Jaman mbavu sina mimi, yaani watu wameshakata tamaa ya maisha hivi unakubali uponyaji kwa mizizi huku mkiwa mmesubiliana hadi watu mamia! si angeamuru wapone kwa Neno tu sasa hadi wanakufa!
Upupu mwingine bana!:hand::hand::hand:
hawa ndio mababu wanaotibu ukimwi mwisho wa siku wanakufa nao
hivi musa alipofika kwenye yale maji yasiyonyweka aliambiwa afanye nini na mungu?
Ngoja tukueleze ulelewe, mti ndio uhai na ukombozi wa mwanadamu, zambi ya kwanza ilianzia kwenye mti na ukombozi wa kweli unapatikana kwenye mti,
musa aliwaokoa watu wa islaeli kutoka misri kwa neema za mungu huku akitumia fimbo (mti)
nuhu aliwaokoa watu wake kwa kutengeneza safina iliyotengenezwa kwa miti,
lutu alipokosa uzao watoto wake walimlewesha kutokana na divai, iliyotengenezwa kwa dhabibu (mti)
na ili ukombozi wa kweli upatikane mwana wa adamu ilimbidi aangikwe mtini (msalabani) afe kifo cha laana, kama ukombozi ulikuwa ni lazima yesu afe kwa nini hakufa kifo kingine chochote mpaka afe mtini?
Huyo babu angekuwa anakwambia njoo na kuku mweusi umwage damu hapo ndipo tungekuwa na wasiwasi, lakini kunywa maji yaliyochanganyika na miti yupo sahihi sana
kwa kumalizia soma kitabu cha timoteo, "na kwa matatizo yako ya tumbo, usinywe maji pekeyake unywe na mvinyo kidogo"
Jina Jipya la Mungu wangu ni Yesu; aliyejulikana zamani kwa majina mengi kama Yehova Yire (Mungu mponyaji), Yehove Nisi (Mungu ndiye bendera ya ushindi wangu) Jehova Shalom (Mungu wa Amani) Alfa na Omega (Yeye ni mwanzo na pia Mwisho), alionekana kwa Musa kama Yuko ambaye Yuko na kwa Wana wa Israel kama Mungu wa baba yao Ibrahimu Isac na Yakobo....So ukiniuliza kuhusu huyo Babu alioteshwa na nani na kama ni mganga au mchungaji; I cant say much he knows better than I do for he is the owner of the dream/vision....Sijawahi kumwona kumsikia yeye kama individual anadai nini hivyo nadhani I have no right to rule out who he is and kwa jina gani anafanya hayo anayofanya...
Kwakukusaidia mimi sina dini na wala siamini katika yeyote I am a christian by faith na ukristo tafsiri yake ni Outward working of Divinity in Humanbeings...The power that worketh is that of Holly spirit of God/Jesus hayo mengine ya dini niwaachie wanazozimiliki am out!
Huwezi kumuwekea mipaka Mwenyezi Mungu katika utendaji wake kwani njia zake si njia zetu.
Habari Za wandugu wa JF,
Nimeamini kuwa kilichosemwa na BIBLIA hakitabadilika hata kama ni kwanini.
1.WATU HAWA WANAMACHO LAKINI HAWAONI, WANAMASIKIO LAKINI HAWASIKII.
2. WENGI WATAKUJA KWA JINA LA MUNGU.
Tusibabaishwe na mganga wa Loliondo ukweli hakuna Mungu wa namna hiyo yeye angetumia tu jina la Mganga wa kienyeji sio Mungu unajua ni kwanini?
a. Dawa ya Mungu hainaga masharti, hata ukipewa sio masharti kama ya Loliondo eti hakuna mtu mwingine kukupa dawa hiyo ukanywa zaidi ya yeye peke yake swali: Watumishi wa Mungu Loliondo ni yeye peke yake? kama wengine wapo kwanini wasisaidiane? si kumpa tu mtu maji anakunywa??
b. Kwanini mti huo kama umefunuliwa na Mungu ukitumiwa na wengine usiponye?? Maana yake Mungu ameanza lini kutufundisha ubinafsi na uchoyo?
Nikomee hapa nitarudi! View attachment 24640
Wana Jf nivumilieni tu nimuulize huyu aliyepost kuhusu mganga wa loliondo kuweka masharti ya kutoa dawa mwenyewe, swali moja
NAAMANI JEMADARI WA JESHI LA WASHAMI ALIPOAMBIWA NA MTUMISHI WA MUNGU ELISHA KUWA AKAOGE MARA SABA MTO YORDAN HAPAKUWA NA MITO KWAO? HATA ELISHA ALIKUWA MGANGA WA KIENYEJI KUMPANGIA MASHARTI? (lazima aoge mara 7, mto Yordan?)
hivi nikichukua hiki kikombe cha babu wa loliondo halafu nikamwagia kwenye nyumba yangu si umeme unaweza usikatike tena niishiwe na tatizo la mgao wa umeme?