MAMBO YA KUJIVUNIA KWA RAISI MAGUFURI MWAKA 2017

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,583
9,666
Kuna siku mheshimiwa raisi alilalamikia watumiaji wa mitandao kuwa watu wa kukosoa kilakitu kana kwamba hakuna zuri hata moja lililokua likifanywa na serikali yake, Kwa kiwango fulani alikua sahihi, pamoja na yale tusiyokubaliana nayo lakini kuna mambo mengi mazuri yaliyo washinda watangulizi wake yeye ameyafanya kwa muda mfupi sana, kwa mambo hayo anastahili pongezi. Baadhi ya mambo ninayompa hongera JPM ni
  • Uwajibikaji kwa watumishi wa umma, japo bado safari ni ndefu lakini kuna afadhari siku hizi ukienda kutafuta huduma dharau za kijinga na uvivu umepungua kwa watumishi
  • Ujenzi wa miundombinu, kuna project nyingi zinaendelea za ujenzi wa barabara na miundombinu ya maji, kuna baadhi ya maeneo ya dar maji ya bomba walijua hawayajui kwakua yaliku yanapelekwa maeneo ya "wazito" tu enzi za JK. Pia kuna reli ya SG
  • Thamani ya shilingi, wengi wanaweza kuchukulia poa hili lakini JPM amejitahidi sana kadhibiti kuporomoka kwa thamani ya fedha yetu, mwishoni mwa 2015 usd 1 ilikua TSh 2171.84 leo hii mwishoni mwa 2017 usd 1 ni sawa na 2236.75. Kwa nchi inayoagiza bidhaa kwa wingi kama yetu ni kweli kwamba JPM amefanya vizuri.
  • Sheria mpya ya madini na gesi, japo tumeshaibiwa sana (kutokana na madudu ya BWM na JK) walau kwa sasa tuna sheria atayoleta tija kwa nchi. Faida inaweza isionekane leo au kesho lakini kwa mipango ya muda mrefu tutafaidika (hususani katika gesi)
  • Kuondoa uswahiba na wapiga 10% serikalini, serikali iliyopita kulikua na uswahiba na kipigiana mapande kuliko kithiri
  • Elimu bure, japo inaweza kuwa ni elimu isiyo na ubora kwa sasa lakini elimu bure ni uthubutu wa hali ya juu katika kuwekeza kwenye elimu. Miaka 10 ijayo tanzania itakua na kundi kubwa la watu wenye elimu angalau ya kidato cha 4
  • Usawa katika ajira serikalini. Japo zimetolewa kiduchu lakini zimetolwewa kwa haki na bila upendeleo, mfumo unaotumika bado ni mpya hivyo bado kuna changamoto kadhaa lakini ni mwanzo mzuri wa kuondoa ukabila kwenye baadhi ya mashirika na taasisi za umma
Unaweza kuongezea lolote zuri alilofanya JPM na serikali yake
 
Back
Top Bottom