Mambo ya kushangaza kuhusu facebook mwaka 2022

Mambo ya kushangaza kuhusu facebook mwaka 2022

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,221
Reaction score
2,425
Facebook bhana Ina mambo mengi sana ya kushangaza ambayo watu wengi walikua hawajui kha wanaweza kuyafanya kwenye Simu zao.

Wageuze marafiki kuwa followers
hivi unafahamu Facebook wameweza kuweka kipengele Cha kugeuza watu wanaokuomba urafiki kuwa followers wako Yani mtu mtu akitaka kumuomba urafiki atakutana na neno follow him / her . fanya hivi
ingia Facebook>> setting & privacy >> public post >> who can follow me >> weka public

Wajue watu gani wanatumia akaunti yako
ukitaka kujua kama akaunti unayotumia huko pekee yako au mko wengi mnaotumia fanya hivi ingia setting >> security & login utaweza kuangalia ni vifaa vingapi vinatumia akaunti yako ya Facebook.

Ongeza ulinzi kwenye Facebook yako
kama akaunti yako ni biashara ni muhimu kuongeza ulinzi wa akaunti yako ili kutoweza kuibiwa akaunti yako . ingia setting >> privacy & security > Enable two factor authentication kwa kuweza kupata code Kila unapotaka kuingia kwenye akaunti yako.

Unaweza kuset nani wa kuangalia post zako
Facebook wametuletea maujanja ya kuweka kuweza kuset nani wa kuangalia post zako kwa kuweza kuchagua everyone , friends, friends of friends, or just specific people. Hivi unaweza ukachagua restrict picha zako mtu asione mpaka utapoweka public.

Angalia ni kwa kiwango unatumia sana Facebook
fb wametuletea njia rahisi ya kuweza kuangalia ni kiwango gani Cha muda unatumia sna kwenye Simu yako. fanya hivi ingia kwenye Facebook yako >> Kisha gusa kwenye mistari mitatu >>setting & privacy > your time on Facebook.

Pakua taarifa zako za Facebook
unahitaji kupata taarifa zako zote kuhusu picha ulizo share fb , video , message ulizotuma na kutumiwa uweze kuwa nazo fanya hivi ingia setting >> Facebook your information>> download your info.

Chagua Mtu wa kutumia akaunti yako baada ya wewe kufa
inaonekana kama jambo la kushangaza ila ndo uwalisia Kila mtu atakufa. Facebook wametuletea njia ya mtu kuendeleza akaunti ya mtu aliyekufa fanya hivi ingia setting >> general >> memorization setting > edit on desktop Settings > Personal Information > Manage Account Kisha chagua legacy contact.

Ebu tuambie ulikua unajua hayo au ndo tunakujuza tuachie maoni Yako ?

Teknolojia ni Yetu Sote

#bongotech255
 
sasa mkuu mbna hayo mambo yote yapo zaidi ya miaka 7 nyuma na zaidi huko iliyopita
iweje wewe utuambie mapya ya 2022 labda hilo la kubadili kuwa followers ndio la miaka ya hivi karibuni
hakuna jipya mkuu la 2022 labda wewe tu ndo umechelewa kufahamu
 
Kama unatumia Facebook lite bonyeza link hii

Italeta waasili wako (your contact) hapo kutakuwa na majina. Hivyo bonyeza jina husika namba itaonyeshwa na unaweza kuikopi.

Ukibonyesha link hiyo telemka mwisho utakuta jina na namba nne za mwisho.

Mfano
Kasomi (...6790)
Mr. Genius (..7647)
Hivyo utabonyeza jina husika na namba ita display full

Mfano
Kasomi 07123456790
 
Mambo hayo yote yalikuwepo Toka zamani labda wewe ndio umeyaona mwaka huu
 
Kama unatumia Facebook lite bonyeza link hii

Italeta waasili wako (your contact) hapo kutakuwa na majina. Hivyo bonyeza jina husika namba itaonyeshwa na unaweza kuikopi.

Ukibonyesha link hiyo telemka mwisho utakuta jina na namba nne za mwisho.

Mfano
Kasomi (...6790)
Mr. Genius (..7647)
Hivyo utabonyeza jina husika na namba ita display full

Mfano
Kasomi 07123456790
Mbona naomba zingine hazioneshi majina
 
Back
Top Bottom