SoC02 Mambo ya kuzingatia kabla hujaanza Ujasiriamali

Stories of Change - 2022 Competition

Tape measure

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,972
3,511
Watu wengi sana wanatamani kufanya ujasiriamali kwa malengo tofauti tofauti ikiwemo kuwa na uhuru wa muda na kuongeza kipato, hata baadhi ya watu ambao wapo kwenye ajira hupendelea kukusanya mtaji ama kwenda kukopa kwenye taasisi za fedha kwa malengo ya ujasiriamali. Changamoto ni kwamba zaidi ya 65% ya biashara mpya zinazoanzishwa hufa ndani ya mwaka 1-2 na asilimia 30 pekee ndio zina uwezekanano wa kuendelea.

Nitaelezea mambo 4 ya muhimu kwa mjasiriamali anayopaswa kuyatambua kabla ya kuanza biashara


1. Aina ya biashara
Unapaswa kujua ni aina gani ya biashara ama huduma unayotaka kuuza, pia unapaswa kutambua tatizo ambalo unataka kulitatua katika eneo lako hapa nikisema tatizo namaanisha uhitaji wa bidhaa yako kwa eneo husika. Fahamu changamoto zilizopo kwenye biashara unayopanga kuifanya hii ni pamoja na kuwatambua washindani wako waliopo kwenye hiyo biashara, hili litakuwezesha kujua ni kitu gani uongeze au kupunguza kusudi uweze kushindana nao kwenye biashara.

Taarifa sahihi kama biashara unayopanga kuifanya tayari una uzoefu nayo hii itakuwa ni hatua kubwa sana kwani uzoefu katika biashara nayo ni sehemu ya mtaji!! Unapaswa kujua fika ni nini hasa wateja wako wanahitaji, aina na tabia za wateja wako labda ni wanafunzi, watu wa kipato cha kati ama chini, ni wasomi, Watoto, wazee, wanawake ama wanaume.

Kushindwa kutambua aina ya wateja wako, unaweza kuboresha sana eneo lako la biashara lakini wateja wakakukimbia wengine wakidhania labda bei yako itakuwa ya juu zaidi! Pia unaweza kushusha bei sana kusudi upate faida kidogo na wateja wakakukimbia wakidhania labda pengine unauza bidhaa feki!! Hapa kuna kitu cha kujifunza Namna na vigezo unavyotumia kupanga bei ya bidhaa au huduma yako.
Kama katika eneo lako umezungukwa na wanajamii wa kipato cha chini sana na ukapanga kuwauzia nguo za viwango vya juu ni dhahiri utakosa wanunuaji, unaweza ukawa unapika chakula kizuri sana lakini ukakiuza bei ya chini kuna aina ya watu watashindwa kuja katika eneo lako sababu tu unauza bei ndogo.

Ujuzi je una ujuzi sahihi wa kutosha kwenye hiyo biashara? Kama huna ujuzi ni vyema kutenga muda wa kujifunza au kuajiri watu sahihi wenye ujuzi ambao unahitajika katika biashara yako. Unapaswa kuwa na taarifa sahihi kwenye swala zima la kodi na sheria za nchi.
Hii inajumuisha kutambua mamlaka ambazo zinahusika na kufanya usajili wa biashara yako mfano uvuvi, asali, mazao ya misitu kama vile mbao, duka la dawa, pembejeo za kilimo, viwanda vya kusindika, maduka, hoteli.


2. Uwezo wako wa kuongoza watu wengine
Kuwa na shauku ya ujasiriamali hakutoshi wewe kufanikiwa mjasiriamali anapaswa pia kuwa na tabia za kiuongozi, kwanza kiongozi ni mtu mwenye maono, mtu wa kuleta na kukubali mabadiliko, mtu wa kujiamini, kuheshimu wenzake, kuunganisha watu, mbunifu, ana watu wanaomwamini na kumfuata (followers).

Ukiwa na Sifa ya uongozi itakusaidia sana pale utakapokuwa unafanya makubaliano ya biashara, itakuwezesha wewe kuweza kutoa maelekezo na miongozo ya biashara kwa wafanyakazi wako, na kukusaidia kuweza kutatua kwa ufanisi migogoro itakayojitokeza kwenye maeneo yako ya ujasiriamali .


3. Andaa Bajeti na Namna ya kufanya matangazo
Hiki ni kipengele muhimu kwenye hatua za ujasiriamali, hapa unapaswa kujua utahitaji mtaji kiasi gani kwenye kufanya biashara yako, kama mtaji ulionao hautoshi unatakiwa kuona namna ya kutafuta partnership na watu wengine ambao wataunganisha nguvu kusudi kuweza kufikia lengo.

Kwenye kupata wadau ama mwekezaji mwenza ni vyema ukafikiri kwa kina namna gani mtaweza kugawana majukumu Pamoja na faida itakayopatikana kwa kufuata sheria na miongozo mtakayojiwekea, hapa itawalazimu kuandika hati ya makubaliano baina yako na partners wapya (memorandum of understanding). Pia unaweza kufikiria kuanza taratibu au kuomba mkopo.

Unatakiwa uwe na kumbukumbu zote za mapato na matumizi katika biashara yako na kurahisisha hayo kwa sasa kuna software nyingi kwa ajili ya kufanya hivyo unaweza kutumia Quick Book, Plan Guru, SMETracker
Marketing ni tofauti na advertisement- kufanya marketing ni ile hali ya kuwashawishi watu na kuwapa sababu ya kwa nini wanunue bidhaa ama huduma yako na kuachana na bidhaa zingine ambazo tayari zipo sokoni.

