Wakuu,
Kuna baadhi ya mambo wanandoa wengi wamekuwa wakiyachukulia kuwa ni mambo madogo ila kiuhalisia ukiyafanya sio mambomadogo yafuatayo ni mambo saba yanayoleta mahaba katika ndoa.
1- Mtolee salaam mumeo/mkeo na umpe mkono kila anaporudi kutoka kazini au matembezini.
2- Muulize mumeo/mkeo unapenda nikuite kwa jina gani?Muite kwa jina alipendalo.
3- Jenga tabia ya kumpiga busu mumeo/mkeo mara kwa mara.
4- Kaa na mumeo/mkeo wakati wakula au kuleni pamoja.
5- Kilaukitoka matembezini mletee zawadi hata kama kidogo.
6- Wafanyie wema wazazi wa mumeo/mkeo kama unavyowafanyia wazazi wako.
7- Akipendeza mumeo/mkeo mwambie hongera/umependeza mume wangu/mke wangu na umbusu"ndoa idumu.
Tuma ujumbe huu kwa wanandoa kwani shetani amekazana kuvunja ndoa zetu.