Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Kuna usemi wa Kiafrika usemao kuwa: Inachukua kijiji kizima kumlea mtoto. Usemi huu unamaanisha kuwa malezi ya watoto yanahamasishwa na familia zao na watu wengine wanaowazunguka. Familia na jamii nzima ina jukumu kubwa la kuwalea watoto kwa mapenzi makubwa.
Leo tuangazie mambo sita muhimu ya kuzingatia katika makuzi ya mtoto ambayo ni: Upendo wa Dhati, Mfumo Maalum wa Maisha na Malezi, Kumuelewa Mtoto, Kuwa Mfano Mzuri wa Kuigwa, Changamoto za Utoto, Kushirikiswa katika familia.
Upendo wa dhati katika malezi ya mtoto ni muhimu sana. Upendo wa dhati humaanisha kumpenda pasipo na masharti, kumpenda wakati wote anapokosea na anapofanya vizuri, kumuonya na kumrekebisha kwa upendo ilihali akijua hata kama amekosea anarekebishwa kwa upendo. Mapenzi kwa mtoto yanajenga uaminifu, misingi mizuri ya uadilifu na heshima. Mapenzi haya yalenge kumjenga mtoto kihisia na kisaikologia na hii itafanya kazi ya malezi kuwa rahisi. Siku zote jaribu kuwa karibu na mtoto wako; cheza naye inapobidi kucheza naye. Ukaribu wako na mtoto kutamsaidia mtoto wako kuwa huru kwako na kuwasiliana na wewe muda wowote anapohitaji msaada wako.
Mfumo maalum wa maisha na malezi. Hii inagusa zaidi katika mazingira ambayo mtoto anaweza kukua, kujitambua na kujengewa mfumo mzuri wa tabia na maadili yanayokubalika na jamii nzima. Mara nyingi inakuwa ngumu kumlea mtoto katika tabia fulani kwa sababu anapokua na kuwasiliana na wengine hujifunza kutoka kwao. Mtoto huweza kujifunza mambo mabaya au mazuri lakini ni jukumu lako kama mzazi/mlezi kuhakikisha kuwa mtoto wako anakuwa na mfumo maalum wa maisha na malezi; sio leo umesema hiki, kesho unasema kinyume na ulichoelekeza jana.
Kumuelewa mtoto. Siku zote kama mlezi jaribu kumuelewa mtoto. Elewa hisia zake, mawazo yake, juhudi zake yeye kama mtoto, msifu akifanya vizuri, mpongeze hata kwa kumkumbatia na kumshika mkono. Watoto wanaopongezwa na kusikilizwa kwa makini hujenga kujiamini na kuthubutu kufanya mambo na kufanya vizuri zaidi katika maisha ya kawaida na masomo yao. Watoto wanapojua kuwa familia zao zinawakubali na kuwaelewa huwajengea uwezo mkubwa wa kufanya vizuri zaidi .
Kuwa mfano mzuri wa kuigwa. Watoto hujifunza kwa kuangalia watu wazima wanaowazunguka na huweza kujifunza mabaya au mazuri. Sasa basi; wewe kama mzazi au mlezi ni jukumu lako kuwa mfano mzuri wa kuigwa. Siku zote jua kuwa wewe ni mwalimu wa kwanza kwa mtoto wako. Atajifunza kwako namna ya kuwasiliana na watu, namna ya kukabiliana na changamoto na kuzitatua. Umewahi kujiuliza mawasiliano yako na wengine yakoje? Je wewe ni mtu wa kugombana na watu hovyo hovyo hata kwa makosa madogo? Unatatuaje matatizo ya kila siku ya kifamilia? Yote haya mtoto huangalia na kujifunza kwako. Tabia kama za ulevi, matusi na ugomvi huwafanya watoto wajue kuwa huo ndio mfumo wa maisha. Hivyo kama mzazi jifunze kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa mtoto wako na hata kwa wanaokuzunguka .
Changamoto za utoto. Kila umri wa makuzi ya mtoto una changamoto zake kwa mtoto mwenyewe na hata kwa mzazi. Kila hatua ya umri mtoto apitiayo ina chngamoto zake ikiwemo kujifunza maswala mbalimbali katika jamii, kuimarisha uwezo wao wa kutatua matatizo/changamoto zinazowakabili na changamoto hizi zisipokabiliwa zinaweza kuharibu mfumo mzima wa makuzi ya mtoto na hata wa familia nzima. Kama mzazi, ni vizuri ukampa mtoto nafasi ya kuweza kukabiliana na changamoto.
Kushirikishwa katika familia ni kuhakikisha mtoto anashiriki kikamilifu katika maamuzi ya kifamilia na hasa mambo yanayogusa maslahi yake binafsi, hata majukumu madogomadogo ya kila siku. Hii humpa mtoto hisia za kuwa ana familia inayomkubali na kumtegemea, humpa mtoto nafasi ya kujiamini na kushiriki katika mambo mbalimbali ya jamii na kifamilia, humfanya achukue majukumu katika familia na pia kuwajengea uwezo wa kujitegemea.
Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia kurasa zetu wa Facebook, Instagram na JamiiForums: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org.