatakayo zaidi kabla rasimu haijatangazwa and I think alishaambiwa rasimu ina kitu gani juu ya muungano.
 
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Likes
104
Points
145
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 104 145
Tuige South Africa ambao wametenganisha makao makuu ya mihimili yao... hii inasaidia kusambaza uchumi wa nchi!

Judiciary [Mahakama ya Juu na ya Rufaa ya Muungano]----> Makao Makuu Unguja- Zanzibar

Executive [Serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania] ----> Makao makuu Magogoni/Lithuli Street- Dar es Salaam

Paliament [ Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania] ----- Makao Makuu - Tanga->Kwa nini Tanga ni muhimu kuendeleza miji yetu kuondokana na dhana ya kulindika kila kitu sehemu mojo. Tanga pia ni karibu na Pemba na Unguja. Kwa nini sio Dodoma... Kwa sababu Dodoma ni katikati ya Tanganyia na sio katikati ya Tanzania.

Mungu Ibariki Tanzania,

Wewe unasema je?

Kwa waTanzania bara... nawasaidia kupendekeza.

Makao makuu ya Serikali na Bunge --->Dodoma.
Makao makuu ya Mahakama yenu --->Arusha

Lazima nikiri sina uhakika ni vyema kuwa kwenye katiba au iko kwenye enabling laws.
 
Dr.Godbless

Dr.Godbless

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2010
Messages
811
Likes
611
Points
180
Dr.Godbless

Dr.Godbless

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2010
811 611 180
[h=5]........"Sisi tuliona Muungano utakuwepo kama kutakuwa na dhamira ya Muungano na ndiyo maana tulisisitiza tusiingilie haki za uraia kwa sababu watu wana nguvu ya kuweza kuufanya Muungano ukawa pamoja kuliko hata vyombo vya Serikali.

Watu wenyewe wakianza kubaguana hata kama Muungano una muundo mzuri kiasi gani hautadumu.

Hata kama kutakuwa na Serikali mbili au tatu, kama hakuna dhamira Muungano utavunjika tu, muundo siyo tatizo, kikubwa kinachotakiwa kutazamwa ni dhamira ya viongozi wa nchi mbili".

JOSEPH SINDE WARIOBA[/h]
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,027
Likes
5,488
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,027 5,488 280
Demokrasia ya kujadili namna ya kuipata Katiba ya Muungano imefanyika kwa uangalifu mkubwa na tuna imani kubwa kuwa makundi yote muhimu yalifikiwa na Tume hiyo iliyoongozwa na Jaji mstaatu, Joseph Sinde Warioba.

Baada ya mchakato mzima wa kukusanya maoni ya wananchi sasa, Rasimu ya Katiba ya Muungano imekamilika, kinachofuata ni kuyasoma kwa makini yaliyomo ndani ya Rasimu hiyo ndipo tuanze kuyafanyia uchambuzi.

Wananchi wengi wameonyesha kufurahishwa na yaliyomo ndani ya Rasimu hiyo, na endapo masuala yote yatapitishwa bila ya kuwa na mabadiliko, basi nchi hii tayari itakuwa na Katiba

mpya kama inavyosomeka ndani ya Rasimu, na ndiyo maana tunatoa angalizo kuwa kinachotakiwa ni kuisoma kwa umakini na kwa uelewa wa juu. La kama yapo marekebisho yawekwe wazi yachambuliwe kupata muafaka kwani lengo ni kuyaridhia yaliyomo kwa pamoja.

Katika majadiliano yanayoendelea sasa, baadhi ya makundi yameeleza kutoshirikishwa katika Rasimu hii, mfano ni wakati mlemavu mmoja alipotaka kujua kama ni kipengere gani cha Rasimu hiyo kilichofafanua umuhimu wa elimu kwa walemavu.

Kimsingi Rasimu imetamka wazi kuwa elimu itakuwa kipaumbele kwa Watanzania wote, bila ubaguzi, mlemavu aliyehoji alijisahau kuwa yeye ni mmoja kati ya Watanzania waliojumuishwa katika kipengele hicho.

Kipindi hiki ambacho Rasimu inasubiri ipitie hatua mbalimbali kabla ya kuipitishwa ifikapo Aprili 26, 2014, ni wajibu wa Wananchi kuyatambua mapungufu kama yapo ndani ya Rasimu hii ili yapatiwe ufumbuzi.

Utaratibu wa kuipata Katiba ya Muungano umeelezwa kuwa baada ya kupata Rasimu ya Kwanza ambayo tayari imetolewa, wananchi wanalazimika wayasome yaliyomo kabla ya mjadala wa Mabaraza ya Katiba kufanyika. Maoni ya Mabaraza yanatarajiwa kuanza kazi zake mwezi Julai na kukamilisha Septemba.

