Mambo ya kudanganyana ya nini?

Mambo ya kudanganyana ya nini?

Mwanapropaganda

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
4,235
Reaction score
2,512
Barabarani tunapishana na watu mbalimbali, kazini, shuleni/vyuoni, kwenye sehemu za burudani, safarini nk ambao wamebeba siri nyingi binafsi ambazo kwa mtu aliye jirani yake hawezi kujua kinachoendelea kwa mwenzake.

Nakumbuka alichosema mkuu KikulachoChako kwenye uzi mmoja kuwa kama matumbo yetu yangekuwa yana kioo basi mambo yangekuwa tofauti sana maana utakuta mtu kala karanga mbili tu na maji halafu anaonekana mjanja na watu wanaamini hivyo.

Hayo ni maelezo tu yanaweza kutufundisha kwa kutufikirisha hata kwenye upande mwingine wa maisha hususani kwenye mapenzi. Yapo mambo mengi kuwahusu watu tunaotaka kuanzisha nao mahusiano ya kudumu kwenye safari ya mapenzi lakini hatufahamu mambo yao.

Kuna wakati unaweza kusema kuwa mwanaume/mwanamke mwenye tabia fulani siwezi kuishi naye, lakini kwa sababu au kwa mfano wa maelezo hapo juu unakuta mtu wako wa karibu ana kasoro hizo ila kwa sababu fulani wewe unakuwa huzioni na siku ukija kuziona unapunguza au kukata mawasiliano haraka.

Mfano unakutana na binti hotelini au hata shopping centers kama Mlimani City nk, ukavutiwa naye kutokana na muonekano wake ukashawishika kumtokea akakubali, binti ana labda aliwahi kupata majeraha kichwani hivyo akaamua kuvaa wigi, ili kuficha hitirafu yake, siku ya siku ukaja kumuona katika uhalisi wake unaamua kumpiga chini.

Unatafuta mwingine, huyu unamkuta ananukia manukato hatari, kila siku unasikia hivyo, siku ya siku hajajipulizia manukato unakuja kugundua kuwa ni mchafu sana, ananuka na alikuwa anatumia hayo ili kukudanganya wewe na wengine aonekane tofauti na alivyo lakini ukweli wanaujua wao.

Kufikia hitimisho hili ndipo naona haja ya watu kuwa kama walivyo, kama una tatizo la kudumu ni bora usilifiche kwa kuvaa wigi au kucha bandia kwa kuwa tu una kucha zilizoharibika au kuwa na mvuto mbaya, bora mtu akuone vile ulivyo alidhike nawe, au kama unajua tatizo lako ni kunuka kikwapa nk tafuta tiba ili hata siku ukikosa hayo manukato usiharibu hali ya hewa na kumfanya mwenzako akushangae na kukuhisi vibaya, pengine kuamua kukuacha.

Nimeyasema haya kwa kuwa sasa hivi imezuka tabia ya watu kujibadili kwa vipodozi kila siku na kujenga muonekano wa uongo/bandia unaovutia japo muda mfupi.

>Nywere bandia.
>Kucha bandia.
>Kope bandia.
>Makalio bandia.
>Lips bandia.

Haya yote yapo kwa ajili ya kuwapumbaza watazamaji na wasikilizaji.
 
Sijui kama utaeleweka na wadau tasnia hiyo.
 
Mbona umebase kwa akina dada tu? Hao wanaojfany sharo kumbe pesa za wazaz je? Hao wanaonuka midomo kutwa wanashnda na bigjii a.k.a jojo? Hao wanaovaa vitu vya bei kutoka mliman city kw pesa za wazaz huku hal chumban hawez hata piga dek wala kujfulia? Hao wahubirio injili huku wanaongozw na miungu bandia? Hao wanaojfany wanapesa z kutunza wake kumbe za kuiba kwenye mabenk na sehemu nyngine? Kuwa makin unapoandka uz. Mnatusema sana bas tuwaachie jukwaa.
 
Maisha ya dunia ya sasa kwa asilimia kubwa sana ni feki.
 
Mbona umebase kwa akina dada tu? Hao wanaojfany sharo kumbe pesa za wazaz je? Hao wanaonuka midomo kutwa wanashnda na bigjii a.k.a jojo? Hao wanaovaa vitu vya bei kutoka mliman city kw pesa za wazaz huku hal chumban hawez hata piga dek wala kujfulia? Hao wahubirio injili huku wanaongozw na miungu bandia? Hao wanaojfany wanapesa z kutunza wake kumbe za kuiba kwenye mabenk na sehemu nyngine? Kuwa makin unapoandka uz. Mnatusema sana bas tuwaachie jukwaa.

Ni akina nani nyiye mnaosemwa?
 
Back
Top Bottom