Mambo ya kuyazingatia ili kumuaminisha mwanamke

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Ni kweli mapenzi kila mja upenda kwa kigezo chake cha kihisia na kiutashi, kubaki mtu au kuondoka kwa mpenzi wake ni suala linalohitaji kila mtu atimize wajibu wake katika mapenzi na ndoa.

Kwa maarifa ya jumla kuna mazingira, vitendo, hali na mawasiliano yanayochangia kwa kiasi kikubwa kujenga mchakato wa akili kwa jinsia zote katika mahusiano, mapenzi na ndoa. Kwa kuanza na wanaume kuna haya ambayo wanapaswa kuyasimamia ili kujenga akili na hisia za mwanamke:

1. Simama katika jinsia yako. Unapokuwa nae hata iweje baki kuwa mwanaume iwe kwenye raha ama shida. Mwanaume unaposhindwa kuwa jasiri katika gumu au jukumu, hata mwanamke wako huwa dhaifu zaidi, unaposhindwa kumridhisha kimapenzi na ukawa unachukulia poa, nae atakuchukulia poa pia ni lazima uoneshe tabia zako za kiume kwake kama uvaaji, kuongea, maamuzi, vitendo na mahusiano na wengine.

2. Mhudumie bila kuombwa. Iwe ni wajibu wako tena anza kwa shida ndogo ndogo za msingi.Wanaume wanafeli kwa kuwaza kufanya makubwa kwa wanawake wao, mitazamo ya pesa ndio hitaji kubwa kwa wanawake hii ni sumu. Tizama mwanamke wako anahitaji nini mpe iwe kingi ama kidogo kisizidi uwezo wako.

3. Mpe uhuru wa kuwa nawe mahali, kimawasiliano na kukushauri. Mapenzi ya kuchungwa chungwa na kutopewa nafasi wala kipaumbele ni mwiko. Kujifanya uko bize kumzidi Mungu ni kujichumia janga katika mapenzi.

4. Mshirikishe kwenye utafutaji wako wa riziki. Sio lazima ajue kila kitu ila angalau asilimia 80% hii inafanya aone mko pamoja naye pia ajitoe kwako kiuchumi nk. Yanini umfiche ikiwa umemtongoza mwenyewe na tena umemuaidi kudumu nae maishani.

5. Jali ndoto zake. Kitu anachotamani kukifanya msaidie, mshauri na kama unaliweza mfanyie, usimfanye aishi kama moto kwako. Geuza wazo lake liwe fursa/pesa/biashara au basi chochote hata kwa kuonyesha tu nia.
6. Tumia ngono kama kiunganishi cha hisia na mkiwa mmekaa kwa muda kiasi usione aibu kuzungumzia utupu wake, utamu wake, utundu wake unapokuwa nae faragha au kwenye meseji au mnapopigiana simu. Msichana / mwanamke huwa anajengeka zaidi mtu anapozungumza yanayomhusu ndani.

7. Penda watu wake wa karibu. Acha kujitenga wala kuonyesha upendi awe na mahusiano na watu wengine kama marafiki, ndugu zake na familia yake. Hao ndio washauri wake, hakimu zake na pia ndio watao kusaidia kumtambua hulka zake usizozijua.

8. Usionyeshe kumchunga sana. Umpa mashaka kuwa haumuamini kwa kiasi fulani.

9. Kuwa mkali unapofanyiwa yasiofaa, ila tafuta sehemu sahihi ya kuzungumza nae. Mwanamke upenda kusikiliza ila sio kwa kudhalilishwa au kufanywa kama pimbi asiye na maarifa ya kujua zuri na baya.

10. Usiache kumpa zawadi. Zawadi uonyesha kumjali, umlingamishi, hujamsahau, unampa thamani na uko tayari kumtetea maisha yake. Kilicho bora utunzwa.

Ikiwa kweli una tamani kudumu naye uliyemtongoza basi huna haja ya kuyakwepa majukumu yako kama mwanaume, ukweli utabaki kuwa mwanamke upenda kubebembelezwa na kuhudumiwa kama mtoto.


20221031_100106.jpg

 
Maelezo yake yote anamaanisha MAPENZI BILA PESA NI KULALIA UPUPU..TUTAFUTE HELA WAKUU
Hapana, pesa ni fikra za mtu kuyatazama mapenzi. Ingelikuwa hivyo tusinge zaliwa maana unaweza tazama familia yako au ya jirani yako, hawana hizo fedha unazowaza( lundo).
Nafanya ushauri katka mahusiano kuna watu nakutana nao wanapesa ila wanashida katika mapenzi, na wamehonga tayar ndoto za watu( vitu unavyowaza kuvimiliki wamewahonga wapenzi wao) na hawana mapenzi.
 
Tafuta pesa.
Ukiwa nazo huna haja ya kujieleza saana.
Kumbembeleza na kumpa zawadi haimaanishi hatagongwa.
Adamu alihonga mbavu za mwili wake lkn bado alisalitiwa.
Kijana mimi babu yako nakuambia, usipoteze muda wa kutaka kuwaridhisha hawa viumbe, tafuta pesa ukijua kakusaliti piga chini, tafuta mwingine atakayekusaliti siku zijazo.
 
Hapa ndio utajifunza ni bora uwajibike #abiria chunga mzigo wako#
 
Sasa kama hajui mambo yako mtu akifariki si utasumbua familia sasa?Kwa Sababu vitu vinakuwa havieleweki.
Nalo ni tatizo, unapo oa ina maana upo na mtu wa kwanza kukutazma maisha yako na kukusaidia, hakuna viumbe wenye huruma na uvumilivu mkubwa kama mwanamke, na kama analengo la kukuua ni haraka sana hata uwe komando wa cheo cha mwisho lakin wanaish wakivumilia mifumo dume, unyanyasaji na wanaficha mapungufu mengi ya wanaume zao.
Kwahiyo, kuweka waz maisha yako kwake ni kujenga upendo na watoto wako.
 
Back
Top Bottom