Kazi kubwa itakuwa kuichambua Rasimu ya Kwanza kabla ya kufanyiwa marekebisho na kupelekwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba. Bunge hilo nalo litakaa Novemba mwaka huu na kuichambua Rasimu ya Pili ya Katiba na kuyatolea maoni kwa ajili ya kuiandaa rasimu ya mwisho.

Utaratibu huo utaendelea tena katika awamu ya Rasimu ya Mwisho kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni. Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa za Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Tume ya kura za maoni kwa ajili ya kupitisha Katiba Mpya inatarajiwa kukutana mwezi Machi mwakani, baada ya hapo kitakachokuwa kikisubiriwa ni uzinduzi wa Katiba Mpya unaotarajiwa kufanyika Aprili 26, 2014.

Ni muhimu sote tukaelewa kuwa bado haya ni mapendekezo ambayo yanahitaji uchambuzi wa kina. Hakuna sababu ya jazba, badala yake tutulie tuyajadili tuainishe mapungufu ambayo tunaamini tume ya Warioba itayafanyia kazi kupata suluhu.

Yapo maeneo mbalimbali katika rasimu hii ya kwanza ambayo tayari yamepigiwa kelele kuwa yanahitaji marekebisho na hasa masuala ya muundo wa serikali kama ulivyotolewa kwamba ziundwe serikali tatu, iwapo serikali ya Muungano, ya Zanzibar na serikali ya Tanzania Bara au Tanganyika.

Mapendekezo yote bado yanaweza kubadilika kutokana na vikao vilivyoainishwa kuyapitia kabla ya kuipitisha kuwa Katiba kamili hapo Aprili mwakani, na ndiyo maana vyama vya siasa pia vinatakiwa kujadili mustakabali wa taifa hili kulingana na mapendekezo ya Rasimu ya Kwanza.

Kutokana na ukweli kuwa Katiba ni sheria, na ikipitishwa na ikaanza kutumika, hapatakuwapo na fursa nyingine ya kufanya mabadiliko makubwa, na ndio maana tunasema kila mwananchi kwa nafasi yake ana nafasi ya mwisho ya kuisoma kwa makini na kutoa maoni kabla haijapitishwa rasmi.

Kumekuwapo na tuhuma nyingi sana nchini za viongozi kutafuta nafasi za uongozi wa juu kwa kutanguliza rushwa.

Kama matajiri wakijiunga na kuwa na umoja wa kumfanyia kampeni wamtakaye ili awe Rais, watamwaga fedha zitakazowachanganya wananchi na hatimaye nchi inaweza kupata Rais wa ajabu.

Siyo ajabu ikapata Rais muuza unga kama ilivyowahi kutokea huko Mexico, jambo ambalo ni hatari tupu, labda iwe mgombea binafsi katika ubunge ambako athari zake si kubwa kama kwa Urais. Sasa tumeona mwelekeo wa kuipata Katiba ya Muungano, tuipe nguvu zaidi kwa

kusoma na kuzingatia kuwa hiyo itakuwa sheria mama itakayolinda haki za wananchi wote kwa miaka mingi ijayo.

Ni imani yetu kuwa kila mwananchi anafahamu wajibu wake, kama kuna eneo halifahamiki wapo wengi wanaoweza kutoa ufafanuzi, tusipoteze nafasi wakati ndiyo huu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

T

tpmazembe

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Messages
2,472
Likes
46
Points
145
T

tpmazembe

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2012
2,472 46 145
Naomba siku ya kupiga kura ya maoni ya katiba kwenye kipengele cha muungano kuwe na majibu matatu ya kuchagua. moja likiwa ni a)unakubali muungano wa serikali tatu b)unaukataa muungano uliopendekezwa wa serikali tatu c) hautaki muungano uwepo kabisa.

Napendekeza iwe hivyo kutokana na kulalamika kwingwi hasa kwa hawa wenzetu wa znz. Pia kwa kuwa hakuna mazingira ya muungano wa serikali moja na serikali mbili ni unyonyaji, serikali tatu ni haki lakini gharama bora HAKA KAMUUNGANO KAFE TU, tutashirikiana EAC maana hayo mambo ya sarafu,jeshi yanaenda kuwa ya jumuiya na ndio malengo ya mbele hakuna haja ya KULALAMIKIANA.

waweke hivyo ili mimi nichague C niwe nimenawa mikono kwa kizazi cha mbele, hakuna sustainability kwenye muungano na hawa waznz
 
Forum statistics

Threads 1,273,861
Members 490,528
Posts 30,493,794