Ni muhimu kuweza kutumia fursa za kidijitali zilizopo katika kuwafikia wateja wako, unaweza kuweka matangazo kwenye mitandao ya kijamii kama Jamii Forum, Facebook ads, Instagram ads, You Tube ads, Tovvuti hii itakusaidia kuongeza wigo wa kupata wateja wapya.

4. Usimamizi wa mauzo ya bidhaa na utoaji wa Huduma bora kwa wateja
Unatakiwa kujua ni kwa namna gani utaweza kutoa huduma bora na zenye kuridhisha wateja wako, kupunguza malalamiko ya wateja na kutengeneza mfumo ambao utakuwezesha kuweza kupata maoni kutoka kwa wateja wako.

Maoni ya wateja yatakusaidia sana kuweza kuona ni wapi unakosea uboreshe zaidi na wapi unapatia, tambua kumpata mteja mpya ni kazi ngumu mno hivyo wateja ambao tayari utakuwa nao jitahidi kuwalinda.

Taarifa mbaya za huduma au bidhaa husambaa haraka kuliko taarifa nzuri hivyo tambua kuwa mteja mmoja ambaye ulimpatia bidhaa au huduma mbovu anaweza kusambaza taarifa mbaya kwa watu 8-16 na hao watu wakawaambia watu wengine 32-64 na kukuharibia kabisa brand yako ndani ya kipindi kifupi.

Hakikisha kuwa unautaratibu wa kurekebisha au kubadilisha bidhaa mbovu ambayo umemuuzia mteja kwani kujenga BRAND sio jambo rahisi lakini ukishaijenga tayari unakuwa umeteka moyo wa wateja wako na wanakuwa wananunua bidhaa yako kwa imani kubwa bila ya kuangalia bei.

HITIMISHO: Biashara nyingi zinakufa kwa sababu ya waanzilishi kutozingatia baadhi ya mambo ambayo kwao wanadhani ni madogo sana lakini yana mchango Mkubwa katika kuhakikisha biashara yako inasimama. Mfano suala la kuandika mpango kazi/business plan watu huzani ni uchuro au ni kwa watu wanaojitia wasomi Tu! Na kuishia kufanya biashara kwa mazoea hili ni tatizo kubwa sana kwa wajasiriamali walio wengi wasomi na wasio wasomi.

Kama wwe ni mjasiriamali na hujui ndani ya mwaka au kipindi cha miaka 5 biashara yake anategemea iwe imefikia hatua gani ni tatizo tayari ambalo linaweza kukufanya kushindwa ? Na ukishakuwa na hizo takwimu mpango kazi wako ndio unakuwa unakueleza ili kufikia hiyo hatua utahitajika kufanya nini?

Labda kuongeza wafanyakazi au uzalishaji ama utakuwa tayari na uzoefu hivyo utaweza kupunguza gharama nyingi tofauti na mwanzoni mfano gharama za matangazo, au kukodisha magari na tayari utakuwa na vyombo vyako vya usafiri.

MABADILIKO YANAANZA NA MIMI NA WEWE TUJENGE UTAMADUNI WA KUANDAA MPANGO KAZI KABLA YA KUANZA KUFANYA BIASHARA YEYOTE
 
Kama uliandaa mpango kazi kabla ya kuanza biashara tuambie ulipitia changamoto gani kufanikisha, faida zake na mbinu zingine zilizoweza kukuvusha
 
Wanasiasa wanatuhubiria tujiajiri bila ya kutupatia mbinu na nyenzo za kukiajiri. Kujiajiri ni mchakato sio suala la usiku mmoja
 
Wanasiasa wanatuhubiria tujiajiri bila ya kutupatia mbinu na nyenzo za kukiajiri. Kujiajiri ni mchakato sio suala la usiku mmoja
Hii ni Kweli lakini pia ukijiajiri wanasiasa wakikuona unaujuzi mkubwa kwenye soko la ajira wanakuja kukufungia.

Sasa watupe muongozo mzuri utakao zingatia haki za binadamu kwamba vijana waruhusiwe kihalali kujiajiri kwenye nyanja zote ambazo ni muhimu naomba nikazie kwenye "sayansi na teknolojia".
 
Nime kupigia kura !!!

Umetoa ushauri mziru "Chanya" japo nimeona ndani ya chapisho kuna vipengere kama vile. Ujasiriamali, ajira nikupongeze Sana lakini naomba nipaweke sawa sehemu moja.

Mimi naomba nizungumzie kwenye kipengere cha "ajira".

wengi wa wajasiriamali wanafanya kazi zisizo za ndoto zao, hili ndiyo tatizo watu wengi wanakosa ujuzi kwenye kazi za ujasiriamali wanakosa ubunifu na mbinu ambazo zitafanya biashara zao ziwape faida.


Unakuta mtu anayo degree ya sheria alafu anakuja kufanya kazi ya kujiajiri kibisa ya kuuza vipodozi sijui "vipodozi vya hasiri" hivyo inaweza kupelekea biashara kufa, kwanza mtu anakuwa hana furaha kwenye hiyo kazi ambayo siyo ya ndoto yake anashindwa kuiboresha kwa sababu za kisaikolojia.
 
Ujasiriamali siyo lelemama.

Unapokuwa mjasiriamali customer care iwepo pia kutunza bidhaa zako unazouza, kuhakikisha haikosekani muda wote iwepo.

Asante kwa andiko
 
Tatizo kile unachokiamini kama hauna fungu mkononi, unaambiwa fanyahiki kutokana na aliyekushika mkono.
Mwanzo inakuwa vigumu kutoboa unaweza kukata tamaa ya kwanini hukusikilizwa lakini kama ni mbunifu na mwepesi wa kujifunza kutokana na makosa unaweza kupiga hatua baada ya uzoefu wa mapito magumu hadi kufikia ndoto ya kile kilichopo ndani yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom