Mambo ya kuzingatia kabla haujaanza kufuga kuku kibiashara

Jun 25, 2021
11
47
MAMBO YA KUZINGATIA KABLA HAUJAANZA KUFUGA KUKU KIBIASHARA

1. AVAILABILITY (uwepo wako)

Kabla ya kuanza ufugaji wa kuku kibiashara hakikisha unapata nafasi ya kushiriki kwa karbu katika mradi wako.kama nafasi yako itakua ndogo sana basi jitahidi mwenza wako asimame kama wewe. Au upate kijana mwaminifu sana japo kushiriki mwenyewe moja kwa moja ni bora zaidi .Na ukiona nafasi yako ndogo basi ujitahidi kuhuzuria kwa mda unaoupata usimwamini mtu kwenye ili swala la usimamizi 100%

Watu wengi wameshindwa kuendelea na ufugaji wa kuku kwa makosa ya kutokuwepo karbu na mifugo yake hii inatokana na kumwamini kijana ambaye unampa kazi ya kusimamia mifugo yako anakua makini sana ukiwepo Ila unapotoka na kumwachia Uhuru anafanya Mambo ndivyosivyo.

Umewekeza pesa zako 100% ila uangalizi 10% tuwe serious kidogo.... Uangalizi ukiwa mbovu au muhudumiaji kuku akifanya uzembe kwakua haupo inapelekea kudumaa kwa kuku,Vifo vya Mara kwa Mara ,Uzembe wa kuwapa chanjo,banda kuwa chafu,magonjwa kila kukicha, kupewa report za uongo,kuibiwa kuku ata na mayai yake kwa kuuza n.k so ni muhimu unapotaka kuanza kufuga kibiashara ujitahidi uwe available kwenye eneo lako la ufugaji.

Sijamaanisha kama tusiajiri vijana hapana Ila wengi wao sio waaminifu na ata ukimpata kijana sahihi uwepo wako sehemu ya kufuga ni muhimu sana hii itasaidia kujua hali ya kuku wako kwa kuwaona direct tofauti na mtu anayeendesha shughuli za ufugaji kwa simu

INAENDELEA

1624551495661.jpg
 
2.COMMITMENT(Kujitoa)

Hakuna mafanikio yoyote hapa duniani ambayo yanakuja kirahisi bila mtu kujitoa na kuchukua maamuuzi magumu...

Ufugaji wa kuku ni kama biashara zingine bila kujitoa uwezi fika popote.. Sikutishi ila nakuambia ukweli hakuna mafanikio bila uvumilivu na subra ata kwenye vitabu vya dini vinatuambia tuwe wenye subra.

Unamtembelea mfugaji unamkuta na kuku broilers wamekua wakubwa wanaelekea kuuzwa ukiwahesabu unagundua ni kuku 1,000 kwa haraka haraka unachukua simu mfukoni au kwenye beg unazidisha idadi ya kuku mara 6,000 bei ya sokoni unapata milioni 6(6,000,000) haraka haraka bila kujua kapitia changamoto zipi mpk kufikia hapo unaenda kununua vifaranga 1,000 chap my friend utakuja kuchukia ufugaji bila kujua makosa ni yako mwenyewe na sio ufugaji...

Unapoanza kufuga jitoe kweli kweli weka imani kuwa hawa kuku ndio ajira yangu,,hawa kuku ndio watanisaidia kuendesha familia yangu,,hawa kuku ndio kila kitu kwangu even if utakua na ajira nyingine aisee ukifanya kazi ya ufugaji kwa kujitoa kama unavyojitoa wakati unafanya kazi za watu amini utashinda

Commitment kupokea changamoto zozote utazokumbana nazo usiwe mtu wa kulaumu laumu sana ila jitahidi kuwa mtatuzi wa changamoto naimani utashinda na ipo siku utakuja kuwa mfugaji mkubwa hapa nchini.

INAENDELEA......
 
3.PASSION (Shauku)

Unapotaka kuanza kufuga make sure unakua na shauku ya kitu unachotaka kufanya.Anza kuwapenda kuku ,penda ufugaji wa kuku,ondoa negativity kutoka kwa watu wanaosema ufugaji mgumu Mara haulipi ww jiandae kuwa na hamu ya kufanya unachopenda

Ukiwa na PASSION utajikuta unakua bize na mradi wako pale unapoanza kwasababu utakua na shauku ya kutaka kuona Jinsi unavyofanikiwa

Watu wengi tumekua na hamasa pale tunapokuwa na mawazo ya kuanza kufuga baada ya kujua faida zake..mwanzo unakua moto sana ila baada ya mradi kuanza unajikuta ile hamasa&shauku uliyokuwa nayo kabla ya kuanza unaiacha.... Sijui unanielewa rafikiii...????

