Mambo ya kuyaepuka kwenye gear box ya Automatic

Habari mkuu, gari yangu aina ya vitz old model nikiliwasha nikiingiza gear D halichanganyi kuondoka hapo hapo ina delay kama sekunde kadhaa ndio inakubali hata ukikanyaga mafuta haliondoki ukilazimisha kukanyaga zaidi mafuta linafanya kushtuka sana..

Yaani mpaka baada ya muda wa sekunde kadhaa ndio linakubali kuondoka, nkiweka R inachanganya vizuri hapo hapo lakini D tu ndio hutokea hivyo mara chache, je sababu itakuwa nini kwa ujuzi wako mkuu? Tatizo linaweza kuwa la gear box au engine?
 

Hilo ni tatizo la gearbox na linarekebishika.
 
Hapa labda ni baina ya D na R. Ila kuanzia L kwenda D, sijaona tatizo, mana kuna kipindi flani ivi nilikuwa niko moto kwenye mambo ya kwenda mbio, naweka L navuta mpaka 60 naweka 2 navuta mpaka 120, naweka 3 navuta mpaka 180, naweka D inaendelea mbele tu.

Sikuwahi kupata tatizo kwenye gearbox hadi leo hii, na hio ni miaka kama 5 nyuma iliopita kitendo ambacho nlikuwa nafanya karibia mara nne kwa wiki kwa miaka miwili mfululizo.
 

Anyway labda kuna kitu sijakiweka sawa kwenyw maelezo yangu.

Hizi gear yaani L, 2 na 3 zina limit zake za speed. Na changamoto kubwa ambayo inaweza kuharibu gearbox ipo wakati wa kupunguza gear. Kama upo kwenye max speed ya namba 3 na ghafla ukashift kurudi 2 au L bila kupunguza speed, Haitakuchukua muda utanunua gearbox nyingine.
 

Siku moja sijui ata nlikuwa na mawazo gani, nimeingia kwenye gari, ile napiga starter tu sikusubiri ata iwake nikajikuta nishaweka D, ah nikaweka neutral nikawasha tena, nikaondoka zangu nipo kwenye 20km/hr ivi mkono nilikuwa nimeuweka kwenye gear knob kwa bahati nikajikuta nimeipush mbele mpaka kwenye reverse, ebana we ule mshtuko nlouhisi apo kwenye engine na gearbox yani sikuchelewa kuirudisha D afu kusimama na kuanza kujaribu gear zote kama zinabadilika bado au zote zishakuwa Neutral!

Ukitoka kwenye max ya 3rd Gear urudi 2nd gear mzee unaweza kujikuta wewe na body mmetangulia mbele na kuiacha gearbox na mashine yake nyuma 😀 Yaani hio ni apo apo tu safari imefika mwisho.

Ivi Automatic tulokuwa nazo zina safety ya kutoka D kwenda R? kwa mfano kama upo speed kubwa itaingia Reverse gear au itakugomea? Sijawahi kujaribu mpaka nipate gari ambayo najua hii inataka kuvunjwa tu ndio nijaribu hilo.

Manual najua kama upo kwenye mwendo mkubwa ukiipeleka kwenye reverse inakugomea kuingia, sijui Automatic.
 

Gearbox za sasa za automatic haikubali utoke D kuja R kama unatembea. Ila za zamani inawezekana. Ila ndo hivyo unasaga vitu. Na ukifanya hivyo mara mbili tatu utakuwa huna chako siku si nyingi.
 
Umezingatia ushauri
 
Hata ukitoka D kuja 2, 3 n.k. kama gari inatembea. ni majanga. Gearbox automatic ni kama mayai tu...

Japo ukiitunza inakaa
Nilishafanya hvyo kwenye mlima mkali shaft ya kulia ikakatikia kule kwenye cv joint, ndo nikajifunza kuanzia siku hyo gari ikiwa inatembe hasa ikiwa inatumia nguvu kubwa sitakiwi kushift gear, maana nilizoeaga sana hako kamchezo kakupanda na D kwenye mlima halafu nikiona kama inataka kushindwa natupia 2.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Aiseew pole... Inaonekana ulikuwa mwendo mkali.
 

ni hivi mfano unarudi nyuma halafu uende mbele upo kwenye gea ya R maana yake rivas wwkati unarudi hapohapo ukaweka gea D drive iende mbele huku bado inarudi nyuma haijasimama kwanza kanyaga breki gari isirudi nyuma uweke hiyo D wakati limesimama
 
Umechanganya, mtoa mada hazungumzii Bodaboda, yeye anaelezea gari. POLE!
 
Huwa natumia N kwenye foleni kali au kwenye mataa.

Kukanyaga break muda wote inachosha.
Na ukumbuke ukiweka N bila kugusa brake gari ina move kulingana na uelekeo wa barabara kama ina kimteremko hivyo swala la brake kwenye folen haliepukik vinginevyo buti za wenzio zitakuwa halali yako au labda pawe tambararw kabisa kwamba hata ukiweka N Gari ibaki hapo hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…