Mambo ya kuzingatia ukitaka usifanikiwe

Mambo ya kuzingatia ukitaka usifanikiwe

Cofta

Senior Member
Joined
Aug 6, 2017
Posts
158
Reaction score
632
Habari za muda huu ndugu zangu za JF.
Leo nina machache ya kuwashirikisha kwakifupi kabisa. Mambo haya yatakusaidia kuweza kupishana na mafanikio endapo utakuwa umedhamiria kuyasikia mafanikio kwa watu wengine tu.

1. LAWAMA
Endapo unadhamiria mafanikio yapite mbali na wewe basi jitahidi angalau kila siku isiishe kwako bila lawama.
Elekeza lawama zako kwenye fulsa ambazo watu wanajitahidi kukuonesha kwakuona kwamba fulsa wenyewe niza kawaida mno ili kufanikiwa.
Pia usisahau kumlaumu muumba wako kukuumba maskini na wazazi wako kwa kutokukujengea msingi bora wa maisha.

2. WIVU
kuwa mtu wa wivu kwa watu ambao wanamafanikio zaidi yako na jitahidi sana kuutumia wivu wako katika kutafuta namna zakuwafanya waliofanikiwa zaidi yako kuweza kushuka chini sehemu ulipo wewe. Ukiweza hilo basi ni dhahiri lengo lako la kutofanikiwa litakufikia bila kukawia.

3. MIPANGO MIPYA.
Naaam ili lengo lako la kutofanikiwa liweze kutimia jitahidi kila mara kuweka mipango mipya ambayo haina utekelezaji.
Pia ikitokea umepata fulsa(project fulani) basi jitahidi kabla haujaanza kuitekeleza angalau uiwekee mipango mingine mipya kadhaa na kila siku ambayo ulipaswa uanze utekelezaji basi jitahidi kuitumia siku hiyo kuweka mipango mipya.
Bila kusahau, jitahidi kuweka mbinu za utekelezaji wa mipango yako kama bumunda yaani usiigawanye project yako ktk hatua mbalimbali za utekelezaji, ukiweza hivyo basi ujue unakaribia kutimiza lengo.

4. ANZA KUWEKA AKIBA KESHO
Naaam ili iwe rahisi kwako kutofanikiwa basi usihangaike kuweka akiba katika siku inayoitwa leo, wewe jiwekee utaratibu wakuweka akiba kuanzia siku inayoitwa kesho. Hamna haja yakuihangaikia kesho hivyo wewe izingatie zaidi leo na akiba utaanza kuweka kesho ikifika.

5. ONGEA ZAIDI KULIKO KUSIKILIZA.
Naam hili nalo ni muhimu sanaaa.
Ili iwe rahisi kutofanikiwa jitahidi sanaa kuwa na mdomo mrefu zaidi, ongea kadri uwezavyo na usitoe nafasi ya kumsikiliza mtu yoyote wala ushauri wa mtu yoyoyte awe ni mwenye utaalamu wa fani hiyo au asiwe mtaalamu. Mafanikio yako ya kutofanikiwa ni yako wewe binafsi hivyo hayawahusu watu wengine hivyo jitahidi mno kutowasikiliza wengine.

6. KUWA MWEPESI WAKUACHA JAMBO LOLOTE(QUITTING)
Yaani hapa ndugu yangu wewe ukiona jambo au kazi yoyote inakuumiza kichwa hata usijisumbua achana nayo tu.
Usijipe stress kwa mambo yanayoumiza kichwa kabisa maana maisha sio vita.
Hakika hakuhakikishia mafanikio utayasikia kwenye bomba.

7. POTEZA MUDA UWEZAVYO.
Siku moja ina masaa 24 na hata siku ya leo ikipotea kesho bado itakuwa na masaa 24 hivyo haina haja yakujisumbua maana kesho nayo ni siku.
Leo itumie kupumzika tuu na kesho nayo ikija utumie kuzurula tuu kesho kutwa ikija sio vibaya kama utaitumia kupiga story.
Usiwe na wasiwasi kabisa na mida wako maana mwaka una miezi 12 na kila mwezi unasiku takribani 31/30/28 na kila mwezi una wiki nne na kila wiki ina siku saba na kila siku ina 24 na kila saa lina dakika 60 na kila dakika ina sekunde 60, huo ni muda mwingi sanaaa aiseeeee hivyo sio vibaya kupoteza muda kidogo na hakika utafikia lengo lako la kutokuyafikia mafanikio.

Mniwie radhi kama kutakuwa na makosa ya kiuandishi.

Mtu yoyote anaweza akaongezea lolote ili tusaidie yoyote mwenye malengo ya kutofanikiwa ili atimize malengo yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya maisha ukijua kulaumu unaishi vema sana, kila tatizo lako una watu wa kunyooshea kidole na sio wewe... yaani unakuwa unafarijika sana.

Siku zote maishani, kwa kila kitu hakikisha unatafuta mtu wa kumlaumu.
 
Bidii katika kutoa walama haziwezi kumuangusha mtu, hakika ajitahidi kulaumu na atafanikiwa kutofanikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli mtamu!

Formular ya life sijui ni lini itapatikana tuondokane na mahard feelings ...
 
Back
Top Bottom