Hamasa ikishuka love ya project inashuka twende kwa mfano:
=unapoanza mradi mwanzoni unakua na passion ya kuwa karibu na mradi wako,mda mwingi unashinda kuwaangalia,ukilala ukiamka unawaza kuku tu but zinapoanza kutokea changamoto let's say za magonjwa,kuku kuanza kufa hapo wengi unakuta anaanza kurudi nyuma bila kujua mda huo kuku ndio wanakuitaji sana kuliko kipindi chochote...
=Baada ya kuku kukua huwajali tena,bandani unaonekana Mara chache unamwachia kijana tu aisee utakuja kushindwa kumbe kosa lako mwanzo ulianza vizuri ila mwishoni ukamalizia vibaya

Tuwe na PASSION ya mifugo yetu pale tunapotaka kuanza na baada ya kuanza.....
#Life begins where fear ends#
INAENDELEA.....
 
4.LOCATION (sehemu ya kufugia)

Muhimu unapotaka kuanza kufuga angalia sehemu unayotaka kufuga unaweza jiuliza maswali yafuatayo:-
=Je..?? Vip kuhusu huduma ya barabara,maji na umeme..
=Je wafugaji walionizunguka wanafuga zaidi kuku aina gani km wanafuga broilers mm ngoja nifuge layers niuze mayai
,,,wafugaji walionizunguka wanafuga zaidi chotara mm ngoja nifuge kienyeji
,,,,maeneo niliyopo watu wanafuga sana kuku wa mayai mm ngoja nifuge chotara kwaajili ya kuuza kuku wa nyama n.k
Ni vyema kujua location uliyopo na market ya hiyo sehemu hii itakuepusha kufuga kuku ambao ukija kwenye soko unapata shida kuuza kwa wakati inaweza ikakurudisha nyuma na kukataa tamaa...

Hakikisha location yako inakua rafiki na ufugaji wako jenga banda sehemu nzuri kuepuka changamoto zisizo za lazma

#life begins where fear ends)
INAENDELEA.......
 
5.RESOURCES (Rasilimali)

Waoo tunamalizia sehemu ya 5 baada ya hapa waiting kwa somo jipya
RESOURCES unapotaka kuanza kufuga hakikisha unajiandaa ata km kipato chako kidogo basi jiandae kutokana na level ya kipato chako,,,,

Maana yangu ni ipi unapotaka kuanza kufuga gharama za ufugaji zipo wazi kabsa
1.Ujenzi wa banda pamoja na vifaa vyote kwa ujumla mf vyombo vya chakula na maji n.k
2.chakula cha kuku
3.kuku wenyewe
4.Chanjo mbalimbali
Sasa unakuta mtu anaanza kufuga kisa tu kajenga banda hapa banda peke yake alitoshi kuwa mfugaji

Mfano kuku aina ya layers yaan kuku wa mayai wao ukianza kufuga inachukua almost miezi 5 mpk 6 kuanza kutaga kwahyo kwa kipindi hiki chote hakuna utakachokuwa unakiingiza zaidi ya pesa kutoka tu Je...??? Umejiandaa vipi na kulisha kuku miezi yote hyoo????

Kwahyo unapotaka kuanza kufuga jiandae na vitu muhimu km kuandaa chakula ili unapoanza kufuga iwe rahisi kwako,,, unaweza nunua mazao kipindi cha mavuno kwa bei rafiki ukaweka store... Sio lazma kununua chakula cha dukani unaweza nunua nafaka kutoka kwa wakulima na ukatengeneza chakula chako cha mifugo kwa bei cheee

Angalia mfuko wako na anza kufuga kutokana na kipato chako
Mfano unaweza kuanza na broilers ambao utawalea ndani ya week 4 wanakua tayari kuingia sokoni ukafanya hivi ili kukuza mtaji wako,,, ukiona hii uwezi bhasi unaweza ukaanza kufuga kuku wa kienyeji kwa kununua rika ambalo tayari limeanza kutaga ili usitumie nguvu kubwa sana ni kitendo cha kuwa chukua na kuanza kufuga baada ya mda mfupi wanataga na kuanza kutamia,, final km upo vizuri unaweza anza na kuku wa mayai au ata chotara ukafuga

Muhimu anza kufuga kutokana na uwezo wako usiforce kufanya vitu oversize utakuja kufail mchana kweupe...

MWISHO

Tucheki Instagram #domcityfarmingcenter# KWA MASOMO ZAIDI au Facebook #Domcity Center#
Au tucheki WhatsApp free wa.me/0656626173
KARIBUNI SANA
 
Ujengewe mnara wa kumbukumbu pale Chato kaka.. shukrani sana
 
Binafsi mleta uzi nakubaliana na wewe.
Ni kweli changamoto ya vijana wa Kazi ni kubwa sana. Nina vifaa vyote vya kufugia kuku hadi mashine za kutotoleshea vifaranga 3000 kwa mwezi lakini kwa miaka 5 nimeshindwa kuvifanyia Kazi kwa sababu ya usimamizi.

Ila sasa nimeamua kijana nitakae mpata nitaingia nae makubaliano ya kumpa Kati ya 20%-30% ya Faida nje ya mshaara wake nione kama hii kero naweza kuikabili.

Kqa upande wa location sehemu ninayotaka kuweka huu mradi kama nikifanikiwa kukuza kuku 1000 ndani ya miezi 3 au 4 naweza kutengeneza 10M profit

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Kila la kheri ndugu
 
Back
Top Bottom