Vijana wanaougua saratani ya njia ya haja kubwa waongezeka
WANAFUNZI wa sekondari wa kike na kiume ni miongoni mwa wagonjwa walioathirika zaidi na saratani ya njia ya haja kubwa wanaofika katika taasisi ya saratani ya Ocean Road.
Akichangia mada kuhusu ugonjwa wa saratani ya tezi ya kibofu cha mkojo iliyotolewa na Dk. Ali Mzige, Dk. Dominista Kombe ambaye ni daktari bingwa wa saratani kutoka taasisi hiyo, amesema mbali na wanafunzi, wagonjwa wengine ni vijana wasiokuwa na kazi ya kufanya.
Sasa hivi vijana wa kati ya miaka 20 na 30 ndiyo wengi wanaokuja hospitalini tena inasikitisha unakuta wameharibika sana, alisema Dk. Kombe.
Alisema kwa uzoefu kwenye kliniki ya saratani, wastani wa vijana wa umri huo kati ya mmoja na watatu hufika kila wiki wakiwa na saratani hiyo tena wakiwa wamesharibika sana.
Inabidi tufanye utafiti kujua sababu ya vijana wetu kuathirika na saratani hii. Inaumiza unapopokea vijana wanakuja wameweka vitenge sehemu ya nyuma wengine wanavaa skin tight tatu, alisema.
Hospitali hiyo ambayo ni maalumu kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa saratani nchini kwa wiki hupokea wagonjwa wapya wenye saratani za aina mbalimbali kati ya 30 na 60.
Aidha tangu Januari mwaka huu mpaka sasa imeshapokea wagonjwa wenye saratani za iana mbalimbali wafikia 3,084.
Awali Dk. Mzige aliyewakilisha Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) alisema kujamiana kinyume na maumbile kwa wanawake kunawasababishia saratani ya njia ya haja kubwa na wanaume hupata saratani ya uume.
Naye mkufunzi wa saratani kutoka Chama cha Madaktari Wanawake (Mewata), Dk. Maryrose Giattas, alisema sasa hivi vijana wengi wanajihusisha na kujamiana na kinyume cha maumbile.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Hii ni tahadhari kwa wale wanaopenda kuji-express, maana madhara hayo kwa wale wanaokwenda kinyume na maumbile tu, bali hata kwa wanaume.
Generation yetu inaelekea kubaya